ms_baruhila
New Member
- May 24, 2024
- 3
- 1
Utangulizi,
Katika ulimwengu wa sasa, vijana wana nafasi muhimu katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika jamii. Nchini Tanzania, vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya kama shisha, bangi, sigara na vilevi vingine, pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia. Ili kuweza kuleta maendeleo ndani ya miaka 5,10,15 mpaka 25 ijayo, ni muhimu kuelewa jinsi tunavyoweza kuwasaidia vijana kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi, huku tukiwasaidia kutumia teknolojia kwa manufaa yao na kwa taifa kwa ujumla.
Umuhimu wa vijana katika maendeleo ya Taifa
Vijana ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Tanzania. hii ina maana kuwa wao ni nguvu kazi kubwa ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya taifa. vijana wanapokuwa na afya bora, elimu nzuri na wanaotumia teknolojia kwa njia sahihi, wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. hata hivyo, changamoto kama vile matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi zinaweza kuathiri uwezo wao wa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Matumizi ya Madawa ya Kulevya na Vilevi
Ushirikiano Matumizi ya madawa kama bangi, heroin,cocaine na pombe kama Kvant, Kiwingu,Absolute vodka ni tatizo kubwa miongoni mwa vijana nchini Tanzania. tatizo hili linaathiri afya zao, uwezo wao wa kujifunza na kufanya kazi, na mahusiano yao na familia na jamii hivyo ili kuweza kuleta maendeleo, ni muhimu kuzuia na kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi miongoni mwa vijana. Hii inaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
• Elimu na uhamasishaji, elimu ni silaha muhimu katika kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi. Kampeni za uhamasishaji kuhusu madhara ya matumizi ya shisha, bangi, heroine pamoja na pombe kali zote zinapaswa kuimarishwa katika shule, vyuo na jamii kwa ujumla. Vijana wanapaswa kuelimishwa kuhusu madhara ya kiafya, kijamii na kiuchumi ya matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi, ni muhimu elimu hii kutolewa kuanzia shule za msingi kwani itapunguza madhara makubwa wanayopitia vijana asa vyuo vikuu na ndani ya jamii kwa ujumla.o
• Kuimarisha sheria na sera, serikali inapaswa kuimarisha utekelezaji wa sheria na sera zinazopinga matumizi na usambazaji wa madawa ya kulevya na vilevi. hii inajumuisha kuongeza juhudi za kudhibiti mipaka na kudhibiti usafirishaji wa madawa haramu. aidha, kuweka adhabu kali kwa wale wanaopatikana na hatia ya kusambaza madawa ya kulevya pamoja na watumiaji, kupiga marufuku matangazo ya vilezi asa pombe katika video na mabango, pia kupiga marufuku ya watu kutumia vilevi hivyo hadharani na mbele ya watoto.
• Huduma za afya na ushauri nasaha, kuwapatia vijana huduma za afya na ushauri nasaha ni muhimu katika kusaidia wale ambao tayari wameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi. Vituo vya afya vinapaswa kuwa na wataalamu wa afya ya akili na ushauri nasaha ambao wanaweza kuwasaidia vijana kujiepusha na madawa ya kulevya na vilevi, vilevile jamii haipaswi kuwabagua waathirika wa madawa na vilevi zaidi ni kua karibu nao na kuwasaidia, serikali ihakikishe pia inaongeza (sober houses) na kusapoti pia zilizopo ili kuwaokoa waathirika.
Teknolojia na maendeleo
Teknolojia ina nafasi kubwa katika kuleta maendeleo nchini Tanzania. Vijana wanapopata fursa ya kutumia teknolojia kwa njia sahihi, wanaweza kuleta mapinduzi katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, kilimo na biashara. Ili kuhakikisha teknolojia inaleta maendeleo chanya, hatua zifuatazo zinapaswa kuchukuliwa:
• Elimu ya teknolojia, vijana wanapaswa kupatiwa elimu ya teknolojia kuanzia ngazi za chini za elimu, Serikali na wadau wengine wanapaswa kuwekeza katika vifaa vya teknolojia katika shule na vyuo na programu za mafunzo ya teknolojia zinapaswa kutolewa ili kuwasaidia vijana kupata ujuzi na maarifa ya kiteknolojia, vijana wanapaswa kufundishwa njia sahihi ya matumizi ya kimtandao toka chini ili waweze saidika na teknolojia ya mitandao kama Instagram, twitter(X) na Facebook katika kujiingizia kipato na si kutumia mitandao kwa matumizi yasiyo na tija.
• Ufikiaji wa teknolojia, ni muhimu kuhakikisha kuwa teknolojia inawafikia vijana wote, bila kujali maeneo wanayoishi. serikali inapaswa kuwekeza katika miundombinu ya teknolojia vijijini na mijini ili kuhakikisha vijana wanapata huduma za intaneti na vifaa vya kiteknolojia kwa urahisi zaidi, pamoja na kuhakikisha inasimamia masuala ya manunuzi ya vifurushi vya mitandao ni rafiki kwa kila mtanzania kununua na kutumia.
• Kuhamasisha uvumbuzi na ubunifu, serikali na sekta binafsi zinapaswa kuhamasisha uvumbuzi na ubunifu miongoni mwa vijana, mashindano na programu za kuhamasisha vijana kubuni na kutengeneza teknolojia mpya zinapaswa kuanzishwa, hii itasaidia vijana kuwa wabunifu na kutumia teknolojia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, hii itaenda sambamba na kuondoa pendekezo la tozo kwa wabunifu wa kidigitali au kimtandao kwani hii imekua hajira kubwa kwa vijana hasa wakati huu ambao vijana wanakabiliwa na ukosefu wa ajira.
• Kukuza ujasiriamali wa kiteknolojia, teknolojia inatoa fursa nyingi za ujasiriamali. vijana wanapaswa kuhamasishwa kuanzisha biashara zinazotumia teknolojia, kutengeneza maudhui tofautitofauti kama kutangaza bihashara na mengineyo. serikali na taasisi za fedha zinapaswa kutoa mikopo na ruzuku kwa vijana wajasiriamali ili kuwasaidia kuanzisha na kukuza biashara zao pia.
Ushirikiano na uwekezaji
Ili kufanikisha malengo ya maendeleo kwa kutumia teknolojia na kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi, ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii kwa ujumla ni muhimu. serikali inapaswa kuunda sera na mikakati inayohimiza uwekezaji katika teknolojia na elimu ya vijana. sekta binafsi pia inaweza kusaidia kwa kutoa fursa za mafunzo na ajira kwa vijana, mashirika yasiyo ya kiserikali yanaweza kusaidia katika kutoa elimu na huduma za afya kwa vijana walio athirika na madawa pamoja na vilevi na ambao hawaja athirika pia ili kulinda na kutengeneza taifa bora la kesho.
Hitimisho
Vijana wa Tanzania ni rasilimali muhimu ambayo inaweza kuleta maendeleo makubwa ndani ya miaka 5,10, 15 adi 25 ijayo, ili kufikia malengo haya ni muhimu kuwekeza katika elimu, kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na vilevi, na kuhakikisha vijana wanapata fursa za kutumia teknolojia kwa manufaa yao na kwa taifa kwa ujumla. kwa kushirikiana na kuweka mikakati madhubuti, Tanzania inaweza kufanikiwa kuleta maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya vijana na jamii kwa ujumla.

Attachments
Upvote
3