bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Vijana Morogoro waikubali na kuisifia Katiba inayopendekezwa. Vijana Mkoani Morogoro wamesema kuwa Katiba Inayopendekezwa ni nzuri sana kwani imewajali vijana hata masuala yao ya michezo. Kutokana na kuikubali Katiba Inayopendekezwa wanawaomba vijana wenzao kote nchini kuipigia kura ya NDIYO. Huu ni ukweli usiopingika kuwa Katiba hii imejali makundi karibu yote. Hima vijana endelea kuisoma katiba kwa makini zaidi ili unapopiga kura yako ya ndiyo upige kura yako kwa uelewa. Tunaishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutuongezea muda wa kuisoma na kuielewa vizuri kabla ya kupiga kura ya maoni.