BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mkulima Mjasiriamali wa Kilimo cha Parachichi Katika Kijiji Cha Igoda Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Aidan Kiwale amewataka vijana kutoka mazingira magumu ambao wapo kwenye mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) kuchangamkia fursa ya Kilimo cha Parachichi kwa kuwa kinalipa.
Mkulima mdogo wa Kilimo cha Parachichi Kijiji cha Luhunga Wilaya ya Mufindi Mkoani, Iringa Aidan Kiwale akitoa mafunzo ya Kilimo cha Parachichi kwa vijana wa Mradi wa Youth Agency Mufindi.
Kiwale ametoa rai hiyo Machi 29, 2022 wakati wa mwendelezo wa Mafunzo ya Siku 10 ya Ujasiriamali yanayoendeshwa na Halmashauri ya Mufindi Kwa kushirikiana na mradi wa YAM pamoja na Taasisi ya Foex Community and Wildlife Conservation (FCWC).
Amewataka vijana waache kukaa vijiweni na badala yake kutumia vizuri muda kwa kufanya kazi za kilimo na nyingine za ujasiriamali ambazo wakizingatia zitawatoa katika dimbwi la umasikini wa kipato.
Awali akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoanza Kiwale ambae ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji Kijiji Cha Igoda amesema mwanzo wananchi hawakumuelewa na walikuwa wakimuona kama amepitwa na wakati ila sasa kila mmoja anamuonea wivu kwa pesa nzuri anayopata kwenye kilimo cha parachichi.
Alisema kuhusu soko la parachichi ni zuri kwani soko dogo la parachichi kwa ajili ya kusafirisha kwenda nje ya nchi lipo Mkoani Njombe na kuwa kwa mkulima mwenye uwezo anaweza kusafirisha mwenyewe kwenda kuuza nje .
Hata hivyo, akishukuru kwa elimu hiyo mshiriki Fex Kitinusa amesema elimu hiyo ni mtaji kwao na watakwenda kuitumia.
Sadick Ngwiso Mkazi wa Kijiji cha Luhunga Kitongoji Cha Igoda Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa akigema Ulanzi.
Halmashauri ya Mufindi chini ya Taasisi ya FCWC ndio watekelezaji wa mradi huo, Youth Agency Mufindi kupitia ufadhili wa Finland ni mradi wa miaka minne utakaowafikia vijana 770 pamoja na watoto kwenye vijiji 16 vya kata za Luhunga , Mdabulo na Ihanu.
Chanzo: Matukio Daima Blog