amranik
Member
- Sep 13, 2019
- 17
- 15
VIJANA NA AFYA YA AKILI
Kijana anatakiwa awe na afya ya akili kwa ustawi wake na jamii kwa ujumla. Afya ya akili nii hali ya kuwa sawa kiakili na kisaikolojia au kutokuwepo kabisa kwa usumbufu wa akili ya mtu, mfano msongo wa mawazo.
Kuwa na afya ya akili itakuwezesha kuhimili mabadiliko yoyote yatakayo tokea wakati wowote, yawe ya kisaikolojia au kijamii. Afya ya akili ndio nyenzo kubwa ya mafanikio ya mtu yoyote kwasababu bila ya kuwa na afya ya akili huwezi kutoa maamuzi endapo kutatokeo tukio usilolitarajia na itapelekea kuwa na msongo wa mawazo na matokeo yake unaweza kujishambulia au kushambulia wengine na kuhatarisha maisha.
Katika jamii ya sasa watu wengi wanaonekana ni wazima na timamu lakini wamekosa afya ya akili, hii inapelekea ongezeko kubwa la vitendo vya kikatili na ukatili kwa ujumla. Matukio ya kujeruhiwa au kuuawa kwa watu katika jamii yameendelea kushamiri na sababu ni upungufu au ukosefu wa afya ya akili.
Mtu anashindwa kudhibiti hisia zake pale anapohisi kutendwa au kusalitiwa na mke au mume wake na kupelekea kufanya ukatili, baba anashindwa kuwa na tafakuri juu ya maisha ya baadae ya mtoto wake na hatimaye anamfanyia ukatili binti yake, na yote hii ni ukosefu wa afya ya akili kwa watu wengi katika jamii ya leo.
Baadhi ya viongozi pia wanashindwa kutimiza majukumu yao katika jamii na badala yake wanatumia vibaya mali na ofisi za umma kwa ajili ya manufaa yao binafi, hii pia ni ukosefu na upungufu wa afya ya akili. Watu wanashindwa kufanya majukumu yao kama inavyopaswa na akili zao hazifikirii kuhusu jamii isipokuwa matumbo yao ni watu watu hatari sana kwa kukwamisha maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kama kiongozi unatakiwa uishi katika mabadiliko na kuweza kuisaidia jamii yako kuvuka vikwazo vinavyo wazuia kupata maendeleo yao, na ikumbukwe tu ya kwamba uongozi ni dhamaa na wala si sawa kuweza kutumia ofisi ya umma katika kujinufaisha kiongozi binafsi. Hivyo basi serikali kam mdau mkuu wa kuleta maendeleo kwa jamii ihakikishe kwamba kila kiongozi wa umma kwa uchache apate huduma ya wanasaikolojia kila mwezi ili kuimarisha afya yake ya akili.
Hii ni muhimu sana kwasababu kiongozi nae ni binadamu anaweza kupatwa na msongo wa mawazo muda wowote na akashindwa kutoa maamuzi sahihi na hivyo kuweza kuathiri jamii yote kwa ujumla kutika na maamuzi yako hasi yaliyo shinikizwa na msongo wa mawazo alio nao.
Vijana wanaopenda kucheza michezo ya kubashiri ni miongoni mwa kundi kubwa linaloandamwa na tatizo la upungufu wa afya ya akili. Hii ni kwasababu huwa wanamatarajio makubwa ya kupata pesa nyingi na mafanikio makubwa kwa fumba na kufumbua na kupelekea kupoteza pesa nyingi bila ya kupata faida yoyote.
Na hatimae akili zao hazitaki kukubali ukweli na kufanya kazi na hazitaki na wala hazipo tayari kubadili mitazamo yao na kuacha michezo ya kubashiri bali kila siku wanadhoofu kiakili na kuishi katika nchi ya matumaini kwamba siku moja watakuwa mabilionea na wengine huita michezo ya kubashiri kuwa ni fursa kwa vijana.
Na ifike mahali sasa vijana tukubali kuwa michezo ya kubashiri ni adui wa maendeleo yetu na inatupunguzia uwezo wa kufikiria, kutafakari, kutafiti, kuchanganua na kuchambua njia sahihi za kuweza kufanikiwa katika naisha yetu ya kila siku. Hii naweza kusema ni upungufu wa afya ya akili kutoka na matarajio makubwa ambayo hayawezi kutokea isipokuwa ndotoni.
Akili inaweza kuwa au kuongeza afya ikiwa saikolojia ya mtu huyo ipo sawa katika maamuzi na utendaji na uwezo wa kuhimili mabadiliko ya ghafla ya mambo mbalimbali yasiyotarajiwa kwa wakati husika.
Vyuoni kuna wana taaluma wa saikolojia wanaohitimu kila mwaka lakini binafsi katika jamii zetu sijawahi kuona au kusikia huduma za saikolojia zikitolewa kwa wananchi wa kawaida kutoka kwa serikali au mashirika binafsi ili kuhakikisha watu katika jamii wanakuwa na afya ya akili iliyo bora, huwa najiuliza wanasaikolojia wakihitimu vyuo huwa wanapoteleaga wapi na ikiwa jamii ina uhitaji mkubwawa huduma zao?
Jamii inaangamia na wao wanaangalia, Je huu ni uzalendo kwa jamii iliyowakuza na kuwapa hizo taaluma? Hii itapunguza au kuondoa kabisa ukatili kwa watoto, wanawake, wazee na vijana na itaongeza amani, upendo na furaha kwenye jamii na pia itawapa vijana ari ya kufanya kazi za kimaendeleo kwakuwa watahisi kuwa wapo salama zaidi kuanzia kwenye ngazi ya familia mpaka taifa kwa ujumla.
Kwa hakika jamii yenye upungufu mkubwa wa afya ya akili ni jamii ambayo inaongoza kwa matukio ya kikatili kwa wapendwa wao, matukio ya uhalifu na ukosefu wa jamii ya vijana wawajibikaji na matokeo yake ni kuzorotesha maendeleo ya nchi kwasababu watu wengi hawana uwezo wa kuhimili na kutuliza akili pale kunapotokea mambo wasiyo yatarajia. Kwa mfano mfanyakazi ghafla bila ya kutajia akafukuzwa kazi kama hana afya ya akili anaweza kujiua na kuhisi kuwa ndio suluhisho.
Tukumbuke kwamba kuwa na elimu sio kuwa na afya bora ya akili ndio maana hata wasomi pia wanapokuwa na msongo wa mawazo wanaweza kujinyonga kwa kuhisi kuwa ndio suluhu ya matatizo yao na kama mtu huyu mwenye msongo wa mawazo akiwa na afya ya akili basi ni rahisi kwake kukubaliana na matokeo na hatimae kuanza upya au kurekebisha tatizo kama inavyokusudiwa na jamii.
Kumbuka : Afya ya akili ndio chanzo cha ukatili. Ongeza afya ya akili, zuia ukatili.
Mwandishi: CHALI
Mawasiliano: 0718167997

Upvote
0