SoC02 Vijana na changamoto za ajira

SoC02 Vijana na changamoto za ajira

Stories of Change - 2022 Competition

Msakatonge19

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1
Reaction score
1
VIJANA NA CHANGAMOTO YA AJIRA

✔️Kipindi Cha hivi karibuni kumekua na kasumba ya waajili wengi kutaka waombaji (vijana) kuwa na uzoefu usiopungua miaka mitatu.

✔️Leo nataka nizungumzie hili swala kwa uchungu Sana, maana imekua ngumu Sana kupata ajira kwa kijana alietoka moja kwa moja chuo, kuna vitu vingi Sana Hawa waajili wanavisahau Kama vifuatavyo.

✔️Kijana alietoka familia masikini, waliuza kila kitu ili mtoto wao asome, na hapo badae awasaidie wazazi wake.

✔️Wamesahau kuwa Hawa ndio vijana ambao walishinda njaa ili kuipambania elimu,

✔️Wanasahau kuwa Hawa ndio vijana waliosoma shule chakavu, zisizo na walimu wa kutosha, madawati Wala vyoo bora.

✔️ Wamesahau kuwa Hawa ndio vijana waliotembea umbali mrefu wakiwa na kidumu Cha maji na mfagio kuitafuta shule ilipo, kitu kilichosababisha hata vyeti vyao matokeo kutoridhisha ukilinganisha na wale wa shule za binafsi, sisi kwetu tunaita shule za magari ya njano.

✔️ Wamesahau Sasa wanataka mtu mwenye wastani wa Kwanza chuo bila kujua kua hakimu wa matokeo ya mwanafunzi chuoni ni mhadhili wake(binadamu mmoja).

✔️Wamesahau kuwa tuko hapa kuomba ajira sio tunataka kua matajili Kama wao bali tunataka kuzisaidia familia zetu zilizo kosa matumaini, maana yule mtoto wa jilani aliejinyonga juzi kwa kukosa ajira za serikali Mara tatu mfululizo, akajaribu ajira za sensa ambazo pia akakosa ukizingatia wanaofanya huo usaili ni walimu wakuu wa shule waliotanguliza kujuana na rushwa mbele.

✔️mkiwaona wambieni sura za vijana wengi zimekosa nuru, mioyo yao haina furaha, tabasamu limepotea katika nchi yao pendwa Tanzania.

✔️Mkipata ujumbe huu wambieni kua wathamini Sana mchango wa vijana, ulimwengu wa Sasa unataka vijana, okoeni hiki kizazi kitakachoijenga Tanzania Bora ya kesho.

✔️Msakatonge namaliza kwa kusema hata nyinyi jamii forumu fanyeni kwa haki haya mashindano kwa wengine sio mashindano ni njia ya kutokea gizani.

Msakatonge huyo naondoka kwenda kutafuta kula yangu.
 
Upvote 2

Makala nzurii..naomba sasa...kura umeipata..sema na mi naomba upitie maksala yangu na kunipa kura ysko
 
Back
Top Bottom