ShadracK2
New Member
- Sep 14, 2022
- 2
- 1
Uchumi ni nini? kumekuwa na maana nyingi kuhusiana na dhana nzima ya uchumi. Kamusi ya uchumi inafafanua uchumi kama "utafiti wa uzalishaji, usambazaji, na matumizi ya utajiri katika jamii ya wanadamu."
Na tukiangazia uchumi kama taaluma ni maarifa ya matumizi mazuri ya rasiliamali ili kuweza kukidhi mahitaji yetu ya kila siku. Kumekuwa na changamoto mbalimbali kwa wakazi wa Afrika kuhusiana na namna ya kujikwamua kiuchumi katika ngazi ya familia, mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Hili limejidhihirisha zaidi katika nchi maskini hususani katika bara letu la Afrika.
A) Uchumi katika ngazi ya familia na mtu binafsi.
Katika nchi zetu za Afrika ni ukweli usiopingika kwamba wakazi wengi hususani kundi kubwa la vijana wamekuwa wahanga wakubwa na wameshindwa kabisa kujikwamua kutoka katika umaskini uliokithiri. Kuna mambo mengi yanayochangia vijana kushindwa kujikwamua kiuchumi. Mambo hayo ni pamoja na;
Uhaba wa mifumo wezeshi kwa vijana. Kundi kubwa la vijana wamekosa uwezeshwaji kiuchumi ambao ungeleta tija kuchochea maendeleo katika ngazi ya familia na mtu binafsi. Kwa mfano; Taasisi za mikopo yenye riba nafuu zimekuwa chache ukilinganisha na uhitaji uliopo miongoni mwa jamii zetu hususani vijana. Hivyo basi taasisi za kifedha ziangalie namna ya kuongeza ufanisi katika kuwezesha jamii kupata mikopo nafuu itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Ukosefu wa elimu ya biashara na nidhamu ya fedha. Watu wengi katika ngazi ya familia na mtu binafsi wameshindwa kujikwamua kiuchumi kutokana na kutokuwa na elimu ya kuendesha miradi yao wanayoianzisha. Kwa mfano; unapoanzisha biashara yeyote ili ikue na kuendelea vizuri lazima uwe na nidhamu ya pesa kwa kujiepusha na matumizi yasiyo na lazima kama matumizi ya pombe kupindukia na wanawake. Utunzaji wa fedha unajumuisha kutunza kumbukumbu za fedha, kufanya makisio, kutengeneza taarifa za fedha, na kutafuta vyanzo vya fedha. Shughuli hizi ni za msingi kabisa katika kufikia malengo yako, kupitia kufanya maamuzi sahihi ya biashara.Utunzaji wa fedha kwa biashara yako ndogo unaweza kuwa changamoto. Ili ufanikiwe na kustawi inalazimu upate faida bila kutetereka, uwe na mtiririko mzuri wa fedha, na udhibiti hali yako ya kifedha.
Ukosefu wa ajira kwa vijana. Ni ukweli uliyo dhahiri kuwa changamoto ya ajira imekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya familia na mtu binafsi miongoni mwa jamii zetu. Kwa Tanzania, inakadiriwa vijana kati ya 600,000 na 800,000 wakiwamo wa vyuo vikuu, vya kati na ufundi uhitimu na kuingia katika soko la ajira kila mwaka lakini wanaopata ni wastani wa vijana 50,000. Idadi ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vya kati wanaojitokeza katika usaili wa ajira na wengine kukaa hata miaka mitatu tangu wamalize vyuo bila kupata ajira ni uthibitisho kuwa tatizo hilo ni kubwa. Wakili Frank Robert anasema tatizo la ajira nchini lipo, na pengine lipo kwa asilimia kubwa zaidi ya ilivyokuwa kabla na sababu zipo nyingi ikiwamo ongezeko la watu na kudumaa baadhi ya sekta. Pia mfumo uliopo hauwafundishi wahitimu ujuzi wala stadi zozote za kujitegemea kimaisha, badala yake umelenga kumwezesha mwanafunzi kutoka ngazi moja kwenda ngazi inayofuata. Mfano mwanafunzi akimaliza darasa la saba akiwa na miaka 13, mfumo utakuwa umemfanya amalize akiwa na maarifa ya historia au jiografia na akimaliza sekondari mambo ni yale yale pia. Mwanafunzi anamaliza shule bila ya kuwa na maarifa, ujuzi wala stadi za maisha, hivyo akikwama katika ngazi moja ni ngumu kusimama katika hatua nyingine ya maisha ya kuweza kiujitegemea au kujiajiri.
B) Uchumi katika ngazi ya Taifa na Afrika kwa ujumla.
Ni ukweli usiopingika kuwa Afrika ni tajiri sana lakini ni Masikini sana. Tuangazie baadhi ya changamoto zinazochangia Afrika kuendelea kutaabika kwa umaskini uliokithiri licha ya kuwa na utajiri mkubwa. Miongoni mwa changamoto hizo ni kama ifuatavyo;
Maarifa na teknolojia. Ni ukweli uliyo wazi kwamba Afrika ina mkusanyiko mkubwa wa maarifa. Ujuzi kuhusu unajimu, kilimo, umwagiliaji maji na hisabati huchukua maelfu ya miaka. Shida ni kwamba, maarifa haya hayajaunganishwa na hayawezi kurejelewa kwa urahisi. Pia bara zima limekaa kwenye kitanda cha maliasili. Takriban 40% ya maliasili za dunia ziko barani Afrika ikiwa itafanyiwa utafiti ipasavyo, idadi hii inaweza kuzidi 50%. Baadhi Nchi za Afrika bado watagundua kwamba wana almasi na dhahabu, mafuta na shaba, kobalti na platinamu, makaa ya mawe, na utajiri mwingine mwingi. Ukosefu wa teknolojia madhubuti ya kutumia rasilimali zetu wenyewe ndiyo umefanya Afrika kubakia kuwa maskini katika nyanja zote hususani kiuchumi.
Umoja na mshikamano. Nigeria inaweza kuwa tajiri kwa uwepo wa mafuta yasiyosafishwa, lakini je, ulifikiri hifadhi ya mafuta ghafi ilikuwa na mpaka mahususi na ilikuwa na mipaka ya Nigeria? Mipaka hii barani Afrika imetengenezwa na Wazungu na haina uhusiano wowote na hifadhi ya asili ya maliasili. Afrika ikiungana na kuwa wamoja tunaweza kujikwamua kiuchumi kwa kiwango kikubwa. Umoja huu utajengwa kwa kuwa na hati ya kusafiria kuruhusu wanadiplomasia na wafanyabiashara wa mfululizo kusafiri kwenda nchi yoyote ya Afrika bila kupata visa. Pia uwepo wa sarafu moja; Sarafu ya Afrika nzima itainua hata nchi maskini zaidi barani Afrika, kama vile Liberia, ambayo inatumia zaidi dola za Marekani kama sarafu yake kuu. Tuseme naweza kusafiri kutoka Ghana hadi Kenya nikiwa na pasipoti yangu pekee katika safari ya kikazi. Katika kesi hiyo, sitakuwa na wasiwasi juu ya ubadilishaji wa sarafu katika bara. Na mwisho lugha tukubaliane mara moja na kwa wote kuchagua angalau lugha kuu mbili zinazotawala na kuzifundisha kwa zote shule za msingi. Tukifaulu haya Afrika itajikomboa kiuchumi.
Mfumo wa hifadhidata.
Mpaka sasa Afrika haina mfumo wa seva. Kuundwa kwa shamba la seva katika bara zima ambalo madhumuni yake ni kukusanya na kushiriki habari. Hifadhidata ya habari itasaidia kupambana na ugaidi, majambazi, na aina ya wahalifu wa mtandao wanaokwamisha Afrika kutoendelea kiuchumi.
Makundi haya au watu wanaweza kufuatiliwa kwa ufanisi chini na kuondolewa, na inaweza kusaidia kufuatilia na kudhibiti magonjwa kama vile Ebola na Mengineyo. Pia Inaweza kutusaidia kukusanya taarifa kuhusu watu wasio Waafrika au Waafrika ambao wanajaribu kuiweka Afrika maskini kupitia migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.

Upvote
1