Kila nikirudi nyumbani (mkoani), nagundua dhahiri kabisa kuwa kuna ongezeko kubwa sana ya maduka madogo madogo ya pombe (grocery stores) katoka mitaa mbalimbali tofauti na hali ilivyokuwa miaka 10 au zaidi iliyopita. Hata maduka yanayouza mchele na sukari lazima kuna droo ya kuuza pombe tena pombe kali za nje na ndani ya nchi.
Lakini unapoona biashara inakuwa kwa kasi maana yake kuna uhitaji mkubwa wa huduma hiyo (law of demand and supply). Katika kuichunguza hilo nikagundua kuwa wateja wengi wa pombe ni vijana wa kiume hasa waliozaliwa miaka ya tisini na 2000. Kusikitisha zaidi athari za pombe zinaonekana dhahiri kwa hawa vijana, kwa mfano unaweza utakutana na dogo wa 2005 uliyembeba ukampita bila kumtambua kwani anaonekana mzee kuliko wewe. Wamekuwa sio wazalishaji katika jamii na kuonekana bure kabisa. Vijana wengi tumewazika kutokana na kunywa pombe kupita kiasi.
Mengi huwapelekea vijana hasa wa kiume kuingia kwenye ulevi kama ukosefu wa ajira, matatizo ya kisaikolojia, stress na kadhalika lakini kila mmoja ana nafasi ya kushauri na kukemea ulevi kwa vijana. Leo ningependa kushauri yafuatayo ili kupunguza ulevi kwa vijana:

- Kupigwa marufuku kwa matangazo ya pombe katika televisheni na redio. Miaka ya nyuma katika kupinga uvutaji wa sigara, serikali za mataifa mbalimbali ziliweka marufuku ya matangazo ya sigara katika televisheni, hata kuitazama filamu kama kuna uvutaji wa sigara huwa kuna onyo kuhusu athari za sigara. Vivyo hivyo, hatua kama hizo zinaweza kupunguza ulevi uliokithiri kwa kiwango kikubwa.
- Kuongeza kodi kwa 200% kwa pombe zote zinazotoka nje, 100% kwa pombekali (spirits nk) zinazotengenezwa ndani ya nchi, na 50% kwa pombe za kawaida (beer). Pombe kali ndio zimeharibika zaidi vijana, kwanza kwa kuwa na kilevi kikubwa lakini pia kupatikana kwa bei rahisi hivyo kuongeza kodi kwa pombe kali kutasaidia kudhibiti ulevi huo.
- Kudhibiti utengenezaji wa pombe haramu. Hapa tunaweza kutumia njia nyingine kuliko tuliyozoea ya kukamata pombe haramu kama gongo. Tunaweza kurasmisha utengenezaji wa pombe kali za kienyeji, kisha kuwapatia mafunzo watengenezaji, kudhibiti ubora, kuwasajili kwa maeneo yao pamoja na kuwatoza kodi kama biashara zingine. Hawa watengenezaji rasmi ndio watakaoshiriki kutoa taarifa za watengenezaji haramu kwani kutakuwa na ushindani wa kibiashara.
- Kuboresha sekta ya michezo katika maeneo yetu. Hivi karibuni tumetoka kushuhudia mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Paris Ufaransa. Katika mashindano hayo Tanzania ilipeleka wanamichezo wachache has katika mbio ndefu. Lakini kuna michezo mingi sana inayoweza kufundishwa kwa vijana wetu wa sekondari yenye gharama nafuu sana. Mfano Riadha pekee ina michezo mingi kama long jump, relay na mbio za urefu mbalimbali 100m, 400m, 800m, 1200m, 1600m nk. Michezo mingine kama volleyball, tenisi, Table tennis, badminton, field hockey, boxing, judo, Karate inaweza kusaidia vijana kuwa na afya njema, lakini pia kushindana kimataifa ili kuwakwamua kiuchumi.