Pre GE2025 Vijana ni kundi lililotengwa na uongozi

Pre GE2025 Vijana ni kundi lililotengwa na uongozi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Teuzi tunazoziona kila siku watu ni wale wale mbaya zaidi viongozi wengi wanaoteuliwa ni wazee hii inamaanisha Nini wadau? Swali je vijana hawatoshi kwenye nafasi hizo wazee hawa tumekuwa nao kwenye uongozi kwa muda mrefu lakini hatujaoni ufanisi

Wazee Hawa waliwaaminisha watanzania kuwa wao Wana uwezo sababu ya usomi wao lakini ufanisi bado hatuoni ufanisi wao kila katika utekelezaji kila ripoti ya CAG inapotoka inaonesha Kuna ufisadi makubwa wazee Hawa miaka mingi wanapambana sana watoto wao wanakuwepo kwenye system

Hitimisho Mimi kwa upande wangu naamini vijana wanauwezo mkubwa kwa sasa kuliko wazee Hawa tangu enzi za ujamaa tupo nao lakini uwezo wao ni mdogo kuliko uhalisia

Vijana wasomi wenye uwezo tunao wengi sana nchi hii basi tu tunawaangalia wanywa visungura na bodaboda na kusema vijana wa miaka hii hawana uwezo
 
Upo sahihi kwenye hilo, ila kwanini wazee wanaendelea kutumika ni kutokana na uzoefu walio nao kwenye mambo mbalimbali, na bado serikali inaona ipo tija ya kuwatumia wazee Ili wawarithishe vijana uzoefu waliokua nao, vijana wengi wa sasa, maadili, subira na ujenzi wa fikra tumbuizi unatufanya tubaki nyuma, ipo haja ya sisi kama vijana tutambue kwanza thamani na wajibu wetu ndio itawafanya wakuu watupe teuzi, lakini wanaotuangusha ni wale wanaoaminika hawatendei kazi thamani waliyothaminiwa wengi wao wanageuka mizigo tu,
 
Sisi sio kwamba hatuwezi..tunaweza vizuri sana mifumo iwape vijana wenye vigezo vya hizo teuzi kipaumbele..pia busara na hekima vinachangia sana ukizingatia sisi vijana baadhi yetu wengi vigezo vipo lakini mambo ya busara na hekima hatuna ukilinganisha na wazee wetu wanalamba teuzi..
 
Back
Top Bottom