Vijana sio waaminifu. Nusura niingie JELA. Sitakuja kumdhamini Mtu walahi

Vijana sio waaminifu. Nusura niingie JELA. Sitakuja kumdhamini Mtu walahi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Prof. Minzi na wengine!

Sijui kama Waafrika kuna siku tuta endelea na kufanikiwa kama wenzetu wazungu, wahindi, wachina, waarabu, nk. We seem to be at the lowest thinking, intellectual and moral level. Kwa nini nasema hivyo?

Nimewekeza hela nyingi sana kununua mashamba Mkoa wa Rukwa wilaya ya Kalambo about 2,000 acres.

Nimeajiri na nalipa mishahara mizuri kila mwezi for the second year! Sijaweza hata kuvuna kuanza kurudisha hela nilizowekeza. Wanapata malazi na chakula bure nje ya misharaha yao kwenye kambi ambayo nimejenga nyumba kadhaa, nimewekeza matrekta ya kilimo na mwaka huu ilikuwa tulime 500 acres kwa kuanzia. mafuta wanatumiwa, fedha za matumizi madogo madogo wanatumiwa.

viongozi ni watu wazima wa elimu ya chuo kikuu nikifikiri natoa ajira kwa waafrika wenzangu. Wapo wafanyakazi kama 50 wote kila mwezi wana mishahara na kula na kulala bure kwani ni mbali na mjini.

İli kusimamia nilimweka mtoto wangu wa kiume asimamie baada ya masomo ya diploma, nikamwondoa baadaye aweze kupata exposure kwenye miradi mingine. Nilimweka mpaka mchungaji rafiki yangu wa siku nyingi awe anatupia jicho la pembeni kwenye kijiji cha jirani na namlipa allowance kwa mwezi ila sio mfanyakazi.

To my surprise, kumbe wamejenga syndicate kubwa mno kati yao viongozi na operators wa trekta na hasa baada ya kumtoa mtoto wangu kwenye kazi zingine nikimwachia uongozi kijana mwingine ambaye nilipewa na mpendwa kanisani graduate wa UDOM wa zaidi ya 5 years experience ambaye kwenye interview showed quite good command of leadership.

Kumbe kwa siri, wameanzisha vijishamba vyao wanalima kwa mafuta yangu ninayowatumia; wanalima mashamba ya wenyeji kwa hela SH. 70,000 kwa ekari na fedha wanagawana kwa siri; matrekta yangu yote mawili yameharibikia kwenye mashamba ya kulimia watu kupata hela, muda wa kulima shamba langu hawana, shamba langu nililopanga kulima 500 acres this year, Limelimwa only 50 acres na matrekta yasingeharibikia huko wangelima hekari zaidi ya 200, ambazo zimethibitishwa kulimwa; gari yangu ya shamba Canter imekatika chasis kumbe wanafanya biashara ya kubebea watu mazao, kokoto na mawe kwa kulipwa hela wanazo pocket kwa kugawana bila sisi kujua na walifanya siri kubwa.

Nilisukumwa kuomba na kufunga for 3 days last week na sasa nipo kwenye maombi ya wiki nzima ya kufunga nikizidi kuomba ustawi na mafanikio kwenye kazi za mikono yangu.

Kwenye migao yao ya fedha za siri mmoja inaelekea hakuridhika na utaratibu wa mgawanyo akiona anapunjwa, walipoona anasumbua wakamfitini na kumfukuza kazi.
Ndiye baadaye aliyeanika syndicate yote ambayo kumbe mpaka mchungaji wa pale niliyemwamini sana sana naye yumo!😭😭

Nikimuuliza mchungaji huyo, kulikoni yote haya yanayotokea na yeye akiwamo kuhusu, aliishia kuwa na kigugumizi na ameshindwa kabisa hata kujitetea amebaki kuomba samahani!!!!

Waafrika tunaenda wapi jamaniii!!!😭😭😭
Umaskini kweli utaondoka kwa kuwa na roho chafu na mbaya kiasi hiki kweli. Hivi kama sio wokovu nilionao, watu kama hao akipigwa risasi na mwekezaji mwingine kama mimi, tutamlaumu hawa wezi, walafi, watu wasio na soni wala huruma kama hawa kweli?

Nimejinyima miaka yangu yote mpaka uzeeni ili niweke urithi kwa vizazi vyangu, nijisikie nilipambana wajukuu waje kuanzia maisha bora zaidi ya yale tuliyoishi sisi, tunaishia kuwekeza kwa wezi vijana wasio na roho kiasi hiki.

Nimeshea hili ili kama taifa tujitafakari tunakwenda wapi kwa kizazi hiki tulichonacho. Hawa ndio tunaowatengeneza wawe viongozi wa kitaifa, nchi itaweza kusogea kwa mentality ya jinsi hii.

Binafsi nimeamua kutafuta ku-employ Indians or Chinese kuendesha miradi yangu, nimechoka na waswahili acha waendelee kuwa vibarua na watumwa milele na laana zao.

Waafrika tusiporudi kumtafuta na kumwinamia Mungu kwa dhamira ya dhati mioyoni mwetu, laana ya umaskini na utumwa itaendelea kututafuna milele mpaka mwisho wa dunia

Nawashuhudia nyote kwamba Maombi yanafunua hata yaliyo sirini yaliyojificha. Mungu anaangalia dhamira iliyo safi mbele zake na humwekea ulinzi mja wake, kwenye hili, binafsi nimemuona Mungu akitenda.

Glory to God Almighty! 🙏🏾🙏🏾

mrangi

Nakumbuka 2018 nilikuwa na pikipiki Tatu. Mbili Boxer Moja Haugue, nikatafuta Vijana Watatu.

Vijana wawili waliochukua Pikipiki za Boxer nikawaambia badala wanipe elfu 10 Kwa Siku kama bodaboda Wengine wafanyavyo Kwa maboss zao Mimi nikawaambia wanipe elfu 8. Kwa wiki wantumie elfu hamsini badala ya elfu 56 kwani Siku Moja niliiweka kama Mapumziko.

Hivyo pikipiki Mbili Kwa wiki wangenipa Laki Moja, Kwa upande wa Boxer.

Kwa upande WA Haugue kútokana na soko la Haugue lilikuwa chini nikamwambia Yule dereva kuwa kîla Siku Pesa yàngu elfu sita. Hivyo kîla wiki anitumie elfu 35 badala ya 42k kwani Siku Moja niliihesabu kama Siku ya Mapumziko.

Haya miezi mitatu ya mwanzo walijitahidi kuwa waaminifu lakini Miezi iliyofuata wakaanza kusumbua.

Wôte walikuwa na familia, wôte walikuwa Watu wazima kiumri kunishinda. Hivyo nilitegemea wangekuwa Makini na serious na Kazi Yao.

Haya mmoja akikamatwa usiku akisafirisha Mirungi akitokea bagamoyo. Asûbuhi napata tàarifa kuwa pikipiki imekamatwa. Niliambiwa na Jirani na Yule bodaboda àmbaye amekimbia na kuacha pikipiki ikapelekwa Kituoni. Naulizia kito naambiwa.

Ikabidi nivunje Ratiba zangu za Siku hiyo niende Kituoni, nafika Kituoni wananiambia pikipiki yàngu inatumika kusafirisha magendo Hapo NI baàda ya kuwapa Kadi ya pikipiki wakajihakikishia Mimi ndiye Mmiliki.

Tunafanyaje? Tukayamaliza, ila Mkûu WA kituo cha polisi akanishauri kuwa biashara ya bodaboda ni ngumu kama sitakuwa nafanya mwenyewe au niwekee Mkataba.

Nikaona isiwe Kesi nikaiuza. Haijapita wiki Mbili anakuja bodaboda Mwingine, oooh! Pikipiki imekamatwa, tunaenda naambiwa pikipiki haina side mirror lakini pia jamaa amekamatwa usiku akaitelekeza,

Bahati nzuri nilikuwa nimeenda na fundi wàngu WA pikipiki, tunamuuliza Bodaboda Wapi zilipo side mirror anambela, mara fundi anasema hata battery imebadilishwa,

Nikawaambia Polisi wamuweke ndàni, wakamuweka, tukafuatilia Mpaka alipoziuza battery na side mirror. Tutamalizana naye.

MWAKA 2021.
Ofisi yàngu inatoa huduma za Usafi Kwa apartments, Ofisi, Nyumba, malls na halls na viwandani.
NI katika huduma hiyo inanikutanisha na Watu mbalimbali WA ndàni ya nchi na nje ya nchi. Wafanyabiashara Kwa watawala. Wajasiriamali na Watu weñye mitaji ya Kati.

Sasa mteja wàngu mmoja àmbaye NI Foreigner àmbaye nahudumia Kampuni Yake ya uwakala WA huduma Kwa wateja, yaani Kampuni Yake inahusika na Ku-train wafanyakazi ili wawe Customer Care Executive na ishu zingine zinazohusu huduma Kwa wateja Kisha hao wafanyakazi wanawa- supply Kwa makampuni ya simu kama Voda, Airtel na tigo na makampuni mengine àmbayo sio maarufu.

Sasa hiyo Kampuni Yake Mimi ndîo nilipewa tenda ya kusafisha na kuhakikisha panakuwa Safi.
Baada ya kuwa marafiki na kuniamini akaniambia Kwa vile yeye NI mgeni hapa nchini anaomba nimtafutie dereva wakuemwendesha.

Sawa Mimi kwèñye email na akaunti zangu kûna Vijana wengi Sana wa Taaluma mbalimbali wanaomba kazi kwangu huku Wengine wakiomba niwatafutie Kazi.

Sasa nikaangalia anayenisumbua mara Kwa mara nikijua huyo ndiye aliyekuwa anashida na Kazi, nilikosea Sana.

Nikampigia kijana huyo tumuite J, nikamwambia aje na document Zake. Kumbuka hatujawahi kuonana, hanijui simjui ila Mimi ananijua kidôgo kutokana na kuwa Mimi Nipo wazi mtandaoni.
Tukakutana.

Kijana mrefu, mweupe hivi, mwembamba mwenye Sura ya upole isiyo na tashwishi. Nikakagua leseni yake na copy Zake, vyeti, barua za serikali za Mtaa, barua za wadhamini. Baada ya kujiridhisha nikampeleka zilipo ofisi za mteja wàngu.

Mteja wàngu Muda huo anajua Mimi namfahamu J. Huyo nikawaacha Sasa nilifanya Kosa Moja la kiufundi. Nitalieleza baadaye.

Baada ya wiki Mbili, napigiwa Simu na mteja wàngu kuwa J hapatikani na ameondoka na gari. Duuuh!
Zaidi anasema ndàni ya gari kulikuwa na Milioni nne Kasoro hivi.

Tumbo joto. Sasa nikaingia kwèñye Maombi ya J nakuta mawasiliano yàngu ya mwisho ya WhatsApp nilimuagiza atume zile documents Kwa mtindo wa pdf na anitumie kwèñye email. Hakufanya hivyo na meseji za WhatsApp zote alizonitumia alikuwa amezifuta.

Tumbo la kuhara Hilo.

Mteja Foreigner naye ananipigia kila dakika tano. Namwambia asijali nafuatilia. Napigia Namba ya J haipatikani.

Nampata Wapi J?

Sasa mawazo ya Jela yalianza kunikonyesa.

Nikileta mchezo Hapa hii Ngoma nitalala nayo.

Nikampigia Mtu mmoja àmbaye anahusiana na mambo ya kipolisi na upelelezi. Akaniambia Kwa maelezo hayo nikienda Polisi Mimi ndio nitakuwa wa Kwanza kuwekwa ndàni alafu mengine ndîo yatafuata, hivyo akanishauri, Moja nisiripoti Kwanza, pili, nisiende Kwa mteja foreigner kwani anaweza kuwa ameshaandaa Polisi na nitakamatwa😃 kukamatwa tenà.

Ilikuwa Saa tatu tangu nipewe tàarifa likapita Lisaa limoja na Nusu. Mchumba wàngu hapo anahaha, namwona alivyo na wasiwasi.

Nikachukua Peni na kidaftari.

Nikaandika Majina ya J niliyokuwa nayakumbuka, nikaingia kwèñye jina la usajili la namba ya Simu aliyokuwa anawasiliana nayo, nikakuta jina la Kike, *****!

Tufanye anaitwa J alphonce Iteba,

Halafu jina la Simu alilotumia ilisajiliwa na Esther hezron kadege.
Nikaandika hayana mahusiano.

Kwèñye WhatsApp yake NI WhatsApp business. Hapo akawa amefanya Kosa Dogo la kiufundi. Nikakuta ameandika akaunti ya Instagram tuipe jina MASHARIKI X GARAGE.

Nika -screenshot upesi Kisha Hilo jina nikaliandika kwèñye kile kidaftari.

Nikaingia Instagram kuifutilia Ile garage, nikaona pîcha za Magari lakini zote plate number zilikuwa zimefichwa au zimepigwa kiubavu. Hatari

Scroll nikiangalie zile pîcha zitanipatia chochote kitu Wapi.

Chini Kabisa nikakuta kuna Carwash àmbayo inajina àmbalo sikumbuki vizuri Ipo maeneo gàni, nikaandika lile jina kwèñye Kile kidaftari.

Nikaanza kufuatilia comments za kîla post ya Ile akaunti, nikilenga Mtu àmbaye atajitokeza ku-comment kwèñye post nyingi katika Ile akaunti ya Mashariki X GARAGE. Nikapata Majina mawili, Moja la Kike jingine la Kiume. Nikayaandika kwèñye kile kidaftari.

Yaani Hapa lengo langu ni kutafuta Wapi nitaanzia nikitoka pale nyumbani.

Saa ya mkononi inasema Saa tano, masaa mawili tangu nipewe tàarifa ya kuibiwa Kwa gari àmbalo ndàni yake kûna Milioni nne Kasoro.

Akaunti ya kike, tuipe Jina Asmara fashion, nikaingiemo Humo nikakuta anafanya biashara ya Nguo za Kike na nguo za Watoto wachanga.

Nikapata Namba, nikaiandika Ile Namba kwèñye kidaftari.

Kisha nikaenda kwèñye akaunti Ile ñyiñgine hii ilikuwa yakiume, huyu alikuwa anauza TV, radio na vitu vya electronic. Nikakuta Namba nikaandika.

Nikazipigia zote, Namba ya Kiume haikuwa inapatikana, yakike ikawa inaita.

Akapokea mdada. Nikamwambia nahitaji nguo za Watoto wakiume. Akaniambia zîpo. Nikamwambia Duka Lao lipo Wapi akaniambia lipo Ubungo shekilango. Sawa.

Nikiwa Njiani nikakumbuka kuwa Simu yàngu mara nyingi nikiitumia kwèñye WhatsApp business nimei-merge na auto screen video recorder.

Nikafungua app ya auto screen recorder, nikaanza ku-scroll video za wiki Mbili zilizopita. Kwa Bahati nikakuta chat zangu na J.

Zaidi nikakuta nilivyoifungua Ile Leseni Yake. Nika-screenshot Ile Leseni ya J. Hapo angalau ninaleseni Yake.

Kosa nililofanya Wakati ule nikiwa na J tukiwa ofisini Kwa mteja foreigner NI kusahau zile hardcopy za documents Zake.

Kitendo cha Kupata Leseni ya J kilinipa Moyo, lakini bado nilikuwa na wasiwasi Mkubwa. Nikashuka shekilango. Nikaenda stationary nika-print Ile Leseni coloured lakini pîcha ya J haikuwa inaonekana Vizuri.

Nikaenda Kwa Asmara dukani, kagua nguo wee, tafuta nguo wee huku namsahili na kutafuta Nafasi ya kumuingia.

Nikamwambia J anajitahidi Sana, akasema J yupi nikamwambia J mwenye hili Duka, akahamaki NI kanakwamba haelewi nazungumzia Jambo gàni.

Nikamwambia mwenye hii Leseni. Huku natoa Ile karatasi.

Alipoiona akacheka Sana. Akasema huyu Dogo fundi garage àmbaye hata kujihudumia hawezi ataweza Kumiliki Duka. Nikafurahi kujua anamjua.

Nikacheka Sana, lakini Kwa kujifanyisha. Nikamwambia mbona jamaa anatamba kuwa hili Duka NI lake. Nikacheka tenà nikaongeza kusema kumbe jamaa mwenyewe Yahaya,
Hivi anaishi Wapi?
Nikamtupia Swali akaniambia anaishi Sinza lakini hajui NI Sinza Ipi.

Moyo ukapiga Paah!
Nikamuuliza anafanya Kazi gereji Ipi Siku hizi. Asmara ni kama akanshtukia. Maswali mbona mengi na bado sijanunua kitu. Ikanilazimu niahirishe maswali Kisha nikanunua kinguo cha elfu tisa. Ili Kumtoa wasiwasi. Kisha nikatoka.

Location Sinza, Msako Mkali Eneo lore la Sinza kuanzia Shekilango mpaka Mori, kutokea Mlimani City, kivulini, mwenge, Sinza ûzuri, kijitonyama. Chamoto nilikipata, Saa sita hiyo Jua Kali Balaa.

Nikiwa nashuka Eneo la Lego nikapata wazo la kuulizia jina la Carwash àmbayo niliona kwèñye Ile Akaunti, kama Bahati tuu katikati ulizauliza nafika Shule ya Mugabe naelekezwa hiyo Carwash Ipo Sinza Mori. Napanda gari chap nashuka Mori kweli ñàona Ile Carwash.

Sasa ndîo nini, nikasema nitaanza kumuulizia J Hapa kuelekea upande huu. Uliza wee huku nawaonyesha pîcha Wapi.

Katika kuuliza sikuwa naulizia Mtu yeyote ninayekutana naye kun Watu walikuwa ndîo target yàngu hasa Watu wazima na vijana wa bodaboda. Nikafeli pakubwa, Saa nane hii Hapa, mteja foreigner kapiga Simu Mpaka kachoka,

Nikasema Acha nifuatilie hiyo Garage, nilikuwa nishapaniki maana niliona Siku inaweza kuisha na sijafika popote. Huku mteja anapiga Simu huku Mchumba anapiga Simu kufuatilia nimefikia Wapi. Jasho kama lote hamna Hamu ya Kula Hapo.

Garage bubu ndîo litakuwa ficho la gari. Nilijua hivyo. Sasa Eneo la Sinza garage bubu zîpo nyingi Sana.
Ulizauliza, nikiwa nimelenga hasa mafundi pikipiki na Magari.

Kwa Bahati naambiwa Mashariki X garage Ipo Sinza Lion Huko. Nachukua pikipiki mpaka lion, nakuta Garage lakini haikuwa imeandikwa Mashariki Bali Maliki X garage. Dadeki! Hoi.

Nikapata wazo "Eastern Garage" Saa tisa hiyo! Uliza Eastern Garage Iko Wapi, uliza uliza uliza uliza kîla Mtu haijui. Mimi mwenyewe nilijitungia tuu baàda ya kuikosa Mashariki X garage. Katika kukata TAMAA anapita jamaa mmoja amechafuka akiwa na Guta, anakula Miwa huku anatupa maganda Barabarani, tupo Sinza kijiweni hapo.

Sijui inakuwaje namsalimia Kisha namtania Muwa ulizamisha Meli, wôte tunacheka, Kisha namuiliza kama anaifahamu Eastern Garage. Kama Mzaha vile ananiambia hiyo garage Kwa Sasa haifanyi Kazi ila NI sehemu wanakusanya vyuma chakavu hasa vya Magari na Pikipiki. Dadeki.

Kwanza Sikuamini, nilisema nitamuamini mpaka nitakapofika kupaona. Akanielekeza Kwa Bahati nzuri Mimi sinza nimeishi Miaka minne hivyo napajuajua.

Sugua Kwa miguu maana Pesa Sasa imeisha. Nafika nakuta Ukuta mkuumkuu na gate lenye kutukutu àmbalo limeandikwa hauruhusiwi kuingia Hapa. Ndàni nachungulia kûna Magari mabovu, mascrepa na kûna jengo kuukuu.
Saa Kumi hiyo. *****!

Nampigia Mshikaji mmoja kuwa aje Sinza pale nilipo. Kweli baàda ya dakika ishirini anakuja na pikipiki. Tunaingia mule ndàni, Mwanaume mmoja na kijana mmoja ndio wanatupokea lakini Mshikaji wàngu anaonyesha kitambulisho. Wanakuwa na Hofu. Tunaingia ndàni zaidi ya jengo kibabe baàda ya nje kutoona gari.

Moyo unanipiga Paaap! Baada ya kuliona gari la mteja wàngu foreigner Likiwa limepaki. Aiseeh nashindwa kueleza Moyo ulivyofurahi. Nilifurahi Sana. Sana. Nikajikuta nikimshukuru Mûngu.

Aliyeileta hii gari Hapa yupo wapi.
Mshikaji wàngu alishangaa Sana kuwa nimejuaje ile gari Ipo pale Siku na Majibu zaidi ya kumwambia NI Mungu.

Wale Vijana tukakamata, hawajui J anaishi Wapi.
Tukarudisha gari.
Mteja Foreigner alikuwa na jazba Sana.

Nikamwambia Pesa yake Kesho italetwa.

Nikarudi Nyumbani nimechoka Sana.

Kîla mara najaribu kuipigia Simu ya J haipatikani.

Kesho yake asûbuhi Kazi NI kutafuta anapoishi J. Niliamini hapatakuwa Mbali na Sinza hasa kwèñye Ile Carwash.

Nikasema Leo sitamuulizia J Alphonce Iteba
Isipokuwa nitamuulizia Alphonse Iteba mwenyewe.

Huyo Kiguu na Njia Saa Moja mpaka Sinza Mori kwèñye Ile Carwash. Kufika nikaona Kuna uchochoro àmbao kûna Mama Mtu mzima anapika chai na chapati kwèñye kibaraza. Nikafika wakanikaribisha Kama mteja.

Nikaagiza chai na chapati Mbili hivi. Wakati nakula nikamuuliza Yule Mama hivi Kwa Mzee Alphonse Iteba ni Wapi? Akajibu Yule Mzee WA kisukuma?

Mimi Muda huo simjui, nikajibu ndîo huku Moyoni nikiomba Mungu awe ndiye huyohuyo ninayemtafuta Mwanaye.

Unamtafu Mzee au unatafuta kwàke? Yule mama akauliza Swali la mtego.

Mimi nikajibu vyote.

Akaguna, mbona Mzee Alphonse kafariki kitambo Sana. Ndîo maana nikakuuliza.

Nikasema Mimi nimeagizwa nifike Kwa Alphonse Iteba sijajua kuwa Mzee mwenyewe kuwa kumbe alifariki.
Yule mama na baadhi ya wateja Wakavutiwa na Stori yàngu kutaka kujua Nina shida gàni. Yule mama akaniuliza kunausalama, nikamjibu upo Kwa nini, au hiyo Nyumba Haina usalama yàani nyumba ya màtukio. Wakasema hamna.

Basi nikaelekezwa, Wala sikutaka kumaliza zile chapati nikatoka zangu. Hapakuwa Mbali NI kama Mtaa WA tatu, nafika nagonga, anafungua Mama mmoja WA Miaka 60 hivi ananiangalia Kwa udadisi huku akinisalimu.

Namuuliza wewe ndiye Mama Iteba, anakubali. Namuuliza J alphonce Iteba yupo wapi.
Ananiambia kuna nini, kafanya nini.
Moyo unashuka shwaah! Nimefika Kwa kina J.
Kazi Kwisha.

Tulimalizana kibabe Sana.

Uaminifu ni Jambo kûbwa sana.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Sema don't make generalization kuna watu tunapambana Sana kuseti standard katika hard working and being honest.

Vijana waaminifu wapo mkuu japo sio wengi.


Hicho kisa kimenisikitisha Sana.

Mkûu Asilimia 95% Vijana siô Waaminifu

Hao 5% waliobaki àmbao NI waaminifu siô ajabu 2.5‰ wavivu na wachagua Kazi. Hiyo 2.5% iliyobaki ndîo Vijana Wazuri
 
Usitafute uaminifu dar, kilimanjaro, Arusha au Babati, umekwishaaaa

Mimi NI wale Watu àmbao Naamini ubaya na Wema hauna Kwao.

Niliwahi jaribu kufuata mapokeo ya Wazee kuhusu Imani na uaminifu wa Watu WA Baadhi ya maeneo nikaangukia pua.

Alafu wale niliowahofia wakafanya vizuri
 
Nilichofurahia na kujuta ni kuwa wewe kazi unayofanya sidhani Kama inakufaa maana mpaka hapo upo kwenye mstari wa kumi na tisa wa Sheria ya alkaline .

Huwezi kunielewa ila jua Kuna sehemu ungefaa kuwepo .

Pole na hongera
yani akawe mpelelezi atuteke,atubinye kende!!.. anafaa lkn kwa limitation huyu akiwa mpelelezi kwa mazonge aliyopitia ukiingia kwenye kumi na nane zake basi kizazi huna!..😂
 
Inafikirisha.

Inaumiza Sana

Kijana Wakati anakuja kuomba Kazi Aiseeh utamuonea huruma. Anakusumbua Miezi na Miezi. Unamwambia tulia subiri, subiri mwombe Mungu Nafasi ikitokea nitakushtua.

Anakuaminisha Kabisa.

Nafasi inatokea, Mtu ananiamini Mimi, ananiheshimu na tunaheshimiana, anahitaji kijana unamwambia kûna kijana atamfaa, unampeleka anajaribu.

Anaondoa uaminifu na heshima yôte. Hatari
 
Back
Top Bottom