Vijana sio waaminifu. Nusura niingie JELA. Sitakuja kumdhamini Mtu walahi

Sio kwa fikra, mawazo, maandishi na maneno yako na genge lako lote.

Yani upo kinyume kabisa na Ulichoandika.

Tufukue?

Kwamba Mtu asieleze kilichotokea?

Mimi nimeeleza Moja ya Stori yàngu na zîpo nyingi siô Moja..

Unàtaka Watu wasiseme ukweli ili tujue tunatokaje?
Au kisa NI Waafrika?
 
Uaminifu kwa mtanzania sahau.

Ni wakuhurumia sana wamiliki was vyombo vya moto kama Mabasi, malori, taxi, boda boda nk.

In short mtanzania si wa kumpa kazi.

Uaminifu zero na wizi ni kipaumbele.

Shughuli yoyote na mtanzania lazima ife tu!

Sawa Mzungu.

Chakushangaza, na yote hayo uliyoyaandika, kesho utaamka na kubandika Uzi Watanzania Wakuamini😂😂😂😂😂😂😂😂


Watanzania. Wasomeni hawa wakuja. Muwatambue.

====Ndio maana nasema CHADEMA haitoweza kuja kushika dola ya Nchi hii.

Manake hawa mnao wasoma waki wadhihaki Watanzania, ni mamluki walioajiriwa nao.

Piga kura kwa Umakini sana.
 
Kwamba Mtu asieleze kilichotokea?

Mimi nimeeleza Moja ya Stori yàngu na zîpo nyingi siô Moja..

Unàtaka Watu wasiseme ukweli ili tujue tunatokaje?
Au kisa NI Waafrika?
Wachana na stori yako......

Umesema, Binadamu wanafanana? Utuambie basi wanafanana na lipi au nini?

Namie nimesema unakinzana na mtazamo huo wa "Binadamu wanafanana"

Maandishi yako, maneno yako, na hata Fikra zako hayajawahi kuwiana na Ulichokisema.

Kwa sababu gani, sijui.
 
Biashara za bodaboda na bajaj soko limefika saturation/ ukomo. Hakuna abiria. Tubuni miradi mingine ya kibiashara. Bodaboda na bajaj mbali ya kufanya uhalifu sasa wanatumika zaidi kisiasa na chama dola kongwe CCM kuwajazia mafuta.
 
Mtu anafanya makusudi alafu anajua atasema Sorry. Alafu kuna ule msemo "hakika Mimi binadamu si mkamilifu" ukisikia Mtu anatumia Misemo ya namna hiyo kama naye Mbali
Kweli mkuu. Mimi kuanzia mwaka jana nilianza utaratibu wa kutumbua kama JPM hadi sasa nimewapata waliotulia kuanzia Januari niko nao. Nilichoshwa na kuombana msamaha kipuuzi.
 

Haipo shaka imekuingia sawia:



Tiba kamili hiyo kwa chawa (aka) kijana wa hovyo kama wewe.

Hatuwezi kuona haya, kuwaonea haya, chawa wa hovyo wenye harufu Kali, kama nyie.

Kwa hakika popote tukiwaona tegemeeni dozi kamili: "600mg chrystapen, daily."

Bure kabisa!
 
Nimesoma kwa makini inasikitisha sana sana.
Ila ngoja niulize na kwenye hili tuwe wawazi kidogo..nami ni kijana pia ila je mnadhani mbegu ya kutokuwa na uaminifu kwa vìjana imetokea wapi.

Mnadhani vijana wamejifunza wapi au tumejifunza wapi.

Ebu wajitokeze watu wazima hapa ambao wanaweza kusema wamekuwa waaminifu kwenye kazi zao toka ujana wao hadi sasa.
Nchi yetu ukiwa mwizi unasifiwa na ukiwa muaminifu unaonekana mzembe sanasana.

Haya ni matokeo ya mfumo mzima wa jamii yetu kwa sasa na hali hii itakuwa hivihivi hadi tutakapo kubali kuishi kwenye misingi ya ukweli kama taifa hali itashuka hadi kwenye ngazi za familia zetu.

Leo hii ukienda sehemu yoyote kupata huduma lazima uhonge ndio utapata huduma nzuri nyie wazee ndio wezi hatari huko kwenye maofisi mnakula 10 percent kwa kwenda mbele kuanzia viongozi, watendaji hadi watumishi, wachungaji, maskofu na masheikh wa hii nchi asilimia 95 wananuka rushwa na wanaishi maisha ya uongo na kujipendekeza yenye unafiki.

Mtindo huu wa maisha ndio wazee wetu mmetuchagulia tuishi na nawaambia vijana watawafurahisha.

Kizazi cha leo ambacho mnakilaumu ni kinyago mlichokichonga wenyewe sasa kinaanza kuwatisha.
 
Interesting story
 

Unapomsema Kijana automatically unasema Wazazi na Wazee.
Kuwasema Wazee direct inaweza isichukuliwe Vizuri kimaadili lakini njia inayotumika ni kuwasema Vijana lakini Vijana hawakujilea wènyewe
 
Unapomsema Kijana automatically unasema Wazazi na Wazee.
Kuwasema Wazee direct inaweza isichukuliwe Vizuri kimaadili lakini njia inayotumika ni kuwasema Vijana lakini Vijana hawakujilea wènyewe
Unajua mtibeli swala la uhaminifu kwa hapa nchini ni swala la kitaifa ni mfumo ndio ulivyo hautaki watu wakweli na waaminifu.

Sasa tukiwa tunawasema vijan pekee hatuwatendei haki tuanze kwenye chanzo hukohuko ili huku chini iwe rahisi.
 
Biashara za bodaboda na bajaj soko limefika saturation/ ukomo. Hakuna abiria. Tubuni miradi mingine ya kibiashara. Bodaboda na bajaj mbali ya kufanya uhalifu sasa wanatumika zaidi kisiasa na chama dola kongwe CCM kuwajazia mafuta.

Kweli Kabisa Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…