ahaaa mi nimesoma civil japo diploma, namna watu wengi wanavyojiajili ni
1.unajifunza kuchora ramani zenye kuendana na hali za za maisha za watu, dau chezea kwenye 50,000 hadi 100,000, hapa watu wengi wanazimudu , unajua nini unakuta watu wengi wanajenga kwa hatua wengi hawana hela ya kujengaa jengo lote bila kupumzikaa, so unakuta anatafuta hela ya msingi akifaulu anatuliaa miezi miwili, anatafuta hela ya boma tena tofali za choma, then anaingia kuezekaa na baadae finishing, so unatakiwa kuuza kulinga na life standard ya watu sio tu unakurupuka ramani moja laki 4 sijui milioni, utakaa nayo kwenye computer unakuja kushtka muda umekutupa hiyo ndo shida wanayoipata maarchtects, wao wanapanga bei zao ambazo hazipo sokoni, unakuta sisi civil tunagonga kila kitu hadi kazi zao tumezivamiaa(tunaitwa malaya wa kazi hatubagui) hatuachi hela ipoteee kizembezembe, mtu kaja na tsh50,000 mama ntilie halafu unakataa hela unamwambia hakuna ramani ya hiyo helaa, subiri matajiri waje wakupe hela unayoitaka sasa, sasa hivi ukisema ufungue kampuni la ujenzi kupata tenda ni kazi ngumu sana huna tofauti na mtu anayecheza casino, tarura,tanroads huwezi kupata hadi uhonge , haya njoo majengoo sasa miradi yote inajengwa kwa force account, local fundi ndo anavuta hela sio wewe mwenye kampuni so utaishiaa kuwa mlipa kodi tu , ukija majengo private, mengi hawatumii waingneer coz wanagarama sanaa wanachofnya ananunua ramani tu, anamtafuta fundi mzuri na formen 1, anawapa ramani mjengo unasimama, kama jengo kubwa sana may be gorofa wananunua logo ya kampuni, ila wanajenga wao so anapunguza garama ya kuwa na maingneer site, ndo maisha yanaenda hivyo.
2.kwa upande wa IT, sijasoma chuo ila najua basis tu, navojua inahusu mambo ya programs , ila kwangu mimi nimejikita hasa kwenye speculation ya sarafu za kigeni, so nachofanyaa nafanya kazi za civil either kuchora ramani, kuandaa BOQ, kutoa ushauri kwa wa kitaalamu kwa tajiri kwenye jengo lake ushauri huo utakuwa wa vipimo ila asimia kubwa ni materials tu kwasababu nyumba ni materials ramani inachukua pati ndogo sanaa, so nikipataa hela kidogo may be 100,000/= natumia leverage principle kwenye forex naimaxmize hio hela ili kuongezekaa so taaluma yangu naitumia kamaa kupata kianzio (benchmark) cha kufanya biashara au project flani, siitegemei initajirishe.