kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nimezunguuka dunia hii hususani Ulaya, Marekani, Australia, na Asia, kote huko nimekuta Uuguzi (Nursing) ikiwa na fursa nyingi sana kuliko kada nyingine za Afya. Kule Marekani Uuguzi uko juu kwa ajira, malipo na kulidhika (satisfaction) ukifuatiwa na udakatari wa memo (dentist).
Vijana wengi wanadhani kuwa udaktari ndio taaluma yenye pesa na hadhi, labda hiyo ilikuwa zamani sana zilizopita wakati Tanzania kulikuwa na chuo kimoja tu cha sayansi za tiba (Muhimbili). Sasa hivi hali sio hiyo tena, udaktari sio dili tena baada ya zaidi ya wahitimu zaidi ya 2000 nchini kuhitimu kila mwaka kutoka vyuo mbalimbali. Wahitimu wa Udakatari wanasota mitaani ukilinganisha na wahitimu wa Uuguzi. Na wengi wao wanafanyakazi zisikuwa za kidaktari kama biashara,na uongozi. Kule Marekani na Ulaya wako madaktari ambao wameamua kusoma upya kozi ya uuguzi ili wapate manufaa kwa urahisi.
Sababu hasa ya mapinduzi haya ni:
1. Hospitali nyingi zinaajiri Madakatari wachache kuliko Wauguzi, hivyo wauguzi wanahitajika wengi kuliko madakatari.
2. Manesi wana taaluma nyingi ukilinganisha na madaktari, hivyo unaweza ukawatumia pia kwa kazi nyingi nyingine kama vile kwenye Uongozi, kutoa na kutunza dawa, kuzalisha, chanjo, stoo, maabara, kupima na kuhudumia watoto, utafiti, komputer/data, au Ualimu, kwasababu mtaala wa Uuguzi unawafundisha vitu vingi sana mbali ya uuguzi wa wagonjwa.
3. Mapato makubwa. Mbali ya mshahara lakini wauguzi wana overtime nyingi, seminar na mafunzo mengi ya kila wakati ambayao yanawaongezea kipato. Wauguzi wanaweza kufungua na kumiliki Maternity Home zao wenyewe na wanaweza kufungua au kutoa huduma kwenye maduka ya dawa muhimu. Daktari mara nyingi anapata kipato cha ziada kwa "kujilipua". Yaani kuhangaika na kutafuta part-time kwenye vi-hospitali mbalimbali wakati ule anaopaswa kupunzika na familia yake ili aweze kujiongezea kipato.
4. Wauguzi siku hizi wanasoma hadi ngazi ya PhD sawa na madaktari kitu ambacho zamani hakikuwepo, hizo siku hizi wauguzi wanafanya tafiti kubwakubwa wao wenyewe na kuandika vitabu na machapisho mbalimbali.
5. Wauguzi wanasomesha watoto wao, wanajenga nyumba, wanaendesha magari yao na ni viongozi wakubwa.
Vijana jiungeni na uuguzi kwa wingi fursa zipo huko pia, avuamae bahari papa kumbe wengine wapo. Achananeni na mawazo ya kizamani.