Kaka udaktari una ngazi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya Assistant Clinical officer, Clinical Officer, Medical Officer, Masters na PhD. Hata uuguzi nao unaanzia Certificate, Diploma, Bachelor, Masters na PhD. Madaktari mara nyingi huwa mnakutana wodini na wauguzi wenye Certificate, Diploma au Health attendants. Hao pia wana elimu ndogo kiwango cha ACO na COs wenu ndio maana huoni makali yao na wanakusikiliza mwanzo mwisho hata ukiboronga. Lakini Nesi mwenye degree ana kiwango cha Anatomy, physiology, Biochemistry, Microbiology, Pharmacology, Parasitology, DS, Biostatistics, Epidemiology sawa na kile cha Daktari. Baada ya hapo anakuwa Obstetrics ya hali ya juu, surgery, medical na Pharmacology nyingine ya hali ya juu kuliko daktari. Unafundishwa leadership na management kubwa.
Fanyakazi na Muuguzi mzoefu mwenye degree au Masters ili uone atakavyokuendesha puta.
Hao uliowaona wewe ni certificate na diploma. Hakuna Daktari ambaye hajafundishwa na kuonyeshwa cha kufanya na muuguzi.