Vijana someni Uuguzi, una fursa nyingi

Sidhani kama ni ushauri wa maana. Kwanza kusoma kozi yoyote ile lazima uwe na vigezo na uwezo wa kozi husika. Pili lazima ujue changamoto, na uhitaji wa hiyo kazi si kusema inalipa tu Basi waende, je uko tayari kupambana na changamoto ya kazi husika?

Pili huwezi kutumia reference ya mataifa ya nje Kama kigezo Cha mtu asome kozi Fulani. Hakuna gurantee ya kwenda huko na hata ukifika huko hakuna uhakika wa kupata hayo uyasemayo. Jambo la muhimu kabla ya kuamua kusomea kitu Fulani uelewa was kazi husika na changamoto zake ni muhimu Sana. Pili uwezo wa kozi husika kwa maana namna ya kujifunza na mwisho commitment ya kozi husika.
 
Watu wanadanganyana tu Nursing Degree Tamisemi anaanza na TGHS C,wakati MD anaanza na TGHS E. nursing huwezi linganisha na MD mpaka siku ya Kiama.
utumishi wanapanga mishahara mishahara mipya kwa watumishi kwa kuangalia pamoja na mambo mengine ni urefu (miaka ) wa kozi mtu aliyosoma. Kwavyovyote vile MD watawazidi mshahara kidogo tena kidogo wenzao wa uuguzi, pharmacy, laboratory, etc kwakuwa kusoma MD ni miaka 5 na mwaka mmoja wa mafunzo (internship) wakati uuguzi ni miaka 4 na 1 intern.

Zamani kidogo urefu wa degree ya uuguzi ulikuwa unawazubaisha sana pale Utumishi kwakuwa kulikuwa na degree za uuguzi za miaka 2.5, miaka 3 na miaka 4. Wengine walienda internship na wengine walikuwa hawaendi intern, hivyo ikawa vigumu kupanga salary scales. Lakini sasa tatizo hilo halipo kwakuwa degree ya uuguzi sasa ni miaka 4 na mwaka mmoja internship. Mambo saafiii. Baada ya kufaulu mtihani wa leseni na kusajiliwa ajira ziko njenje ndani na nje ya nchi.

Hii ya MD sasa hivi ni historia tu bro,. Na sisemi kuwa sio kozi nzuri, lakini kila siku maisha ya wanajamii yanavyoendelea kuboreka na magonjwa kama kipindupindu, malaria, kaswende, gonorrhea, UTI, TB, surua, polio, pepopunda, kifaduro, tetenasi, ajali, kwashiorkor, nk yainavyopungua kwenye jamii ndio hospitali zinavyopunguza uhitaji wa madaktari wa kuajiliwa. Badala yake wanahitaji wauguzi zaidi Na madakatari wa part-time tu. Na wakati mwingine wanahitaji clinical officers tu Na MD mmoja tu wa kudumu. Amkeni vijana wangu.
 
Hata hivyo dunia sasa ni kijiji, unaweza kufanya utafiti mdogo we we mwenyewe kuhusu hiki ninachoshauri, changanya Na zako. Hata usipotaka kwenda nje ya nchi hata nchini uuguzi ni dili pia. Nenda mahosipitalini ukahesabu idadi ya madakatari Na wauguzi walioajiliwa uone nan wako wengi. Faida nyingine wauguzi wanahitimu wachache vyuoni kuliko kada nyingine Afya.
 
Unaumwa wivu wewe ..... manesi karibu wote Tanzania ni doctors wannabe.....ndio change cha wivu kama huu
 
Sidhani kama jamaa anazungumzia ishu ya mishahara. Nadhani kajikita kwenye urahisi wa kupata ajira kati ya kozi tajwa hapo juu.
Watu wanadanganyana tu Nursing Degree Tamisemi anaanza na TGHS C,wakati MD anaanza na TGHS E. nursing huwezi linganisha na MD mpaka siku ya Kiama.
 
Tatizo ni kuwa committed kwenye kazi, na kuwa tayari kujitolea kufanya kazi husika. Usimshauri mtu asome kozi Fulani kwasababu in ajira au rahisi kupata ajira, Bali mtu Kwanza awe na wito kwenye kazi husika. Kupata kazi ya nesi ni rahisi mahali kote lakini je mtu anayajua majukumu ya nesi?

Ni kazi ambayo ya kujitoa kwelikweli na kama huna wito hutaweza utafukuzwa tu a utaacha mwenyewe.
 
Kwahiyo kazi ya md ni kutibu stis,na kwashiorkor tu ebu kua serious chief? Mahitaji ya md bado ni makubwa Kuna mashirika mbalimbali yanayotaka hao mds ,kufundisha vyuo vya Kati kunataka mds etc usiwakatishe tamaa watu wanaopenda hiyo kozi .Kama unesi mtu asome akitaka
 
Maswala ya Afya ni muhimu kwetu kama wanadamu ila siwezi shauri mtu wa karibu nami ayasome
 
Sio kwamba watoto wanasoma MD kwa passion, wazazi ndo wanamwambia lazima uwe MTU Fulani bila kufahamu ugumu wa kozi na trend ya fani ikoje. Unasoma kozi miaka 6, masters miaka 4. Utawakuta watoto wenzio wa kozi fupi wako mbali sana kwenye maisha na familia.

Kazi ya udaktari ni ngumu kwelikweli ni wito tu unahitajika. Unacholipwa na ugumu wa masomo na Kazi havilingani kabisa na malipo. Utawaonea huruma vijana wakihangaika kutoka hospital moja kwenda nyingine kutaguta kipato ili angalau kifanane na title, wana madeni ya magari kama watumishi wengine tu, wanapanga nyumba kama wengine tu, wana magari ya mikopo kama wengine tu. Mbaya zaidi hata ajira ni shida pia.

Siku hizi wenye hospitals wanaringa, wanaangalia umehitimu udaktari kutoka chuo gani, maana vijana ni weupe mno vichwani. Kusema ukweli wanapofika kazini wanategemea manesi, lazima wafundishwe upya na manesi.
 
Upuuzi.... Hizi data ni za nchi gan??, em ifike point utafte ukweli kwanza kabla hujapayuka

upuuzi.... Maelezo yako yanakinzana... Mara kuna ajira nje na ndan ya nchi, mara unaweza hata kujiajiri pharmacy...

Tafta data zenye ukwel ndo uje utusihi huku
 
Ni uzi wa kitambo ila huyu jamaa anadanganya mno, sijui anadhani sisi hatuishi na hao madkt na manesi au sijui anadhani ni yeye pekee alieajiriwa kwenye hiyo kada.

Kweli hawa manesi ni wa kuwafananisha na madkt kwa kipato kweliii??
Mwamba umetukosea sana aisee.

Kama we umesomea hiyo kitu na unaipigia chapuo sawa ila huku mtaani hakuna ajira na jinsi vyuo vilivyo na utitiri ndo kabisaaaa.
 
Huyu jamaa anaacha kusa huko nje ya nchi hii ni ajira pendwa eti anasema hapa tz!! Huko mbele hata ualimu ti ni ajira nzuri na wanalipwa vyema.

Ila kibongo bongo kufananisha muuguzi na dkt ni matusi.
 
Udom MD 500??
Takwimu zako umezitoa wapi mkuu??
Hivi unazielewa kweli takwimu zako??
 
Madaktari wengi siku hizi ni jobless mkuu usikatae. Pia wamekuwa wadangaji sana (kwa upande wa wanawake) mtaani maana hawana hata ajira.

Kwa upande wa vijana wa kiume ambao ni Madaktari wametekwa na betting.
 
Unachobisha kitu gani? Muhimbili tu madaktari wa meno (DDS)wanaohitimu kwa mwaka ni zaidi ya 200.
 
Madaktari wengi siku hizi ni jobless mkuu usikatae. Pia wamekuwa wadangaji sana (kwa upande wa wanawake) mtaani maana hawana hata ajira.

Kwa upande wa vijana wa kiume ambao ni Madaktari wametekwa na betting.
Mi sijaongelea kuhusu ujobless wa madaktari au hujaelewa nilichoandika??

Rudia kukisoma tena ulichoquote.
 
Kama hujui ni heri ukakaa kimya. daktari halisi (udaktari mama) ni physician (internal medicine) hao wengine ni branches tu. Kazi mama ya physician ni kuhangaika na magonjwa ya ndani yakiwemo communicable (malaria, tb, kaswende, chlamydia, HIV, kipindupindu, kichocho) and non communitie (kisukari, pressure) diseases. Hebu nambie, tangu ujue kutumia choo, kunawa mikono baada na choo na kabla ya kula, kulala kwenye chandarua
Udom MD 500??
Takwimu zako umezitoa wapi mkuu??
Hivi unazielewa kweli takwimu zako??
Wahitimu wa udom ndio worse kwenye market, why? Intake kubwa Na practical sites chache, wagonjwa wachache Na walimu wachache. Hiyo takwimu ya 500 isikuchanganye sana inaweza kushuka Na kupanda, LA muhimu ni kwamba udom inamimina sokoni ma MD kibao sokoni kila mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…