Kazikazinione
New Member
- Jul 27, 2022
- 4
- 3
Kumekuwa na msemo usemao "VIJANA TAIFA LA KESHO" msemo ambao nimekuwa nikiufanyia uchunguzi kwa muda sasa na nimegundua kuwa msemo huu umekuwa chanzo cha kutudumaza kifikra ama kutufungia nje sisi vijanana taifa letu, kifungo ambacho nakiita kifungo huru huku tukisubiri kesho yetu ifike, cha ajabu haupo msemo tena au hayupo wa kutukumbusha kuwa kesho yetu imefika sasa, ila hapo ndo inabaki jitihada binafsi ya kila mmoja wetu namna atakavyojaaliwa kupenya ili aipate kesho yake.
Kwani tumekuwa na vijana wengi wasomi wa makaratasi tu lakini hatujitambui kwamba sisi ni akina nani katika taifa hili na tuna mchango upi? na tupo duniani kufanya nini? Maana wengi tumesoma kwa mikopo ambayo ni pesa ya walipa kodi na wengine tumesomeshwa na wazazi masikini ili baadae tulipe ama wazazi waone matunda, leo utakuta vijana hao hao ndo wanaingia katika makundi mabaya na elimu zao, mbaya zaidi elimu hiyo hiyo wanaitumia kufanya uhalifu katika nchi yao.
Kwa vile tu hawajui wafanye nini basi ili wawe faida ya jamii na nchi kwa ujumla kupitia elimu yao,maana msemo huu hauwapi nafasi nafasi ya kujishughulisha na utaifa wakiwa bado wadogo ama baada ya kumaliza masomo yao,msemo huu hauwaandai kivyovyote kutumika kuja kuwa walipakodi wazuri baadae,kwani katika kusoma kwao wengi huamini kuwa baada ya kusoma ni ajira ofisini! hiyo ndo kesho yao inayoimbwa na msemo huu.
Katika uchunguzi wangu nilipata msemo mpya ambao ni "VIJANA TAIFA CHANGA" Msemo huu unajichambua wenyewe kwamba kijana anakuwa mwana taifa mchanga, kwani maana hata mtoto akizaliwa haitwi mtu wa kesho au mtoto mkubwa wa kesho bali huitwa mchanga au mtoto mchanga.
Labda nitoe mfano hai kidogo
"mimi ni naitwa jackie maduhu miyeye ni baba wa watoto wawili,mkubwa anaitwa steven na mdogo joseph
Siku moja nikiwa najiandaa kwenda kazini mtoto mkubwa akanililia niende nae kazini ila kwa vile kazini mbali na kulingana na umri wake nikaona nikienda nae sitafanya kazi maana alikuwa na umri wa miaka 7 ila nikamwambia kwamba "wewe ni fundi wa kesho" ikawa kila siku anauliza "baba kesho ntaenda kazini namimi?" Namkubalia ila mpaka nikachoka kumjibu ikatokea siku nikabadilisha baada ya uchunguzi wangu na kumwambia kwamba "wewe ni fundi mdogo ukiwa mkubwa utakuwa fundi mzuri sana" akadakia "kwanini baba kama mimi ni fundi mdogo usiniletee na mimi vi simu vidogo nitengeneze?" Kweli nikamwahidi nikamletea kesi ikaisha,
POINTI
Point kwa vijana wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine tumejaaliwa ujuzi mbalimbali tutambueni kuwa tunaishi mara moja tu,tukifa na ujuzi wegu umekufa,tuwekezeni ujuzi ili taifa letu liwe na vijana wengi wa maana na wenye faida kitaifa.wengi wanakufa wanazikwa na ujuzi wao bila hata kubakiza kama mbegu kwa taifa,huku vijana maelfu wakibaki wazurulaji bila mchango kwa taifa, na ikitokea mmoja wapo akapata majanga yoyote taifa tena linaingia gharama kumsitiri kijana mwenzetu, SWALI je serikali ipo kwa ajili ya kuingia gharama mtu anapofikwa na mabaya tu? Kwanini hiyo gharama isitumike kumjenga ili awe nyota kwa wengine kuanzia familia, jamii na taifa?
WITO
Serikali ni watu, na watu ndo sisi,hivyo vijana wote ambao tuna ujuzi wowote ambao ni halali tujitokeze kuwafundisha vijana wenzegu hata bure au kwa gharama kidogo ili tulikwamua taifa, tuanzisheni program inayoenda na msemo mpya wa vijana taifa changa ili tukusanye vijana na kuwapa ujuzi wowote kulingana na upendeleo wao,hapo tunaweza kuanzisha program nzuri tukaomba ushauri serikalini ama taasisi binafsi,ili kwa ajili ya kupata challenges tukawa na tamasha kwa kila mwaka kuwakutanisha vijana wote nchi nzima ambao wako ndani ya mpango wa "VIJANA TAIFA CHANGA", na program hiyo tukaipa jina la "VIJANA CHANYA" ili kuleta chachu kwa vijana na kuona wanathaminiwa na kubadilishana uzoefu kulingana na ujuzi mbalimbali,hapo hata serikali inaweza kuubariki mpango huu
MFANO HAI
Mwezi wa nne nilitafuta vijana 7 wa kike wawili wa kiume watano,wa kike wakachangua ushonaji,wa kiume wawili ninao nawafundisha ufundi simu,watatu walichagua useremala,nilichokifanya nilitafuta wanawake wawili washonaji nikawashirikisha kuwa kama wadau nikawahamasisha kweli wakakubali kuwapokea hao mabinti kuwafundisha bure kabisa, kwa upande wa useremala waliomba wachangiwe kidogo hao mafundi ikabidi niwatembelee wazaz wa hao vijana nikawasihi wakafunguka na vijana mpaka saiv wanaendelea na mafunzo, unadhan hao wakikamilika na kuwa na ofisi zao watakataa nikiwapelekea tena vijana wenzao ili nao wawafundishe? Je kwa mtiririko huo ndan ya miaka mitano nitakuwa nimetenda msaada kwa vijana wangapi?
TUINUANE SISI KWA SISI ILI TUJENGE NCHI YETU

Upvote
6