Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Huu ni uzi wa wazo yakinifu kwa fikra mrejeo,
Kama mada inavyosema, watu walilaghaiwa wakalaghaika kwa ulaghai wa kilaghai mwisho wa sike mchumba kabebwa na ambaye aliwaangukia akikiri yeye ni kama wao, hana kitu, wanamfahamu, hatanii na akatoa tahadhari harusi waliyoahidiwa kesho yake haitafanyika kwa kuwa mlaghai ana safari kesho hiyo hiyo hivyo watapoteza lakini baadhi walipuuza na wachache wengine wakashituka saa za mwisho kubadili uamuzi.
Kesho yake ilipofika mlaghai kweli akaonekana amepanda kaa wa kigeni kisha akashuka na kupanda ungo ulioandaliwa kubebwa juu angani kwa upepo wa kisulisuli. Dakika chache baadae upepo ulivuma kutokea kusini kuelekea kaskazini, ghafla ungo ukageuka mshale na kutoweka na laghai.
Baada ya saa kadhaa mmiliki wa kaa wa kigeni na ungo mshale alisikika akithibitisha kwamba laghai hatimaye amefika sehemu njema ya mapumziko ya mtima huku vijana wakishindwa kujua kulikoni?
TAFAKURI