Vijana tunayumba sana

Vijana tunayumba sana

Emar

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
1,789
Reaction score
2,965
Salute,

Naomba nianze kwa kunukuu na kunukuu baadhi ya mistari kwenye vitabu vya dini
"Mwanume utakula kwa jasho"
"Ewe mvivu mwendee chungu"
" Asiye fanya kazi na asile"
"Hapa kazi tu"

Okay tuendelee, jana mida fulani hivi katika harakati za mjini hapa na pale nikajikuta nimedondokea maeneo ya Kinondoni. Ila wakati nipo maeneo hayo mara ghafla nikakutana na nyomi ya wanawake na wabinti ilikuwa kama ishirini kwenda hamsini na wengine wanazidi kuingia.

Mtu mzima nikasema hawa wanaenda wapi? Mawazo yaliokuja kichwani
- Kuna mtu kafumaniwa
- Vicoba
- Kuna kusutwa
- Kuna shughuli

Ikabidi nijisogeze sasa wakati najisogeza, dah kuja kuona wanachokifanya nilichoka kabisa, eti foleni mpaka barabari eti wanapakwa rangi kwenye kucha dah! Mimi kwa girlfriend wangu sijawahi kuwa na times na kucha zake ingawa anapakaga, eh kumbe ndo kazi hivi. Nikasema asante Mungu kuwa wa kiume.

Ila niliangalia lile nyomi nikaangalia katika mtazamo wa kibiashara nikasema yule jamaa anafanya scrub, kucha, sijui anaosha miguu nikasema kama ni 50 na wakamwachia 10000 kila mtu jamaa atakuwa na 500000 Sh kwa siku nikashtuka inamaana ana zaidi ya 10 M kwa mwezi, ambao ni zaidi ya mshahara wa mzee wa hapa kazi tu.

Nikakumbuka kuna jamaa alikuwa Posta alikuwa alikuwa muosha magari alikuwa anaondoka na hela hiyo kwa siku .
Yeye anaosha gari 3000 Sh na alikuwa na access ya kuosha magari mpaka 50.

Nikasema vijana wanakwama wapi kwanini unafikiria ajira tu, ili upewe laki tano uendeshe IST. Eti utamkuta mtu yupo nyumbani anasubiri Rais Magufuli atoe ajira ana miaka miwili anangoja chai ya shikamoo. Hebu fikiria unaweza kuta jamaa ana ndinga na gari kali kazi yake mpaka rangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na Ukweli huu jiandae for Criticism
 
Hii hesabu ya kuosha gari moja kwa Tshs: 30000/= mara magari 50 kwa siku haina uhalisia - ni porojo tu
 
Back
Top Bottom