Vijana tusiozidi miaka 25 ambao tupo humu JF tukutane hapa

Vijana tusiozidi miaka 25 ambao tupo humu JF tukutane hapa

Niliijua JF kwakua mimi ni mtu wa kusoma soma online nilikua namsoma Dinahcious & co kuna siku nikiwa nasearch online story yenye kutisha ikaja link ya jf. Nilivyoingia na kuzidi kuperuzi nikakuta stori ya jamaa ambaye alitaitiwa na vibaka akiwa na mpenzi wake wakataka kumlawiti mshkaji, jamaa akakimbia akamuacha mke.

Niko mtaani, najitegemea ila soon narudisha mpira kwa kipa.

Kwa wazee ilinibidi tu nitoke sikua na option. Ila sitaelezea kilichotokea.

Bado nasota mtaani.

Sijaoa. Sipo single.
Usirudishe mpira kwa kipa mkuu
 
Jf niliifahamu kipindi nipo form 4, awamu ya pili ya J.K. Nilikuwa msomaji tuuu mpaka nilipomaliza form 6 ndiyo nikajiunga kwa mara ya kwanza.
Siku ya kwanza tu kuweka bandiko humu nilijibiwa "pumba" na mkuu bulldog, nilipanic sana ila baadae nikajifunza namna ya ku-handle matters online.

Nipo ghetto naendelea na harakati za kuboresha kesho yangu, chuo nimeshamaliza tayari ila mambo bado hayajawa "mswanu", tunakomaa kimtaa-mtaa.
Bulldog hutamsahau kwa alichokufanyia hahaa
 
JF nilifaham nikiwa na miaka 15 mwaka 2012 nilikua kidato cha 3 ..
Nilisha fungua ID kama 2 apo nyuma ila zote nilisha sahau nywila zake.
The Bold ni moja ya watu walio fanya nijiunge JF kwa zile Nyuzi zake
 
Ilikuwa 2011 nlianza kuifahamu kupitia kaka wa rafiki yangu.. kipindi hicho sikuwa na cm wala pc nlikuwa natumia techno bapa hivi ..kupitia operamini nkawa naingia na kusave simulizi mbali mbali na baadhi ya materials kwenye thread ya jukwaa la Elimu ..hata hivo mwezi wa 11 ndo nimejirejista rasmi kama memba wa JF ..Huwa napenda kuwa humu ndani kwasababu ya utofauti mkubwa na social network zingine tu
 
Kuna watu wengi saana pia walionifanya niipende JF nkimtaja mmoja wengine watajiona nothing ...ila ni weengi saana huwa wanaandika point sana humu ndani
 
Niliwahi kuwa member wa jf mwaka 2013

Nikajipa break mpaka mwaka nmejiunga tena lakini cha kushangaza hata miaka 25 sijafikisha
 
Wakuu member tajwa hapo juu wa uzi huu huwa tuna mambo mengi sanaa...
Ukipata penzi linalo noga (mahusiano) ni rahis kupotea JF,

Ukiwa masomon kipind cha paper ni rahis kupotea JF

Ukisafir ukaenda sehemu ambayo hujaenda siku nying pia kukaa na cmu sana ni ngumu.

Ukianza biashara za kutwa nzima,

Muda wa mpira...
Kukaaa vijiweni..
Ku watch movies
Kufanya kazi za hapa na pale,
Kutafuta hela kwa nguvu,
Mala nyingi twaweza kuwa busy.

Mimi naona tunahitaji sana ushirikiano kwa wakati huu ili kila mmoja wetu aone umuhimu wa uzi huu tajwa hapo juu.

Na mimi naona walio na rika hili tajwa hapo juu ndio watu muhimu zaidi humu JF, ukiacha kwa mambo ya siasa.
 
Back
Top Bottom