PreGE2025 Vijana UVCCM Bukoba Vijijini Walalamikia Kukwama kwa Kampeni ya SANEVO ya Rais Samia

PreGE2025 Vijana UVCCM Bukoba Vijijini Walalamikia Kukwama kwa Kampeni ya SANEVO ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Vijana wa umoja wa UVCCM wilaya ya Bukoba Vijijini wamelalamikia kukwama kwa kampeini ya kutafuta kura mpya za Rais Samia inayoitwa Samia New Voters Campagn (SANEVO) iliyopangwa kufanyika wilayani humo mwishoni mwa mwezi machi, mwaka huu 2025.

Wakiongea na Vyombo vya habari mara baada ya kutokea sintofahamu baadhi ya viongozi wa vijana hao wameeleza vurugu zote zilizotokea zimeratibiwa na kikundi cha vijana ambao wanasemekana wanatumwa na mbunge wa jimbo hilo kumuhujumu Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Faris Buruan na kamati yake.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ziara ya hiyo iliyoanza tarehe 10 mwezi huu ilianzia wilayani Karagwe ikilenga kuyafikia makundi mbalimbali kutafuta kura mpya ya Rais Samia akiwa ndiye mgombea pekee aliyepitishwa na chama chao.

 
Back
Top Bottom