Vijana wa 1980's tunaelekea kuwakana mastaa tuliokua nao, tuliiga kila aina ya maisha waliyoishi, hatukujua ya sirini

Vijana wa 1980's tunaelekea kuwakana mastaa tuliokua nao, tuliiga kila aina ya maisha waliyoishi, hatukujua ya sirini

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Siku zinakwenda namkumbuka Tupac Amar Shakur 2Pac msanii mwenye sauti yenye nguvu katika muziki wa hip hop,Alijitokeza sana kuhamasisha vijana na jamii kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa,Nyimbo zake nyingi ziliangazia ubaguzi wa rangi,umaskini, na ukosefu wa haki za kijamii,je angekuwepo hai hivi leo yangemkuta ya P.Diddy au ya R.Kelly?

RIP Notorious B.I.G.:Christopher Wallace,je ungeungana na Kanye West,50 Cent,Meek Mill kumshambulia P. Diddy kwamba tuhuma zake ni za kweli,Bad Boy Entertainment,Death Row, Suge Knight,Dr. Dre,Snoop Dog Doggy,Nas,Jay Z,Eminem,je tutarajie mengine mengi ya sirini kuwekwa wazi,sisi vijana wa 1980's tutakosa mastaa wa kujivunia tuliokua nao.

Je ni vita kati ya Wazungu na Blacks kule Marekani Au ni Vita ya Blacks vs Blacks,pamekuwa na mfululizo wa kesi zinazofanana kuwahusu Blacks kule America (Vita Dhidi ya Blacks) ilianza kwa R.Kelly the pide piper sasa ni Puff Daddy,je tuhuma zao ni za kweli!? Kuna msanii wa Marekani nilimsikia akitoa ushuhuda ya kwamba ukialikwa kwa P. Diddy kuna kitabu maalumu inatakiwa usaini kwamba utakachokiona huko hutakiwi kusema kitu ambacho hata yule jamaa yetu wa Tandale alisema,kwa taarifa na evidences za mitandaoni tunaweza kuhukumu ni kweli P.Diddy alikuwa mchafu wa tabia lakini je si Movie za Hollywood!?

Niliangalia interview ya Manager wa jamaa yetu wa Tandale anasema walivyoenda Marekani kuonana na P.Diddy jamaa aliwakaribisha chumbani kwake wakacheck movie Swizz bitz aliyekuwa mwenyeji wao akawa mkali hakutaka jamaa waende,wakaona kama Swizz anawabania ila walikuja kuelewa baadae,Nadhani Producer Swizz Alikuwa anaelewa uchafu wa Puffy Daddy,kuna clip ya video ya Mike "Iron" Tyson anasema aliutoa mkono wa Puffy Daddy uliokuwa unaelekea kumchezea,na baada ya kipindi alimwambia aheshimu mipaka,yeye mbweha na mbweha halaliwi,

Soma Pia: Waendesha Mashtaka wadai nyumba ya Diddy ilikutwa na Vilainishi, Silaha, Dawa za Kulevya, Mafuta ya Watoto Chupa zaidi ya 1000

"I was almost losing my steeze when I jokingly removed his hands and shifted myself away from him and we both laughed over it"

But after the show, when we were off cam, I walked up straight to him and i said.

"LOOK MAN, LETS RESPECT BOUNDARIES, I AM A TIGER and TIGERS DONT GET LAID"----Mike "Iron"Tyson.

Je niseme nini wazungu wamefanikiwa kuutoa ukuu wa mwafrika kwenye tasnia ya muziki au nionye kuwa ufakara unakera lakini pia malengo makubwa kuliko uwezo wako yasikupeleke kucheki movie na P.Diddy. I need a girl.
 
Hahahahahaha tusiwasingizie wazungu, WaAfrica tunajuana tabia zetu, wanachofanya wazungu nikuanika tu ujinga tu.

Hata hapa bongo zipo tetesi kitambo kuna jamaa anawatoboa vijana wetu kwa issue zilezile za tamaa zao, ingekuwa Kwa wenzetu tayari watu wangeingia kazini na kuanika ujinga woote.

Vijana wanashine mjini wameanzisha tasnia mpya wanajiita machawa na kusaka noti.
 
Back
Top Bottom