Vijana wa 90's wanahisi kuchelewa, wanahitaji mabadiliko ya upesi

Vijana wa 90's wanahisi kuchelewa, wanahitaji mabadiliko ya upesi

05CUBA

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2025
Posts
1,106
Reaction score
1,650
Kutoka Kila chama, TAALUMA na mazingira mahitaji ya vijana wanaochipukia utu uzima yanafanana.

Vijana wote wa kitanzania waliozaliwa myaka ya 90 mpaka 99 wanahitaji hoja za mabadiriko na utekelezaji wa hoja husika.

Hivyo kunapoelekea uchaguzi wa 2025 vijana wanahitaji kusikia na kuona hoja na mikakati mabadiriko ya kuwavusha .upesi mahali wamekwama.

Japo Kuna kugawanywa kwa itikadi za vyama na mirengo ya kushughurikia mahitaji husika Ila hii haipingiki Tanzania inahitaji mageuzi makubwa.

Wale wanaoshabikia mfumo ambao ni radical (mrengo wa kulia), moderate (mrengo wa Kati), na mengo tulivu (mrengo wa kushoto) mahitaji yanafanana.

My take: vijana wakiungana na kuweka tofaut pembeni mahitaji yote yanaweza fikiwa upesi kuliko wakitengana.

Janja janja za wanasiasa wenye maslahi binafsi zinatuchelewesha Sana Ila vijana tulipaswa kuwa na kauli zinazofanana juu ya mustakabali wa taifa letu japo tuo na mirengo au Imani zinazotofautiana.

Japo ni ngumu Ila ni rahisi Sana vijana Kwapamoja wakaomba katiba mpya , kuwajibishwa kwa wezi na mafisadi, kuongeza fursa na nafasi za Ajira, kuboresha maslahi kwa wafanya kazi, kuboresha mfumo wa

Huduma za jamii kwa ujumla , kuboreshwa kwa Hali za kiusalima na ulinzi Huku haki za binafamu zikiangaziwa zaidi, kuwezeshwa kwa vijana wajasiriamali na wafanya biashara wadogo wadogo, kuweka kwa mifumo rafiki ya Kodi na ukuswanyaji wa mapato navingine vyote .....

Vijana wakiungana bila chuki kesho ahsubuhi tz inaanza kusogea mbele.

#siasa
 
30 May 2025
COSS UDSM
Tanzania

PAN-AFRICANISM IS STILL RELEVANT : REVIVING THE SPIRIT OF UNITY, EMPOWERMENT AND PROGRESS FOR AFRICA


View: https://m.youtube.com/watch?v=XaudQf55Sn0
Pan Africanism started as a movement not from the existing centre of power governed by the ruling class.

Red carpet Pan Africanism no political space, questioning the status quo including Tanzania is not allowed, only Chawa-ism is allowed in our current political space...
 
Back
Top Bottom