R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Wanatumia pikipiki ya kichina zisizo za michezo kufanya michezo, hawana helmet, gloves ngumu, guard ya viwiko, guard ya magoti, safe jacket, suruali ngumu, buti, begi lenye sponji, n.k.
mwendo wa Ngiri mkia juu, kasi ya kuwapumzisha wadudu inazidi kuwa kubwa, vifo vingne nikujitakia sio Mungu kupenda, family zinapoteza watu zinabaki kwenye majonzi kwasababu ya haya mambo, kabla ya vifo wanashauriwa sana na wao wenyewe wanaona jinsi wenzao wanavyofekwa na haya machuma lakini bado wanajitia wajuaji.
Piki piki hizi wanazotumia ni kama Toyo, kinglion, fekkon na San Lg. Hizi piki piki ni za daraja la chini sana na hazijatengenezwa kwa kufanyia kazi hizo hata wachina wenyewe wakiwaona wanashangaa vijana hawa waliogeuza maisha yao kama shilingi inayochezewa kwenye tundu la chooni.
wanaoteseka ni watoto wanaoachwa yatima, baba zao wanatangulia kwa kujitakia kabisa, watoto wanaanza kuishi maisha magumu na hawana hatia.
CONCLUSION
chuma zina spea ila mwili wako hauna spea, kikiumana mda wowote ni family yako, watoto wako na mamiloo ndio watapata shida, tujaribuni kuzitumia kistaarabu, ata wachina walio tengengeza sijawah ona wakitembea nayo tairi juu, kama huu mchezo unaupenda sana ni vema ukajichanga ununue bike ambayo iko special kwa ajili hii michezo pamoja na vifaa vya usalama,