Vijana wa Bodaboda kuweni makini, vinginevyo mtaisha

Vijana wa Bodaboda kuweni makini, vinginevyo mtaisha

Von_Lufuta

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2023
Posts
1,528
Reaction score
3,641
Wakuu habarini za wakati huu..

Nipo Pwani huku wilaya ya Rufiji kuna Kijiji kinaitwa Mloka, mida ya jioni hii kuna kijana wa Bodaboda kapata ajali mbaya sana.

Kama mnavyojua maeneo haya gari za kutembeza watalii ni nyingi sana, sasa kuna vijana kama watatu walikuwa kwenye kushindana kumwaga moto. Kuna mmoja alikuwa anaendesha huku kazima taa kabisa halafu mwendo wake ulikuwa mkali sana na bashasha za kutosha maana aliivuta Ili kuwa overtake wale wenzake na alifanikiwa lakini muda Ule anamalizia kumpita wa mwisho alikuwa kageuza shingo kuwaangalia wenzie kitu ambacho ni hatari sana kwenye pikipiki, muda huo taa hajawasha na ni usiku.

Barabara waliokuwa wanaelekea kulikuwa na gari ya kubeba watalii ikiwa mwendo wa kawaida tu kuelekea wanapotoka wao, sasa chalii Ile anageuka tu kakuta gari ipo karibu hata jinsi ya kuamua haraka kurudi upande wake isingekuwa rahisi..

Aisee.. alisikika tu akitoa sauti "uuuuuuuh" Kisha kishindo Cha maana kikasikika baada ya kupiga pale kwenye gari..

Watu walijaa ndani ya muda mfupi kuja kumpa msaada maana alionekana kazima kabisa baada ya kuburuzwa kwa sekunde kadhaa..

Sijui atakuwa kwenye Hali Gani maana nilihisi kuchanganyikiwa, isitoshe huwa sipendi kuona tukio la vile. Nilikimbia eneo lile.

Cha kuwaomba tu Bodaboda acheni michezo ya hatari na pikipiki, mtakwisha, mtaingiza familia zenu matatizoni ambazo yawezekana nyie ndio mnaotegemewa, mtaharibu future zenu. Kuna ulazima Gani wa kuweka league na kumiliki barabara?

Kuweni na hekima na busara kwenye kuamua mambo kabla hamjaingia matatizoni.

NI HAYO TU
 
Baadhi wanabalehe kwenye pikipiki,yaani wanafanya mambo ya foolish age,kwenye boda,matokeo yake,wanawapa shida wazazi wao,kwa kuumia vibaya,na kuishia kukaa ICU muda mrefu na meishowe kuwafilisi wazazi wao.
Wanahatarisha maisha yao kwa makusudi kabisa. Wengi ni under 25 ndio wana michezo hiyo ya hatari.
 
Back
Top Bottom