Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,903
- 3,139
Hivi karibuni kuna vijana (kwa akili zao timamu) wameaumua kuunga mkono Chama cha Mapinduzi. Wakiwa wanaonyesha support kwa Serikali na chama kwenye mitandao ya kijamii, wamepokea kejeri, matusi na lawama kwa vijana wengi sana; sasa jambo hili limewafanya wahisi vijana wao wanaona wajinga, mazwazwa, wapumbavu au watu waliopeleka matumbo yao na si maslahi ya uma wa Watanzania.
Kwanza kabisa muelewe, hicho mnacholalamika ninyi; vijana wa vyama vya Upinzani, hususan CDM tumekuwa tukikililia miaka yote, onjeni utamu wa mitazamo ya uma dhidi yenu; kwa maana wenzetu tumekuwa tukionekana wavunjifu wa amani, wajuaji, wagomvi, viburi na wapenda shari. Kweli nimeamini "Bichwa halioni mwenge" yaani ni kweli "Nyani haoni kundule" hivi mnafahamu gharama za kuwa mwanachama wa CDM kwenye hii nchi? Hususan ukawa unajulikana na unataka huduma za Kijamii? Ukawa unataka kufanya deals, au uwe Mfanyabiashara mkubwa halafu uwe Mfuasi au Mwanachama wa CDM? Mnachekesha nyie.
Vijana wa CCM waliwahi kunigharimu maisha yangu, nilipoteza kazi kwa sababu ya Upumbavu wao, na namna wanawaona vijana wa CDM, japo sikuwahi kujihusisha na siasa, au kutambulika kama Mfuasi wa CDM wakati nipo kazini.
KISA KILIKUWA HIVI;
Miaka mitatu nyuma nilikuwa kwenye kipindi kigumu sana cha maisha yangu, kiasi kwamba ilifika wakati nilijisemea hata nikipata kazi ikanilipa Shilingi 250,000 ningeifanya, kwa maana hata kula yangu ilikuwa ya shida, katika kuhangaika kutafuta kazi za Ualimu nikabahatika shule moja ya Private kule Mbezi, kwa kweli katika siku niliyomshukuru Mungu ni pamoja na ile, kwa sababu hali ya maisha yangu ilinifanya nione sasa nimekombolewa, ile shule nilikuwa situmii nauli kwenda, japo ni parefu lakini nilikuwa nakomaa, "mtafutaji hachoki" nilipewa Mkataba wa Muda wa Uangalizi (probation contract), kwa miezi mitatu; moyoni nilijisemea lazima nikomae kupata mkataba, na ningefanya kazi kwa jitihada zote. Ile shule nilikuta wapo kwenye kipindi cha mitihani, nilipewa darasa nisimamie; kwa sababu ya uzoefu wa muda mfupi niliiweza ile kazi.
Baada ya mitihani ilikuwa kufanya masahihisho, sasa hapa ndipo shughuli ilianza, kwa kuwa nilikuwa nafundisha somo la Kiingereza, nilikuwa nikifanya masahihisho wa swali la kuainisha (matching the items), kwenye kipengele B kulikuwa na chaguo lililosoma "Death of the President". Sasa nikawaambia wanafunzi watoe wa mfano wa kifo cha Rais, of course walimtaja Hayati Magufuli, ila kuna dogo mmoja ambaye ndiye aliyezusha haya yote akanyoosha mkono; nikampa nafasi ya kuongea; akasema japo wakati Magufuli yupo hai alikuwa mdogo lakini anajua tofauti ya upatikanaji wa umeme kwenye enzi yake na hii ya Rais Samia. Akasema sasa hivi nyumbani kwao umeme unakatikakatika hovyo kiasi kwamba kuna siku ilimpasa aje shule bila kupiga pasi, na wakati mwingine wanashindwa ku operate vifaa kadhaa ya umeme nyumbani kwao, hili jambo likazua mjadala mule ndani; kila mwanafunzi akawa na la kusema, wengine wakaanza kulaumu kabisa, tena kwa sauti; sasa kwenye jaribio la kuwanyamazisha ili niendelee na kipindi ikabidi nitumie sauti ya juu zaidi, na wakati huo Mkuu wa Shule alikuwa akipita nje, so akasikia. Akaja moja kwa moja darasani kwetu. Akauliza "Mwalimu wanakusumbua hawa?" nikamwambia "Hapana, ila kuna wachache walikuwa kwenye mjadala wakati nafundisha" sasa kwenye kuanza kuuliza uliza yule dogo akanyanyuka tena, na kutoa maelezo yale yale; sasa Mkuu akahisi kwamba mimi nawalisha watoto maoni yangu ya Kisiasa kuhusu utawala uliopo; ikabidi ninyamaze, ila akatoka nje halafu akarudi tena ndani akaniambia nimuone ofisini.
Baada ya kipindi nikamona ofisini, akaanza kutoa maelezo ya kunionya kuhusu kuhubiri siasa shuleni, ila mimi nikamueleza kwamba sikuwa nawaambia Wanafunzi wala kuwapandikiza chochote kuhusu siasa; tukamalizana hivyo nikatoka nje, tulikaa likizo fupi ya kama wiki moja ambapo ilipindukia wiki ambayo ulikuwa unaingia mwezi mwingine, ule mwezi wiki ya kwanza tu, ilikuwa siku ya Ijumaa nikaitwa ofisini, nikaona ananitolea barua ananipa, sasa sikuwa najua ni barua ya nini; ila nilipofika ofisini (staff room) kuifungua nikakuta ni BARUA YA ONYO kuhusu lile jambo lililotokea siku ile, nikawa naongea na moja ya walimu pale, nikamuelezea kilichotokea kisha ndio akanijulisha kwamba ile shule ilikuwa inaendeshwa na Makada wa Chama cha Mapinduzi, kuanzia kwa Mtaaluma mpaka Mkurugenzi, ni jambo ambalo lilinihuzunisha sana.
Nilifanya kazi mpaka ule mwezi ulipoisha; ukabaki mwezi wangu mmoja wa mwisho wa probation, nikapokea barua ya kutoridhishwa na mwenendo, japo Mtaaluma hakutaka kuniletea ile barua, akawa anagombana na Mkuu wa Shule, baadae Mtaaluma akaniambia nisijali anaongea na Mkurugenzi ili ikiwezekana niende kwenye shule yake nyingine iliyopo Kibaha huko (kama ningependa) akaniambia ikiwa wangenitetea niwepo pale ningekuwa na wakati mgumu na Mkuu wa Shule, nikamwambia haina haja; Walimu wengine waliposikia ile kesi walimind sana, nikaona siwezi kuishi kwa huruma yao; ngoja nimalize mwezi mmoja bila shida niondoke. Mind you, jamaa ni kijana mdogo sana; hakuwa hata na 35, namimi sikuwahi kuwa na discpline case yoyote ile, sijawahi kuchelewa, kutegea kipindi au jukumu lolote lile. Baadae Mkuu Msaidizi alinipa connection ya shule nyingine, ila hakuwaambia kama nilitoka pale kwake, na aliniambia "usiwaambie umetoka huku" baada ya ile probation na kulipwa ule mshahara wa mwezi ule niliondoka nikahamia kule nilipoelekezwa. Nikaanza kazi rasmi, licha ya kwamba mwaka jana mwishoni nilihama.
Ila wito wangu kwa vijana wa CCM, kwa kuwa mnahisi mna hati miliki ya hii nchi, twendeni hivi hivi; kuna mahala hivi karibuni tutafika; Kwa maana siku hizi tumeona mna Confidence ya kutangaza kuwafanyia ubaya watakaompinga Rais wenu bila ya ninyi kuchukuliwa hatua, ila anayetoa maoni bila uvunjifu wa sheria ni aidha atekwe, akamatwe au afanyiwe figisu ya kwenye shughuli zake. Hamuwezi kubadili msimamo na imani yetu. Ikiwa mnaweza tumalizeni wote ndipo muishi kwa amani, ila hatuwezi kuishi mtakavyo ninyi as if nchi haina sheria.
NRNE.