Vijana wa Dar na ajira mpya ya kubet

Ujumbe mzuri sana.. Lakini JF wana thread yao kule tena imewekwa pin kabisa ....

Wanawadumaza akili vijana wetu, inabidi serikali iangalie kwa jicho la tatu hii cancer maana ikishakomaa itakuwa ngumu kutibu


Kubet ni ajira sema sio favourable kwako
 
Unaweza kuwa na uwezo wa kufikiri ila ukafikiri upumbavu...Mtu kapost kitu cha maana ila unacommet upumbavu ..adilikeni Ndugu zangu acheni sifa za kipuuzu kwenye mambo ya msingi
 
Vijana wengi (sio wote) wanapenda maisha ya kwenye tamthilia ambazo hazina uhalisia. Hawapendi kazi lakini wanapenda maisha mazuri (gari, nyumba na mke wa maonyesho). Vijana acheni ujinga fanyeni kazi. Betting na pool hazitawafikisha popote. sio vyanzo endelevu. Baadae mtasema serikali. Na mwisho mtatamani kuiba na hamtaweza kuiba maana akili zitakuwa zimeshaoza
 

Tuseme Uwe unashinda tu na hao wenye michezo wana poteza hela, undhani kuna mtu anaye taka kupoteza hela hivyo, je wao watakua wanapata faida gani?
Leo kama umeshinda ujue kesho utapoteza, huu mchezo ndio unaanza sasa hapo TZ huku ulaya inamiaka mingi tu na kuna watu wamepoteza hela zao chungu nzima
Huu mchezo ni hatari sana
 
Mhindi wa betting anapiga profit before tax ya 2bil per day, unajua serikali inapata kodi kiasi gani hapo?
 
Wafunge betting shops maana zimezidi sana
 
how old are you ..?! mtu mwenye akili zake hawezi akasema kamari ni ajira


Mimi nina miaka 39 kama kubet sio ajira wafunge izo cassino lofa wewe

Watu wanalipa kodi unasema sio ajira

Sema wanaobet wengi wao hawana elimu kuhusu ili swala Trump mwenyewe huwa anabet, ile ni biashara kama zilivyo zingine maana zipo kihalali
 
Mimi nina miaka 39 kama kubet sio ajira wafunge izo cassino lofa wewe

Watu wanalipa kodi unasema sio ajira

Sema wanaobet wengi wao hawana elimu kuhusu ili swala Trump mwenyewe huwa anabet, ile ni biashara kama zilivyo zingine maana zipo kihalali
Wengi hatuelewi maana ya neno ajira, kwa uelewa wangu mdogo ajira ni shughuli yoyote inayokuingizia kipato halali.
Kwa maana hiyo kubet ni ajira ila sio rasmi na inaingiza kipato inalipa kodi sasa mtu anayesemaje kubet sio ajira?

Alafu haina madhara kama mnavyotaka kutuaminisha, huu mchezo unahusika na soka kama hujui lolote kuhusu soka nakushauri usibet utafeli na sio kubet hata biashara yoyote iwe kilimo au ufugaji kama hujui lolote utafeli pia
Watu tunampiga muhindi daily ukisema niache kubet hata sikuelewi
 


Good point kichuna

Kitu kama huna ujuzi nacho unakifuata cha nini
 
Mimi nimejenga na kununua gar kupitia betting, msitake kutuharibia kazi yetu hii pendwa
 
Hawa jamaa wanatuchukilia poa sana hawa.
 
Kuna yale mokochokocho mengine ya kudumbukiza token yaliyofungwa na wahindi au wachina kwenye vibanda na bar ndo balaa kabsa...
Alafu hayo sijui huwa yanachezwaje, nikipata mtu wa kunifundisha nitashukuru sana
 



Naomba mwangaza wa kubet, hivi wanapocheza mfano Yanga na Majimaji au Jana Barca na Arsenal ambapo timu inayoshinda inajulikana tu, kwahiyo inatosha tu kuweka hela labda 100,000 na kusema Yanga / Barcelona itashinda mechi hii au hadi utaje idadi ya magoli na wafungaji wake?
 
Sasa hivi naenda kubett draw ya UEFA champions league itakayofanyika kesho. Ubashiri wangu ni huu

Bayern atapewa A. madrid
R. Madrid vs Man city
Barca vs PSG
Wofsburd vs Benifica
 
Sasa hivi naenda kubett draw ya UEFA champions league itakayofanyika kesho. Ubashiri wangu ni huu

Bayern atapewa A. madrid
R. Madrid vs Man city
Barca vs PSG
Wofsburd vs Benifica

kwahiyo hapo ili upate pesa ni lazima uwe umepatia timu zote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…