Pre GE2025 Vijana wa IT na Computer Science tengenezeni programu itakayowezesha zoezi la Uchaguzi Mkuu kufanyika kwa Uhuru na Haki

Pre GE2025 Vijana wa IT na Computer Science tengenezeni programu itakayowezesha zoezi la Uchaguzi Mkuu kufanyika kwa Uhuru na Haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bando la wiki

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2023
Posts
911
Reaction score
3,017
Sisi kama watanzania tunataka uwazi na haki itendeke wakati wote wa kupiga kura, kutangaza matokeo, na kutangaza mshindi wa uchaguzi wa diwani, mbunge na rais kwa uchunguzi wa 2025.
Japo mifumo yetu ya uchaguzi sio rafiki kufanya uchunguzi mkuu uwe wa uhuru na haki ila ni TAKWA LA WANANCHI kwamba sasa YATOSHA UCHAGUZI MKUU NI LAZIMA UWE NI UWAZI, UHURU NA HAKI. HESHIMA YA WANANCHI KATIKA KUCHAGUA KIONGOZI WAO WANAOMTAKA LAZIMA IZINGATIE KWA 100%.

Sasa mchongo wa kazi kwa vijana wa IT na Computer science kuelekea uchaguzi Mkuu ni huu.

Najua nyie ni watalamu wa software na kutengeneza application mbalimbali. Hivyo vijana wataalamu wa mambo hayo nawapa idea mje na APP MAALUM YA UCHAGUZI MKUU.

iko hivi; kwa kuwa sisi watanzania tunataka uchaguzi ulio huru na haki hivyo settin hii app katika mfumo rahisi wa kuwezesha kupiga kura popote mara moja tu akiwa mahali popote hakuna haja ya kupangana mistari kwenye vituo.

Kufahamu nini kinaendelea kwenye mikoa yote Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu ingia hapa: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sasa kuingia kwenye hiyo app ni mtatumia njia kudhibiti mamluki;
  1. Lazima kila mtu akitaka kuingia kwenye hiyo app atajisajili kwa kutumia NAMBA YAKE YA NIDA.
  2. Atathibitisha Umri wake kama kafikisha umri wa miaka 18
  3. Atataja eneo (kata) alipo ili kuweza kupigia kura diwani wa kata yake, na mbunge wake na rais.
  4. Huyu mwananchi aliyejisajili anaweza kuingia kwenye app hiyo na kuona takwimu za kura zinavyopigwa na matokeo yake.
  5. Serikali itatangaza kupitia hiyo app kura zitapigwa kwa siku ngapi ili kuwafikia wananchi wote.
  6. Dhibiti kwa kutumia NIDA namba hiyo mtu atapiga kura mara moja tu. Hata kama akipiga kura mtandaoni halafu akajikata kwenye kituo kupiga kura manual mfumo hautakubali kwa maana NIDA number yake itasoma ameshapiga kura.
Ndani ya mfumo mtatengeneza kipengele ambacho majiina na picha za wagombea kuanzia diwani, mbunge kulingana na kata na jimbo lake na chama chake wataingizwa kwenye mfumo ili wapigiwe kura.

Mkishamaliza kutengeneza app hiyo muilete kwa wananchi na sisi wananchi tutaitaka serikali iinunue mfumo huo ili itusaidie kuwa na uchunguzi wa huru na haki.

Vijana wa IT mchangamke basi mchongo huo hapo tunataka mabadiliko kwenye nchi yetu zama za analojia zimeshapitwa na wakati.
 
CCM hawatokubali hata siku moja kitu cha namna hiyo.

Uwazi katika upigaji kura , kuhesabu na kutangaza matokeo hiyo ndio itakuwa kwaheri ya CCM.
 
Hata ukiunda huo mfumo. unampatia nani kwa mazingira haya mtu anachukuliwa mchana kwa basi . ..haki haipo katika taifa hili bado kuna kazi ya kufanyika .
 
CCM hawawezi kukubali sababu toka 1995 hawajawahi kushinda uchaguzi wowote....wanatawala nchi ki magumashi magumashi na ndiyo maana wanasema kwa sasa wananchi wana njaa hawawezi kula katiba mpya.
 
CCM hawawezi kukubali sababu toka 1995 hawajawahi kushinda uchaguzi wowote....wanatawala nchi ki magumashi magumashi na ndiyo maana wanasema kwa sasa wananchi wana njaa hawawezi kula katiba mpya.
Wananchi watawashangaza hawa jamaa, unajua kadri watu wanavyopitia ugumu wa maisha huku kundi fulani likionekana linakula mema ya nchi hapo ndipo machafuko huanzia.
 
Wananchi watawashangaza hawa jamaa, unajua kadri watu wanavyopitia ugumu wa maisha huku kundi fulani likionekana linakula mema ya nchi hapo ndipo machafuko huanzia.
Sasa hivi chawa anaishi maisha mazuri mjini kuliko kijana Graduate wa SUA - aliyesota kusoma Kilimo ati wanamwambia akajiajiri mashambani.
 
Back
Top Bottom