Vijana wa JKT wadaiwa kuua

Vijana wa JKT wadaiwa kuua

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1576485226417.png

Baadhi ya Vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Milundikwa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa wanadaiwa kuvamia Kijiji cha Kipande na kutembeza kipigo kikali kwa Wananchi hadi mmoja wao Sabato Mbalamwezi kupoteza maisha.

Inaelezwa kuwa Sabato Mbalamwezi na mwenzie Renatus Wankamba walikamatwa na kuhifadhiwa Kituo cha Polisi kwa tuhuma za kuiba simu yenye thamani ya Tsh 25000, na wakiwa kituoni hapo walifika Vijana watano wa JKT na kuanza kuwaadhibu wakiwatuhumu kuwa wameiba simu ya mwenzao mmoja, Sabato alizidiwa baada ya kipigo na akafariki muda mfupi baada ya kukimbziwa Zahanati.

Wanakijiji walichukizwa na tukio hilo na kuanza kuwashambulia JKT hao hadi mmoja akakimbizwa Hospitali.

Kamanda wa Polisi Rukwa Jutine Masonje amesema Vijana watano wa JKT waliosababisha kifo cha Mbalamwezi wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano na watafikishwa Mahakamani, pia Wanakijiji 35 waliofanya fujo kwa Vijana hao wa JKT wamehojiwa na kuachiwa kwa dhamana.
 
Yaan hao madogo wanakuaga na moto kama wameajiriwa ebu kwanza wakaonje joto La jela na hao wananchi punguzeni jaziba ila mlifanya vizu mlimpa kichapo cha kumfundisha ili na wengine wajifunze
 
Hawa jamaa kuna baadhi yao wana mambo ya kishamba sana aisee acha tu
 
Back
Top Bottom