Vijana wa Kariakoo (mawinga) ni muda sasa wa kurudi vijijini kulima

Ila ukiwa na mshikaji winga huwa wanasaidia sana. Unanua simu kwa bei ya peke yako halafu unamwambia baadaye tuonane las carinyo.

Ila bahati mbaya ikisumua unaona aibu kumrudishia.

Winga oye!
 
Kariakoo haswa hapa China plaza ,congo ,uhuru yote kweny maduka ya simu unaweza kuvutwa shati ,ni kero namna moja
 
Washauri hao unaowaita mawinga wasajili ofisi wabadili Majina Kutoka kuwa winga Hadi kuwa " commission agents"

Walipe Kodi, walipe pango maisha yaendelee.

Usisahau kuwa wewe mwenye duka kariakoo ni winga, sababu unalangua china Kisha unakuja kuuza Kwa retailers, maana huna kiwanda Cha kuzalisha bidhaa unazouza.
 
Kuna winga alitaka kuni Uzia viatu vya 20,000 kwa 25,000-30,000 nika kaza nilivyo muona mwenye duka anasema 20 Tu,winga aka komaa 30 hiyo mwenye duka nae anasema kweli nimekumbuka ni 30, nika ondoka nikajua hapa mtoto winga kazua mikosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…