Vijana wa Kitanzania tutajiajiri vipi au kutengeneza uchumi binafsi ili kuondokana na kuwa tegemezi?

Vijana wa Kitanzania tutajiajiri vipi au kutengeneza uchumi binafsi ili kuondokana na kuwa tegemezi?

Nashauri vijana waanze uwekezaji kwenye masoko ya mitaji. Uwekezaji kwenye masoko ya hisa hasa kwa zile kampuni zinazofanya vizuri ndio msingi ambao unaweza kutengeneza uchumi imara kwa vijana. Kuwekeza kwenye mifuko ya pamoja kama UTT naona ndio suluhisho bora kwa vijana ukizingatia unaweza kutengeneza compound interest. Uwekezaji kwenye government Bonds ni ushauri mzuri kwa vijana.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Tuanzie hapo kwanza sasa hizo hela za uwekezaji anazipata wapi?
 
Fursa zipo tatizo ni exposure, udhubutu na dharau.
vijana wengi wanaishi kwa mazoea na hawana mpango na kupata maarifa mapya ya kibiashara
Thread closed.
Inajua nimejiuliza maswali mengi sana watanzania ni wapi tunakwama.
Nikiwa ughaibuni maeneo ya Airport kila siku naona bidhaa za kutoka Kenya na Uganda wanaexport bidhaa za mazao kama ndizi,avocado na flowers ila sizioni bidhaa za kutoka Tanzania.
Kuna tatizo mahali,badala ya kujikita kwenye kulaumu wanasiasa kila siku hebu tujitathmini ni wapi tunakosea.
 
Hapa ndiposa unahitajika kuweka hiyo Idea ili vijana waichambue nakuikaribia_ karibu tuweze kuipokea kila wazo litaheshimiwa
Mkuu iko hivi ili utoboe unahitaji creativity yako binafsi,yaani lazima uwe na kitu ambacho kipo kwenye passion yako,ni kitu gani ambacho moyo wako unakusukuma ukifanye.
Ukiiga kitu anachofanya mwingine huwezi kutoboa.
 
Ok, kwa Upande wa hisa kwa sasa hata moja unaweza kununua mfano hisa Moja CRDB ina range sh 380-390. Mfuko wa Umoja UTT unaweza kuanzia uwekezaji kwa sh. 10,000/= Hivyo kijana akiamua anaweza kabisa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Kwa sisi wa mikoani tena vijijini tutajuaje soko la hisa tena hatujui pa kuanzia wala utalatibu wa kununua hizo hisa
 
Thread closed.
Inajua nimejiuliza maswali mengi sana watanzania ni wapi tunakwama.
Nikiwa ughaibuni maeneo ya Airport kila siku naona bidhaa za kutoka Kenya na Uganda wanaexport bidhaa za mazao kama ndizi,avocado na flowers ila sizioni bidhaa za kutoka Tanzania.
Kuna tatizo mahali,badala ya kujikita kwenye kulaumu wanasiasa kila siku hebu tujitathmini ni wapi tunakosea.
Wanasiasa wanatumia ujinga wetu kujunufaisha mfano hizo fursa sasa hivi ndio wanaopambana kuzishikilia mpaka tukishktuka wao washamonopol soko tunabaki kulia lia
 
Back
Top Bottom