Vijana wa Kiume badilikeni

Vijana wa Kiume badilikeni

Mkuu Ahsante kwa kuwakumbusha hawa madogo
Ingawa post yako haitasomwa na wengi wao
Mimi niongelee zaidi kwenye wanaume kusahau wajibu wao kama wanaume kwenye familia zao
Once umeamua kuowa!! Jua kwamba kila kitu kwenye familia yako wewe ndio responsible kulijibia na kulimaliza
Ajabu ni kua wanaume tumepoteza sifa yakiume
Tumeingizwa kitu kinaitwa haki sawa!!
Ni aibu
Pesa ya mwanamke ni yakwake
Yeye aamue kufanya kwa familia(hata akigoma usigadhabike)


Ndio maana hua nasema ikiwa hauko tayari kuowa usiowe!
Hiyo haiwezi kutokea kwangu hiyo pesa yake anatakiwa anunue japo mafuta yake au atumie saluni sio kuniomba mimi hivyo vitu wakati ana pesa.

Nyie ndo wahongaji wakuu mnasababisha wanawake wanadanga na kusema kwa nini waolewe wakati wanapata pesa ya kutosha,kwamba ndoa ni umaskini kwao
 
Ni kweli kaka

Ile women empowerment imeleta matokeo chanja sana, kiukweli wanawake wanaobweteka wamebaki wachache nao hao wachache utakuta kuna sababu inayomkwamisha tu

Lakini mwanamke ukimuonyesha njia anafanya wonders, leo wanawake wanacheza vikoba, sijui upatu, kuuza vitenge karanga etc ila wanaume sijui wamepatwa na nini kabisa yani wamebaki kubeti kamari bangi na vitu vingine vibovu tu

Kuna mahali tulikuwa na kikoba watu kumi among of us 9 ni wadada na mmoja ni mkaka, uwezi amini yule kaka tulijuta kumuweka hana plan yeyote, tunakutana kila tarehe mbili ya mwezi unaleta hisa na kama una rejesho unapeleka, yule kaka siku inafika haji wala aleti pesa, siku akija awe alikuwa ana shida ya hela wala hana akisikia tu kuna hela anataka kukopa hata kama hana shida imagine anakopa anaenda kutowa watu out au basi anaenda kula tu basi tukaona huyu anatupotezea muda tukamtowA
So Sad tunakoelekeaaa
 
Hiyo haiwezi kutokea kwangu hiyo pesa yake anatakiwa anunue japo mafuta yake au atumie saluni sio kuniomba mimi hivyo vitu wakati ana pesa.

Nyie ndo wahongaji wakuu mnasababisha wanawake wanadanga na kusema kwa nini waolewe wakati wanapata pesa ya kutosha,kwamba ndoa ni umaskini kwao

Naomba nikukanushe kua
Sipendi na wala sijawaza kuhonga bado
Pesa yangu naitafuta kwa jasho mkuu
Ila wajibu unabaki kua wajibu
Kama sivyo usiowe
 
Habari za jumapili wana Jamii Forum

Leo naomba nizungumze kidogo na hawa wenzetu upande wa Kiume mana miaka ijayo kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi

Siku izi ni kawaida kabisa kukuta mdada anauza matunda, anatembeza mtumba, anachoma mandazi ubuyu na juice na mengine mengi ya kuingiza kipato, huko kwenye vikoba ndo usiseme wanawake wameamua kutafuta hasa tofauti na zamani

Lakini upande wa pili kuna uvivu na kujisahau ambapo trend ikiendelea hivi kuna hatari kubwa mbeleni
Wanaume hasa hawa wanaojiita graduate mnapotea kaka zangu, najua mmesoma bodaboda mnaona si hadhi zenu tena, saidia fundi pia siyo hadhi yenu kuuza matunda siyo hadhi yenu mmebaki mnatembea na bahasha kutwa kutafuta kazi, ebu ndugu zangu acheni u brazamen wa kishamba, jichanganyeni hakuna pesa inakuja kukugongea mlango lazima tu uitolee jasho kidogo, mbona wadada wazuri tu wanajishughulisha??

Kuna mtoto wa ndugu yangu alifikia kwangu ili aende interview jamani anaamka saa tano akiamka anaamka na laptop na muvi, anakunywa chai anaendelea na muvi mchana anakula anaendelea na muvi narudi nyumbani nipo hoi bin taaban yeye hata kuoga ajaoga,saa mbili na nusu tunakula dinner ndo anamwambia dada akampashie maji ya kuoga [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi huyu mtu hata akipata kazi si mzigo huu??????

Huu ni mfano lakini wanaume wa aina hii ni wengi sana

Wakati ambapo dunia ipo busy kuimpower mtoto wa kike hebu Wazazi wekeni juhudi kidogo na kwa watoto wa kiume, wajitambue na kuwafundisha kufanya kazi kwa mikono yao wenyewe.

Ni aibu sana


Huyo hata akija kuoa mkewe atapata tabu sana atataka afanyiwe kila kitu hata sawa ya mswaki awekewe kwenye mswaki wenyewe. Wamefanya na ndoa zimekuwa ngumu
 
Tatizo kubwa lipo kwenye jamii sio vijana.. yani kijana akimaliza chuo akaendesha bodaboda au kufanya Kazi ya saidia fundi watu wengi huanza kusema vibaya kumchukulia kama kitendo cha kwenda shule alipoteza muda.. na hakuna maarifa aliyo yapata ya ziada tofauti na walio baki mtaani hii kitu sio kizuri kwenye jamii yetu, na ndo kimefanya vijana wengi wajifungie majumbani.

Yani ili nchi iendelee inatakiwa tujifunze kuwasifia watu wanao kujituma kufanya Kazi kwa bidii hata kama ikiwa ni Kazi ya kuzibua choo.. na kingine pia tujifunze kwa nchi zilizo endelea.

Jamii yetu inaona kama mtu ukimaliza kusomea Uhandisi ukaenda kulima au kujiajiri katika fani tofauti unakuwa umepotea.. kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinacho kwamisha vijana ni majungu kutoka kwenye jamii.

Mfano niulize tu.. ni wazazi wangapi wataruhu mwanao aliesomeshwa kwa gharama mpaka chuo akawe bodaboda,saidia fundi, au hata kuwa mpishi mgahawani?? Wazazi kama mpo humu naomba mjibu kwa uwazi kabisa [emoji1488]
We ndio umenena
 
Maisha ni magumu aisee

SIJUI TUNAPO ELEKEA

UNADEGREE UKISAIDIA FUNDI WADHARAULIKA


BINAFS SIJAL VYET VIPO KABATN

NAJIKUTA NAWAJENGEA WANA NYUMBA

AMBAO SIWAELEW NI WA AWAKE TU
 
nimejaribu kufikiri tu.......sasa kuna haja gani kijana aende shule kwa maana kuanzia form six mpaka chuo kikuu halafu akirudi mtaani tunataka awe saidia fundi...sasa si bora tufute hizo elimu watu wasome mwisho form four au wasisome kabisa....?...

Sijui umefanya utafiti wapi na kujua ratio ya wanaume wapambanaji vs wanawake wanapambanaji na kuitolea maamuzi dhidi ya wanaume....hapa natofautiana na wewe...shida iko kwa jamii nzima kwa maana kuna shida kwa jamii yetu si kwa akina dada wala wanaume....huku mitaani idadi ya wanawake wadangaji na wauza K imekuwa kubwa kupita kiasi....binafsi naamini hawa ndio wengi kuliko wanaume wanaozagaa zagaa bila kujishughulisha...

Naamini tatizo sio hawa vijana, tatizo liko kwenye mifumo....ni aibu kwa nchi masikini kuwa na vijana wasio na kazi na wanazagaa mitaani...hii ni aibu yetu sote...vijana wengi kama nguvu kazi wanatafuta tu hela ya kuishi kwa maana kula kulala, wengi masikini hawana future....
 
IMG_20210511_004441.jpg
 
Back
Top Bottom