A
Anonymous
Guest
Sisi ni Kikundi cha Vijana wa Kusoma Mita za Maji katika Wilaya ya Mtwara, kilichosajiliwa kisheria na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani chini ya Ofisi ya Mkurugenzi.
Kikundi chetu kilipata fursa ya kuidhinishwa na Mamlaka ya Maji Mtwara (MTUWASA) kutekeleza kazi ya kusoma mita za maji kuanzia Agosti 2023 hadi Juni 2025. Hata hivyo, mkataba wetu ulisitishwa mwezi Juni 2025 kufuatia maelekezo ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.
Wakati MTUWASA inasitisha mkataba huo, tulikuwa na malimbikizo ya malipo ya zaidi ya miezi mitano. Kutokana na hali hiyo, MTUWASA ilisaini makubaliano ya maandishi ya kulipa deni hilo ndani ya kipindi kisichozidi miezi minne, kuanzia Julai hadi Oktoba 2025.
Pamoja na makubaliano hayo, hadi sasa, Oktoba 2026, hatujalipwa malimbikizo yetu. Hali hii imetuumiza kiuchumi na kutuweka katika mazingira magumu, licha ya kuwa tulitekeleza majukumu yetu kwa uaminifu.
Tumefanya jitihada mbalimbali za kufuatilia haki yetu kupitia ngazi tofauti za uongozi, lakini hadi sasa hatujapata suluhisho. Tumewasilisha malalamiko rasmi katika ofisi na mifumo ifuatayo:
Tulitekeleza kazi hii katika mazingira magumu, tukifanya kazi chini ya jua na mvua. Tulikabiliana pia na malalamiko na matusi kutoka kwa baadhi ya wateja tuliokutana nao mitaani. Hata tulipokuta maji yanavuja, tulijitahidi kusaidia kuzuia upotevu wake, ingawa jukumu hilo halikuwa sehemu ya makubaliano yetu ya mkataba.
Kwa mujibu wa takwimu tunazozifahamu, makusanyo ya MTUWASA yanafikia zaidi ya Shilingi milioni 300 kwa mwezi, huku deni letu likiwa zaidi ya Shilingi milioni 30. Hali hii inazidisha maswali yetu kuhusu sababu za kushindwa kulipa malimbikizo hayo kwa kipindi kirefu, licha ya kuwepo kwa makubaliano ya maandishi.
Tunajiuliza kwa nini watu wengine wanaofanya kazi na Mamlaka hiyo hulipwa kwa wakati, lakini sisi tumekuwa tukisubiri kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu muda wa makubaliano ya malipo ulipopita.
Tunaomba mamlaka husika ziingilie kati suala hili, zifuatilie utekelezaji wa makubaliano yaliyosainiwa na kuhakikisha tunalipwa malimbikizo yetu. Tumeifanya kazi tuliyopewa, na tunaamini tunastahili kulipwa kwa huduma tulizotoa.
Tunaomba sauti yetu isikike na haki yetu ipatikane.
Imetolewa na: Kikundi cha Vijana wa Kusoma Mita za Maji – Mtwara.

- Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
- Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mikindani.
- Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
- Mfumo wa kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Maji.
- Mfumo wa kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Vijana.
- Mfumo wa kidijitali wa E-Malalamiko wa Wizara ya Ajira na Kazi.