Vijana wa miaka 20-29 tukutane hapa

Umeongea points ila ujue muda mwingine mazingira yanam-shape kijana katika zama zozote ziwe enzi za mwalimu ama sasa
 

[emoji5]
 
Umeongea points ila ujue muda mwingine mazingira yanam-shape kijana katika zama zozote ziwe enzi za mwalimu ama sasa
Sahihi nakubaliana na wewe, ni kweli kabisa mazingira kwa namna moja ama nyingine yanambadilisha kijana, ila jambo la msingi ni kwa namna gani kijana anatumia "kubadilika huko kwa mazingira" kujikwamua hapo alipo...yaaani kimaendeleo huku akijua wajibu, thamani na majukumu katika jamii inayomzunguka?
Kuna wanaoishi mazingira magumu lakini wanapambana wanafanikiwa vizuri...na cha kushangaza kingine ni kuwa unakuta kijana amezungukwa na fursa nzuri/kedekede/lukuki lakini bado suala la kufanikiwa kwake inakuwa ni mtihani...

Suala la mazingira lisiwe kikwazo katika kutimiza majukumu yetu labda tu endapo kunakuwa hakuna namna ambayo itamfanya asisogee kutoka pointi moja hadi nyingine.
 
Kaka katika ubora wako.[emoji5]
 
Mbona naona komenti za wazee nyingi walengwa kama akina Mimi hatuonekani
 
Kaka katika ubora wako.[emoji5]
Ndiondio Dada yangu mpendwa...najaribu kutoa kile nilicho nacho labda huenda kuna watakaojifunza..

Kama na wewe una chochote, tafadhali usisite kutushirikisha kwa maana tuko hapa kwa lengo la kujifunza

Karibu sana..
 
Ndiondio Dada yangu mpendwa...najaribu kutoa kile nilicho nacho labda huenda kuna watakaojifunza..

Kama na wewe una chochote, tafadhali usisite kutushirikisha kwa maana tuko hapa kwa lengo la kujifunza

Karibu sana..
Nitarudi
 
Umenena vyema mkuu,na hapo kwenye kuchagua kazi ni kitu ambacho vijana wengi imekua kama ndo desturi yao,tena unakuta ni kijana msomi tu mwenye elimu yake,hapa nadhani ni kutokana na mfumo wa elimu wanayopata mashuleni
Huku mashuleni/vyuoni masomo mengi yanamuelekeza mwanafunzi/msomi kua akimaliza masomo ataajiriwa iwe serikalini au sekta binafsi,mwanafunzi huyu anapomaliza na kuingia mtaani mambo yakabadilika anakua hawezi tena kufanya kazi nyingine tofauti na kazi ya ofisini,hivyo atabaki kuzunguka mtaani tu.

Laiti elimu zetu hizi zimgekua zinatusaidia kupambana na hali mtaani,vijana wengi wangekua wameshatambua wajibu wao kwa familia,jamii na taifa zima,mana wangetafuta fursa za kujiajiri na kuachana na fikra potofu kwamba msomi lazima akae ofisini.
 
Nianze kwa kusema you are what you eat...you become what you study...... Tuchukulie mfano kijana amesoma course ya ualimu, automatically huyu kijana atahitaji shule afundishe.

Hivyo basi ili kumkomboa huyu kijana, inabidi tubadilishe mfumo wa elimu...ambao utaweza kumwandaa kijana kupambana na changamoto za suala la ajira.
 
Umemaliza kila kitu.Nafikiri somo la ujasiriamali lingetiliwa mkazo kuanzia ngazi za chini huku mashuleni,ili mwanafunzi akue akitambua kuna njia mbadala tofauti na elimu ya darasani ambayo itamkomboa,kuliko kukaa tu nyumbani au mtaani kwa kutegemea au kusubiri serikali imuajiri.Mfano huyo huyo kijana kasoma course ya ualimu lakini bado kakosa ajira,kama alipata msingi wa kua mjasiriamali tangu chinu kwa vyovyotr hawezi kukaa kizembe mtaani/vijiweni na kuishia kupiga soga
Lazima atachakarika kwa faida yake,familia yake na taifa kwa ujumla,na hapo ndipo tutasema huyu kijana amejitambua na ameujua wajibu wake
 
kwakweli bado nasoma ila kwa jinsi ninavyoiwaza kesho yangu na Tz ya leo nakosa matumaini na elim yangu kabisa
 
kwakweli bado nasoma ila kwa jinsi ninavyoiwaza kesho yangu na Tz ya leo nakosa matumaini na elim yangu kabisa
Inabidi wakati unasoma ..pia ujishughulishe na ujasiriamali...biashara au ufugaji. Hii itakusaidia ukimaliza kusoma, utajua wapi pa kuanzia.
 
Ingekuwa vema kama mngeenda kukutanikia fesibuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…