Je,vijana tunatambua thamani yetu,wajibu wetu pamoja na majukumu yetu katika ngazi ya familia,jamii na Taifa kwa ujumla!?
Asante kwa swali zuri, jibu hapo linaweza kuwa ndio na upande mwingine hapana..
Nasema ndio kwa sababu kuna baadhi ya vijana wanajua majukumu yao, wajibu na thamani katika ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla..na hii inatokana na misingi ya malezi waliyoyapata kutoka kwa walezi wao...pia elimu waliyopata imewasaidia kujitambua na kujua wajibu wao ni nini...Mathalani leo hii kuna vijana ni nguzo kubwa kwa familia (wanategemewa) kutokana na kuwa waliona fursa na wakazifanyia kazi. Kazi wanayofanya inasaidia kukuza familia, jamii na hata taifa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo... Misingi mizuri ya malezi ya maisha imewafanya wawe bora na mfano wa kuigwa katika jamii yetu tunayoishi kwa hiyo utaona ni jinsi gani wanatimiza majukumu yao na wajibu huku wakiilinda thamani yao...
Kwa upande wa HAPANA PIA, naweza kusema pia kuna ambao (baadhi) hawajajua thamani, wajibu na majukumu katika familia,jamii na taifa kwa ujumla..
Leo hii tunashuhudia vijana wengi wakichagua kazi, kuishi vijiweni kupiga soga na kuishia kuilalamikia serikali kila kukicha..Wao ni kula kulala tu, yaani wapowapo... Wengi wao ni "Fuata mkumbo" na ndio husababisha kukithiri kwa tabia hatarishi kama utumiaji wa madawa ya kulevya, ukahaba na ujambazi..ila laiti kama wangebadili fikra na kuumiza kichwa haya mambo mabaya tusingeyasikia kamwe na ninaamini vijana tungeamka na taifa lingesonga mbele kwa maana kama ujuavyo VIJANA NI TAIFA LA LEO NA NGUVU KAZI YA TAIFA...
Kwa hiyo kwa kumalizia, ningependa kuwaasa vijana tuamke, tuache ukorofi na tuchape kazi kwa sana.. Utandawazi usitupumbaze tukajisahau kabisa...
Tuwe na maadili mazuri ili vizazi vijavyo vijifunze mema kwa manufaa ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla kimaendeleo...
Asante...