Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Wote mlio above 30's mliwahi pita huu umri wa 20's......Nyie mkiwa kwenye 20's mlifanya nini mpaka saivi mnapata ujasiri wa kuwasagia kunguni madogo? Acheni unafiki Watanzania wote ni maiti kabla na baada ya uhuru
UKISOMA KATIKATI YA MISITARI UTAKUTA MIAKA HAPA INAHUSU GEN X,GEN Y NA HIYO GEN Z.
 
Yaani mtu mzima mwenye miaka 40 anamuagiza mtoto wa miaka 20... Mtakuja kutuambia tugombee na urais... Ya Kenya waachieni wao nyie mlishindwa kutengeneza njia acheni laana ya RUSHWA na undugu bila kusahau ufisadi itunyooshe
 
Tz kilichobaki ni kuomba Mungu tu apatikane kiongozi shupavu... Kama Magufuli japokuwa wengine hawakumkubali ila in real kwa hali ambayo nchi ilifikia alijitoa sana... Ukisema uvunje vunje CCM unakufa siku chache tu...
 
Tanzania kumejaa maiti TU!
 
Hamia Kenya.
 
Usilinganishe mtu mwenye njaa na asiye na njaa. Vijana wa Tanzania Wana uhakika wa chakula, kusoma bure elimu ya msingi na sekondari na chuo wana uhakika wa kupata mikopo ya vyuo vikuu
Mtanzania gani hana njaa? Yupi ana uhakika wa kupata mkopo?

Hii nchi ni ya wajinga na wapumbavu full stop. Hakuna la zaidi!
 
Hapo
 
Tanzania ni nchi ya amani. Kila kitu kizuri kinapatikana Tanzania. Ya nini kujihangaisha kama Kenya?
Mna amani or mna pretend amani?
wanacholinganisha ni society norms, wakati wenzetu wakiwa serious na nchi yao hapa wako serious na nini? Unategemea ufisadi utaisha kwa jamii hii? Viongozi wabovu wasio waadilifu?
Uchumi weak?
 
Swali langu wakikaa pembeni? Wanadhani nani ataitoa nchi hapo kama si wao?
 
Vijana wa Tz wengi ni watumwa wa vyama vya siasa mawazo yao hayako huru ukiwaweka hapa wajadili maslahi ya taifa utawaona wanaanza kujadili kwa muelekeo wa vyama vyao na fikra za mwenye kiti..
 
TV channel zetu zinachambua tu soka siasa aahh.
Vyombo vya habari vimekaa kichawa tu na watangazaji wanawinda nafasi za uteuzi hakuna namna wanaweza kuleta challenge kwa serikali. Hata ikitokea kuna uchambuzi wa kisiasa basi mgeni lazima aongee kwa kusifiasifia.
Watawala wanafurahia hali hii ya kusifiwa tu lakini hawajui ni kwa namna gani wanaua taifa la kesho. Muda si mrefu kati ya miaka 10 hadi 20 kutoka sasa, tutakuwa tunaongozwa na kizazi cha chawa ambao tumewalea wenyewe. Enzi hizo watakuwa wameshika hatamu ktk nyadhifa kubwa hapa nchini hivyo uchawa wao utapelekwa kimataifa.
 
Kuna watu wataanza kunielewa sasa pale niliposema kunamwaka watanzania watakuwa slave wa waAfrica wenzao.

Nilifikia kuzungumza hivi baada ya kuona level ya kiasi cha ujinga kwa watanzania.

Ukikuta mtanzania amesoma na hafuatilia maujinga ya mpira, Bongo movies nk basi utamkuta kichwani uelewa ni mdogo na ameajiliwa mahala analipwa mshahara anakula analala kwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…