Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Wote mlio above 30's mliwahi pita huu umri wa 20's......Nyie mkiwa kwenye 20's mlifanya nini mpaka saivi mnapata ujasiri wa kuwasagia kunguni madogo? Acheni unafiki Watanzania wote ni maiti kabla na baada ya uhuru
UKISOMA KATIKATI YA MISITARI UTAKUTA MIAKA HAPA INAHUSU GEN X,GEN Y NA HIYO GEN Z.
 
Yaani mtu mzima mwenye miaka 40 anamuagiza mtoto wa miaka 20... Mtakuja kutuambia tugombee na urais... Ya Kenya waachieni wao nyie mlishindwa kutengeneza njia acheni laana ya RUSHWA na undugu bila kusahau ufisadi itunyooshe
 
Tz kilichobaki ni kuomba Mungu tu apatikane kiongozi shupavu... Kama Magufuli japokuwa wengine hawakumkubali ila in real kwa hali ambayo nchi ilifikia alijitoa sana... Ukisema uvunje vunje CCM unakufa siku chache tu...
 
Vijana wa miaka 20s wako CitizenTV muda huu wakijadili masuala yanayohusu nchi yao, na wanafanya hivyo kwa weledi mkubwa sana.

Vijana wa miaka 20s wa Tanzania hawajui chochote na wala hawaelewi chochote kuhusu mambo ya siasa na mustakabali wa nchi yao.

Ukimuuliza kijana wa miaka 20s juu ya mahusiano ya siasa na maisha yake utaona anaanza kuelezea makalio ya Poshi Queen, kitovu cha Yammy, na maisha ya wasanii wengine.

Vijana wa Tanzania wako bize kufuatilia Simba na Yanga, "connection", madanga, uchawa na ujinga mwingine.
Tanzania kumejaa maiti TU!
 
Hamia Kenya.
 
Usilinganishe mtu mwenye njaa na asiye na njaa. Vijana wa Tanzania Wana uhakika wa chakula, kusoma bure elimu ya msingi na sekondari na chuo wana uhakika wa kupata mikopo ya vyuo vikuu
Mtanzania gani hana njaa? Yupi ana uhakika wa kupata mkopo?

Hii nchi ni ya wajinga na wapumbavu full stop. Hakuna la zaidi!
 
Vijana wa miaka 20s wako CitizenTV muda huu wakijadili masuala yanayohusu nchi yao, na wanafanya hivyo kwa weledi mkubwa sana.

Vijana wa miaka 20s wa Tanzania hawajui chochote na wala hawaelewi chochote kuhusu mambo ya siasa na mustakabali wa nchi yao.

Ukimuuliza kijana wa miaka 20s juu ya mahusiano ya siasa na maisha yake utaona anaanza kuelezea makalio ya Poshi Queen, kitovu cha Yammy, na maisha ya wasanii wengine.

Vijana wa Tanzania wako bize kufuatilia Simba na Yanga, "connection", madanga, uchawa na ujinga mwingine.
Hapo
 
Tanzania ni nchi ya amani. Kila kitu kizuri kinapatikana Tanzania. Ya nini kujihangaisha kama Kenya?
Mna amani or mna pretend amani?
wanacholinganisha ni society norms, wakati wenzetu wakiwa serious na nchi yao hapa wako serious na nini? Unategemea ufisadi utaisha kwa jamii hii? Viongozi wabovu wasio waadilifu?
Uchumi weak?
 
Taka taka kabisa wengi machawa tupu kutwa wanawaza teuzi tu wakipewa mike wanaropoka vijana wajiajiri hapo yy kaedit umri ana 74 kaandika 49 ili aendelee kufanya kazi alipwe 540k za Kila mwezi

Vijana sio kwamba hawaelewi nini kinachofanyika na madhaifu ni yapi, madogo wanajua kuliko hivi vizee venye pressure na kisukari....ila madogo wamekaaa pembeni baada ya kuona siasa za Tu bado hazijapevuka watu wapo kupiga pesa, kufanya propaganda ili watimize ndoto zao
Swali langu wakikaa pembeni? Wanadhani nani ataitoa nchi hapo kama si wao?
 
Vijana wa Tz wengi ni watumwa wa vyama vya siasa mawazo yao hayako huru ukiwaweka hapa wajadili maslahi ya taifa utawaona wanaanza kujadili kwa muelekeo wa vyama vyao na fikra za mwenye kiti..
 
TV channel zetu zinachambua tu soka siasa aahh.
Vyombo vya habari vimekaa kichawa tu na watangazaji wanawinda nafasi za uteuzi hakuna namna wanaweza kuleta challenge kwa serikali. Hata ikitokea kuna uchambuzi wa kisiasa basi mgeni lazima aongee kwa kusifiasifia.
Watawala wanafurahia hali hii ya kusifiwa tu lakini hawajui ni kwa namna gani wanaua taifa la kesho. Muda si mrefu kati ya miaka 10 hadi 20 kutoka sasa, tutakuwa tunaongozwa na kizazi cha chawa ambao tumewalea wenyewe. Enzi hizo watakuwa wameshika hatamu ktk nyadhifa kubwa hapa nchini hivyo uchawa wao utapelekwa kimataifa.
 
Kuna watu wataanza kunielewa sasa pale niliposema kunamwaka watanzania watakuwa slave wa waAfrica wenzao.

Nilifikia kuzungumza hivi baada ya kuona level ya kiasi cha ujinga kwa watanzania.

Ukikuta mtanzania amesoma na hafuatilia maujinga ya mpira, Bongo movies nk basi utamkuta kichwani uelewa ni mdogo na ameajiliwa mahala analipwa mshahara anakula analala kwisha.
 
Back
Top Bottom