Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Tanzania na Kenya ni Chongo na Kipofu respectively
Kenya is more than 10 times corrupt to Tanzania. Mbaya zaidi corruption zenyewe za Kenya ziliasisiwa 1960s na viongozi waandamizi waliorithi ul'wa toka kwa Waingereza
Mbaya ya zaidi ya zaidi corruption yenyewe ilikuwa based on land grabbing
Ukiangalia sana Ruto is not a sole problem, he is part and parcel of the problem
Umewasifia wa Kenya kwamba ni mahiri wanazungumza wakijiamini. Lakini ukiangalia sana wao wanazungumzia zaidi juu ya dalili za tatizo na sio mzizi wa tatizo la Kenya. Wanachezeshwa comedy na akina Odinga, Uhuru na Ruto. Mzizi wa tatizo la Kenya ni land grabbing by fewer politicians

Katika uzalishaji the mother of all resources is Land, sasa Kama over 50% of Kenya's is owned by Kenyatta Family unatarajia nini ?
Nakuunga mkono, Wakenya wanakumbuka shuka kumeshakucha. Matatizo yalianza utawala uliopita kwa kenyata. Ruto ama Sakayo kama wanavyomuita amepewa nchi tayari imejichokea. Nchi haikopesheki tena inabid ategemee mapato ya ndan na grants ili ajenge mashule, hospitali na mirad mingine ya huduma za kijamii. Ruto ana mapungufu ila hakua na namna zaid ya kuwakamua wananch(taxation).

Point yangu kubwa, kama wakenya wangeshtuka tangu enzi za kenyata wasingefikia hapo. Na kuharibu miundo mbinu ni kama wanajikomoa wenyewe, ni jasho lao ndo wanalichezea hapo.
Anyway yote niliyoandika sio excuse yakwanin generation zote za watz hatuungan kupinga kwapamoja kabla mambo hayajachachamaa.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kasoro unasema vijana wetu hawajitambui hapo ndio napata shida kidogo
Kama wapo vijana hapa wanao jitambua, sijawaona wakijitokeza mbele watambulike. Siyo lazima kujitokeza kwa fujo, la hasha. Kuna njia nyingi sana sasa hivi za kujitambulisha wanakosimamia. Mbona wengi wao wanajitambulisha tena kwa madaha mengi, kuwa wao ni 'CHAWA'?

Hata hao wa Kenya wanao sifiwa sasa, hawakujitambulisha kwa fujo, hizo fujo zimeingizwa na makundi mengine toka nje. Sasa hivi vijana wenyewe ndio wanaoonekana kwa kusema/kuzungumza.
Hapa umemsikia nani akizungumza tu!

Sijasema hawapo, lakini waliopo watalaumiwa kwa ukimya wao wakati nchi yao inakwenda mrama.
 
Sio Tanzania pekeee hata Ulaya na Marekani vijana wana utofauti sana na wazee wao waliochuma mali na kujenga nchi zao kwa kazi ngumu,vita,maradhi na ufukara.
Factor zipo wazi
1.Malezi
2.Elimu
3.Mfumo wa nchi

4.Jambo zuri hawana stress ni bora kiafya.
Umeegemea kona ya kipekee kidogo hapa ambayo inaibua mjadala mkubwa katika hali ya kawaida.

Hivi ni kweli vijana wa hapa hawana 'stress'? Unawaangalia vijana wapi hasa; machinga/bodaboda, au vijana ambao baba zao ndio waendesha nchi?
Hivi unaweza kweli ukawalinganisha vijana wengi wa hapa na wa kule majuu Ulaya; 'seriously'?

Sasa wa hapo jirani Kenya wao imekuwaje wakawa tofauti na hawa wa hapa? Wao hali zao ni duni zaidi kuliko hawa hapa Tanzania?

Hapo katika 'factor' ulizo orodhesha, nachukua tu hiyo ya "elimu." Elimu yetu imekuwa siyo ya kumfungua akili mwanafunzi. Mkazo umekuwa zaidi katika kukariri ili afaulu mitihani, basi. Elimu ya namna hiyo haisaidii sana.
 
Kwani hao vijana wa Kenya, walikuta mifumo siyo kandamizi? Mbona wao wanapambana lkn vijana wa TZ wamekalia kubeti na kudanga tu?
Katiba ya Kenya inawalinda raia wake tofauti na hapa hivi.

Hallelujah!!!
 
Katiba yao iko vizuri.Mabosi wa askari ni wananchi wa mitaani na siyo watawala.wapiga kura ndiyo wanawaweka madarakani viongozi na vijana wa gen z wamewafuta kazi Baraza la mawaziri na IGP,wamemwambia Rais kuwa hawana imani na Baraza lake la mawaziri na Mkuu wa jeshi la polisi.
Vijana wa tz sina uhakika kama wanaelewa mapungufu ya katiba, wengi ni wabinafsi,chawa wa baadhi ya viongozi.kazi yao ni kuwatia hofu na kushabikia kwa ahadi za teuzi.
Tz wateule Rais wanaweza kutishia wapiga kura kukamatwa na kuwekewa rumande bila kosa lolote na baada ya siku tatu ukaachiliwa bila maelezo.Hapo ndipo inakuja tofauti kati gen z wa Kenya vs Tz
 

Vijana wa miaka 20s wako CitizenTV muda huu wakijadili masuala yanayohusu nchi yao, na wanafanya hivyo kwa weledi mkubwa sana.

Vijana wa miaka 20s wa Tanzania hawajui chochote na wala hawaelewi chochote kuhusu mambo ya siasa na mustakabali wa nchi yao.

Ukimuuliza kijana wa miaka 20s juu ya mahusiano ya siasa na maisha yake utaona anaanza kuelezea makalio ya Poshi Queen, kitovu cha Yammy, na maisha ya wasanii wengine.

Vijana wa Tanzania wako bize kufuatilia Simba na Yanga, "connection", madanga, uchawa na ujinga mwingine.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo 😳🙌
 
Wote mlio above 30's mliwahi pita huu umri wa 20's......Nyie mkiwa kwenye 20's mlifanya nini mpaka saivi mnapata ujasiri wa kuwasagia kunguni madogo? Acheni unafiki Watanzania wote ni maiti kabla na baada ya uhuru
In Mzee Kenyatta voice 😅😅😱 R.I.P
 
Wazee wa bongo jau sana 🤣🤣🤣
Hiv wakati wazee wa kenya wanapigania katiba mpya, wanapigania kuitoa KANU, niny mlikuwa mnafanya nn?

Msijifanye mnasahau upuuzi wenu
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo 🙌
 
Achen kila mtu adili na maisha yake vile anaona yeye inafaa. Msilazimishe vujana wabkitanzania wawe kama wakenya, haiwezekani
 
Wewe ukiwa na miaka 20 ulifanya nini kwa ajili ya nchi yako? Au nyie mnaowaponda vijana hamkupita kwenye ujana? Hawa vijana wa miaka 20 walijizaa wenyewe? Huwa nashangaa sana watu kuiona Kenya kama nchi fulani hivi ya ahadi wakati ni nchi iliyojaa ukabila na kuchukiana. Pia sera zao za kibepari zimesababisha uchumi wao wote kumilikiwa na familia chache. Kenya walishajivuruga tangu wanapata uhuru. Acheni upumbavu wa kujidharau mbele ya Kenya.
Mama samia punguza hasira.

Hata huku kwetu uchumi unamilikiwa na wachache..mfano familia ya kikwete, makamba na sasa wewe mama samia unamleta mwanao ale keki ya nchi.
 
Back
Top Bottom