Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Vijana wa miaka 20 Kenya wanajadili mustakabali wa nchi yao kwa weledi mkubwa sana. Vijana wa Tanzania wanakwama wapi?

Ngoja tubeti kwanza kaka, maana kazi zinazolipa TZ kwa sisi vijana ni 3 tu
1. Kubeti
2. Uchawa
3. Kulikamata jimama au jibaba lenye mpunga.
 

Vijana wa miaka 20s wako CitizenTV muda huu wakijadili masuala yanayohusu nchi yao, na wanafanya hivyo kwa weledi mkubwa sana.

Vijana wa miaka 20s wa Tanzania hawajui chochote na wala hawaelewi chochote kuhusu mambo ya siasa na mustakabali wa nchi yao.

Ukimuuliza kijana wa miaka 20s juu ya mahusiano ya siasa na maisha yake utaona anaanza kuelezea makalio ya Poshi Queen, kitovu cha Yammy, na maisha ya wasanii wengine.

Vijana wa Tanzania wako bize kufuatilia Simba na Yanga, "connection", madanga, uchawa na ujinga mwingine.
Huku tuna mjadili Magoma.
 
Mnatuonea buree aya nyie vijana wazaman mliongelea tz aya mamb yanafata mkundo mle mle........🤣🤣kwan kumwagiana tulitoa wapi skwenu nyie vijana wazaman🤣🤣🤣🤣 au ndio mnatuanguxhia mizigo tuuy
 
Wazazi wao hawajitambui pia. Maana wajinga wa leo ndo genZ ya miaka iliyopita.
Wewe umeongea ukweli tupu.
Tunawalaumu bila kuangalia mtoto anajifunza tabia na mazoea flani toka kwa wazazi, walezi, wakubwa zao na jirani wanao mzunguka
 
Shida sio vijana, shida ni mfumo wenu huo ambao haueleweki, ujamaa sio ujamaa, ubepari sio ubepari.

Waulizw wakina abdul nondo walivo jaribu kujifanya ni vijana wanao taka kuhoji kipi kiliwakuta? Je unazani kila kijana anaweza kufanya hiyo sacrifice?

Lazima tukubali kama hatuwezi kufanya siasa safi, hakuna sector itabaki salama, kuanzia kilimo, elimu, afya, mapenzi nk
 
Huku uwaambie kula kimasihara, kupigania katiba aaah
Mkuu tukipigania katiba tunapigwa risasi na kuswekwa ndani n no body cares, na shida bado ziko pale pale.

Sasa tusijifariji hata kwa kula mbususu 😀 hapana kwa kweli.
 
Kila mtu analalamika hii nchi 🤣🤣 yeye hafanyi anategemea wengine wafanye
 
Tz kilichobaki ni kuomba Mungu tu apatikane kiongozi shupavu... Kama Magufuli japokuwa wengine hawakumkubali ila in real kwa hali ambayo nchi ilifikia alijitoa sana... Ukisema uvunje vunje CCM unakufa siku chache tu...
Manabii hua hawakubalikia kwao.

Mimi nilikua na pinga sana baazi za sera za Magu. Lkn alikua sahihi kwenye mambo mengi tu na nilitamani amalize miaka yake 10
 
Vijana wa Tanzania wao wanajua tu kuwa mama anaupiga mwingi.
Wanatumia muda mwingi kuongelea mpira wa timu za Dar tu.

nadhani tatizo ni elimu; vijana wengi wa Kenya wana elimu nzuri kuliko vijana wa kitanzania. Kwa mfano msululu wa Rais samia wa magari 156 pamoja na safari za nje zisizokuwa za lazima huku mikopo ikonezeka wakati wananchi wanaambiwa walipe ushuru, tozo na kodi lukuki ama sivyo wahamie Burundi ni mambo ambayo hayangekubaliwa na vijana wa kenya, lakini watanzania hata hawajui bajeti yetu ilikuwa na tozo zipi mpya
 
Itoshe kusem kwamba vijan wa tz wapo sahih ila wazee na watu wazima ni useless katika maendeleo ya nchi
Sisi vijana tukisema tuandamane, hatuandamani kuchapa viongozi.

Inabidi tuchape hao wazee viboko, mapaka waseme wametufikishaje hapa.

Wazee wameua viwanda vyote alivo anzisha nyerere ili sisi tukose ajiria alafu wanaona poa tu.

Kiukweli ninyi wazee mnamengi sana ya kutuelezea sisi vijana wenu kabla hamjaanza kutulaumu.
 
Engineer anamlalamikia daktari, daktari anamlalamikia mwalimu, na mwalimu anamlalamikia mwanasiasa.

Mwishowe kazi kubwa inayofanyika hapa ni kulalamika tu

Kila mtu anaona mwenzake hafanyi wajibu wote ni kulalamika toka juu hadi chini 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom