Vijana wa Rorya wamuenzi Baba wa Taifa kwa kushiriki katika Bonanza la Nyerere Day

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Katika kuenzi miaka 24 ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka ameandaa bonanza la michezo mbalimbali kwa vijana wilayani hapo.

DC Chikoka anasema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuendeleza kutoa elimu na mwamko kwa vijana kukumbuka na kuenzi yote mazuri aliyoyafanya Muasisi wa Taifa letu Hayati Julius Nyerere.

Bonanza lilianza na jogging na baadaye kuwa mechi za mpira wa miguu kwa Wanawake na Wanaume.

DC amesisitiza kuendeleza umoja, mshikamano na uzalendo kama njia ya kumuenzi Baba wa Taifa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…