benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na TAWA limewakamata watu wawili waliotambulika kwa majina ya Richard Paulo (Miaka 23) na Masiaya Lais (Miaka 19) katika kijiji cha Minjingu katika hifadhi ya Jamii ya Burunge wilayani Babati wakiwa nyara za serikali ambazo ni nyama ya Twiga inayokadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni 30 pamoja na silaha mbalimbali zikiwemo bunduki mbili aina ya Gobole pamoja na pikipiki inayotumika kubeba nyamapori.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amesema watu hao walikamatwa tarehe 14/2/2023 majira ya saa 8 za mchana.
Pia ameendelea kufafanua kuwa katika hifadhi ya Jamii ya Makame iliyopo kijiji cha Ndedo wilayani Kiteto askari polisi kwa kushirikiana na askari wanyama pori walimkamata mtu mmoja anayeitwa Meshaki Mohammed (54) akiwa na nyama ya Twiga anayekadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni 30 pamoja na silaha aina mbalimbali ikiwemo visu pamoja na unga wa baruti.