Vijana wadogo wakamatwa kwa ujangili, waua Twiga

Vijana wadogo wakamatwa kwa ujangili, waua Twiga

Wale wauzao zinazopanda ndege wao ndio Wana hatimiliki ya kuila keki ya Taifa pekee.yaani hawa mapolisi bana wanaonea tu wasio na mbavu. Kuna ufisadi wa kufa mtu Ila hawawakamati wahusika
We unawafahamu?
 
Marehemu Babu yangu mzaa baba alifariki akiwa na miaka around 108....
Alifariki 2006
Maana wakati wa vita ya kwanza ya Dunia WW1
Yeye alikua anatambua kilichokua kinaendelea....
Alikua ananipa story nyingi sana za ki maisha aliwai kunisimulia Kuna jamaa siku wamekula twiga for the first time wakawa wanasema LEO TUMEULA WA TWIGA
Kwa maelezo ya marehemu Babu twiga ana nyama tamu sana...

Wa Tz walianza kula twiga zamani sanaaaa
Binadamu walianza kula kila kitu zamani sana sio Twiga tu
 
Kuwafunga sio suluhisho!!!

Juhibu TAWA na Tanapa pamoja na Wilaya. Kushirikisha jamii ya Mdori, Minjingu Vilima Vitatu..kaeni mjadili kwa KINA

Kwa uzoefu wangu katika eneo hilo kuna Changamoto kubwa sana kwenye kunufaika na Mapato ya WMA kuhusisha jamii ya mtu moja moja.....wachache ni WANUFAIKA

Hao watoto wahukumiwe ki Jadi kuhusisha wazazi....kuwamangelepaa sio suluhisho
Wahukumiwe kijadi, kwa sheria ya wapi?
 
Wange deal na mapapa wa hio biashara Ina uzunisha hao watoto wa ki maskini kua VESSEL (mbuzi wa kafara)

Japo Sheria hainaga huruma na ni msumeno.....

Na shaur hao vijana waachiwe huru for any means na wasaidie KATIKA kuumaliza mtandao wa wawindaji haramu....

Inasikitisha mtoto kwenda kutumikia miaka miaka 30 Kwa kuua Twiga mmoja.....nashaur hao watoto wange pewa training na kutumika kama ANT-POUCHING TZ AMBASSADOR.....
Umesema vyema, sheria haina huruma
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na TAWA limewakamata watu wawili waliotambulika kwa majina ya Richard Paulo (Miaka 23) na Masiaya Lais (Miaka 19) katika kijiji cha Minjingu katika hifadhi ya Jamii ya Burunge wilayani Babati wakiwa nyara za serikali ambazo ni nyama ya Twiga inayokadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni 30 pamoja na silaha mbalimbali zikiwemo bunduki mbili aina ya Gobole pamoja na pikipiki inayotumika kubeba nyamapori.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amesema watu hao walikamatwa tarehe 14/2/2023 majira ya saa 8 za mchana.

Pia ameendelea kufafanua kuwa katika hifadhi ya Jamii ya Makame iliyopo kijiji cha Ndedo wilayani Kiteto askari polisi kwa kushirikiana na askari wanyama pori walimkamata mtu mmoja anayeitwa Meshaki Mohammed (54) akiwa na nyama ya Twiga anayekadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni 30 pamoja na silaha aina mbalimbali ikiwemo visu pamoja na unga wa baruti.
View attachment 2526214
do! madogo wameiua TANESCO? umeme ukikatika wanahusika
 
Back
Top Bottom