SoC01 Vijana, wafanyakazi, wanafunzi na vizazi vijavyo vinaangamia kwakushindwa kuelewa maana halisi ya neno "Elimu"

SoC01 Vijana, wafanyakazi, wanafunzi na vizazi vijavyo vinaangamia kwakushindwa kuelewa maana halisi ya neno "Elimu"

Stories of Change - 2021 Competition

Moses nyambeya

New Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Nawasalimu wana jamiiforums, haswa jukwaa hili pendwa la "stories of change" naimani nyote ni wazima.

Ujumbe huu unalenga kusaidia jamii yote hususani vijana, wafanyakazi, wanafunzi na vizazi vinavyo kuja.Ili kujua maana halisi ya neno "elimu" na kuacha upotoshwaji mkubwa unao toka kwa wazazi wetu, serikali yetu na jamii kiujumla unaopelekea vijana kukosa ajira, wanafunzi wengi kupata elimu ambayo baadae inashindwa kutoa mchango chanya kwenye maisha yao na kuishia kupoteza muda wao mwingi pia wafanyakazi wengi wa serikali na sekita binafisi kuishia kuishi maisha ya shida Sana wawapo kazini na wanapo sitafu au kuachishwa kazi wanaishia kuwa omba omba na wengine huenda mbali na kujitoa uhai kabisa.

Nitaenda kutoa ufafanuzi juu ya maana ya neno "elimu" , makundi ya elimu, ushauri kwa jamii na serikali juu ya elimu

1.MAANA YA ELIMU
Unapo zungumuzia neno elimu watu wengi mawazo yao huwapeleka moja kwa moja shuleni au vyuoni mfano hujawahi kukuta mzazi anamrudisha mtoto shuleni zaidi ya mara tatu sababu tu hajafauru darasa la saba au kidato cha nne, hii sumu tumemezeshwa Sana na wazazi wetu na sekita ya elimu kiujumla kuwa mtu akifeli shuleni hawezi kuwa na elimu nyingine itakayo msaidia kufanikiwa kimaisha.

Nini maana ya elimu?
Elimu: nivitu au mambo yote unayo jifunza siku zote za maisha yako,mtu anaweza kukutana na mambo mengi Sana siku za maisha yake hayo mambo yanaweza yakawa mazuri au mabaya ila kwa pamoja hutoa elimu.
Watu wengi wanashindwa kutambua maana halisi ya neno elimu hiyo imepelekea wasomi wengi wa ngazi mbalimbali za utaalamu huwa wakimaliza masomo yao hujiona kuwa wamepata elimu ya kutosha na hawapaswi kuongeza elimu yoyote siyo hao tu hata wafanyakazi, vijana hata hawazezi kusoma kitabu hata kimoja cha kumuongezea maarifa Wala kuhuzuria mafunzo yoyote yale baada tu ya kumaliza ngazi tofauti za taaluma au kuajiliwa

2. MAKUNDI YA ELIMU
(i)Elimu ya kutoa ujinga(scolastic education)

Hili kundi la elimu hufundisha juu ya kusoma,kuandika na kuhesabu.Hata tukiweka kumbukumbu vizuri mwalimu Julius kambarage nyerere alisitiza Sana juu ya hii elimu ili ituondoe ujinga
Aina hii ya elimu hutolewa kuanzia ngazi ya shule za awali yaani chekecheya hadi kidato cha sita (form six) naomba ufikilie kwa kina hivi ukimaliza kidato cha sita unaweza kwenda kuomba wapi kazi? Kiujumla huna tofauti na darasa la saba au kidato cha nne wote mnaaina moja ya elimu kitu ninacho shukuru kwa Tanzania kundi hili la elimu limeboreshwa kiasi watu wengi wamepata aina hii ya elimu na wazazi wametilia mkazo Sana juu ya kundi hili la elimu

(ii)elimu ya utaalamu (professional education)
Hili ni moja Kati ya kundi la elimu ambalo hutoa mafundisho juu ya taaruma flani mfano udakitari, ualimu, ufundi cherehani, ufundi magari kundi hili la elimu hutolewa na ngazi zote za vyuo kuanzia ngazi za chini mfano veta hadi vyuo vikuu. Aina hii ya elimu naweza kusema ni elimu ya biashara kwa sababu taaluma uliyo ipata katika kundi hili unaenda kuiuza badae unalipwa mfano mzuri mwalimu anaweza kuuza taaluma yake kwa serikali badae mwisho wa mwezi unalipwa mshahara fundi wa magari anauza utaalamu wake kwa kutengeneza gari badae analipwa.
Sasa shida iko hapa tena kubwa Sana vijana wanalia hamna ajira siyo kweli bali tu wamechagua taaluma ambazo haziuziki mfano ukiwa unauza nyanya mbovu nani atazinunua ko wito wangu kwa vijana kabla haujaamua kuchukua utaalamu( professional) wowote lazima utambue kuwa hiyo taaluma yako badae inahitajika iuzike ni biashara na kama ukigundua haiuziki ni bora ukafanye mambo mengine kabisa
Changamoto nyingine kwenye kundi hili la elimu limefanya watu wengi kutumia kipawa kimoja tu mfano wewe ni dakitari unaamini huwezi fanya kazi nyingine zaidi ya udakitari huu ndo ujinga tunao jazwa kutoka kwenye kundi hili la elimu

(ii) Elimu ya fedha
Kundi hili la elimu hutoa mafundisho juu ya unatafutaje pesa, unatumiaje pesa zako,unawekezaje pesa zako.Kundi hili la elimu watu wengi hawapendi kulitilia mkazo lakini ndo kundi linaloweza kumfanya mtu akafanikiwa bila kuwa na aina nyingine ya elimu mfano haujawahi kuta mtaani kwenu unaambiwa mtu flani hajasoma lakini ndiye taajili wa mtaa hii yote ni kwasababu ya kuwa na aina hii ya elimu vijana wengi, wafanyakazi, wamekuwa wahanga wa kukoswa aina hii ya elimu mfano unakuta mfanya kazi wa serikali anasitafu ndipo anajenga nyumba ya kuishi au anasitafu anamiliki nyumba ya kuishi na gari tu vijana na wanafunzi pia hawatilii mkazo aina hii ya elimu na wazazi huwa wakali endapo mtoto akionekana anafatilia aina hii ya elimu huenda mbali zaidi na kusema wanaweza kuwa na maadiri mabaya mbeleni hii ni sumu kubwa kwenye jamii yetu

(iv)Elimu ya utambuzi (self development education)
Hili ni kundi la elimu ambalo humsaidia mtu kujua vipaji alivyo navyo, malengo yake, kuweka mipango yake, kujua haki zaki, nini afanye nini asifanye katika maisha yake.
Aina hii ya elimu niyamuhimu Sana hata ukiwa na makundi mengine ya elimu usipokuwa na hili kundi na elimu unakuwa kama bendera upepo unapo vuma unaenda huko huko unaweza ukakuta mtu anakaa sehemu bira faida yoyote zaidi ya miaka kumi (10) huko kote nikushindwa kuwa na kundi hili la elimu unaweza ukakuta msomi amesoma lakini anashindwa kutumia fulsa zinazo patikana katika jamii yake, unaweza ukakuta mtoto au kijana ana kipaji mzazi au yeye mwenyewe anashindwa kukikuza kwa kukosa kundi hili la elimu.

(v) Elimu (mafundisho) ya kimungu.
Kundi hili la elimu limesahaulika Sana lakini linamaana kubwa kwenye maisha ya kila siku kundi hili la elimu hupatikana kupitia mafundisho mbali mbali yaliyo tolewa na watumishi mbali mbali wa Mungu na kuandikwa katika vitabu vitakatifu biblia na kolohani. Hutolewa kupitia misikiti na makanisa mbali mbali tambua mtu anaweza asiwe na aina hizo zingine za elimu Ila akawa na aina hii na maisha yakaenda
Elimu hii ni ya muhimu Sana na inafaa jamii kwa ujumla kuipata inamchango mkubwa katika maendeleo na mafanikio.


Ushauri kwa jamii na serikali juu ya elimu

Kupitia andiko hili nadhani utakuwa umefunguka kimtazamo juu ya maana ya neno "elimu" na hii itasaidia jamii kuondokana na mitazamo hasi juu ya swala la elimu

Ushauri wangu kwa jamii, jamii kiujumla lazima ichague elimu sahihi ya kuwapatia vizazi vyao ili kuondokana na maisha tegemezi na maisha yasiyo kuwa na tija yoyote kutokana na elimu tunazopewa lazima tuchague elimu sahihi kulingana na dunia tuliyopo kwa sasa.

Ushauri wangu kwa serikali: Serikali itoe uwanja mpana kwa watu binafisi na sekita binafisi kutoa mchango wa uboreshaji wa elimu itakayo leta tija kwenye nchi yetu mfano mwanafunzi anasoma darasa la Kwanza Hadi kidato cha sita (form six) kalibia miaka 20 mda huo hana utaalamu ( professional) yoyote na makadilio ya WATANZANIA kuishi ni miaka 45 happy amebakiza miaka 25 ondoa miaka mitatu Hadi minne ya kusoma chuoni amebakiza miaka 20 hii itaenda kuleta shida Sana serikali ibadilike elimu ya utalaamu ianze kutolewa hata baada ya darasa la saba kwa wale watakao hitaji mengine haya nimizunguko tu mfano unasoma Nutrition ukiwa kidato cha pili alafu unasoma Nutrition ukiwa chuoni kwenye Anatomy tutazungushana Hadi lini?

Mwisho: Nawashukuru kwa kusoma andiko hili ambalo litaenda kubadili maisha yako na vizazi vyako vijavyo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom