Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
CCM itashinda huu uchaguzi kirahisi sana, kwa sababu muundo wa tume ya uchaguzi, na jinsi katiba ilivyo havitoi mwanya wa asiye madarakani kushinda u rais!!
Hivyo naungana na ww Pasco kusema kwamba CCM itashinda!!
Binafsi nilitamani JPM ashinde kwa ushindi finyu wa angalau 51% labda pengine ingeweza kumbadilisha na kufanya vizuri zaidi kuliko awamu iliyopita!!
Wapinzani kama kweli wanataka mabadiliko, basi waanze na kupigania badiliko la katiba kwanza. Lasivyo watakuwa wakilia kila mwaka kuwa wanaonewa!!

Hii dhana ya “wapinzani” sijui inaelewekaje nchini? Ninavyojua ni kuwa ni juu ya Watanzania kuamua wanataka nini si viongozi wala makada wala wanachama. Hicho ni kikundi kidogo sana. Wao kwa wingi wao ndio wanaoweza kuidhibiti serikali iliyoko madarakani.
Kama wengi wao wanapendelea “status quo” basi utawala wa CCM utaendelea tu. Ndio takwa lao. Rejea asilimia 80 ya Nyalali. Na hakuna atakayeweza kufanikiwa katika kupigania mabadiliko yoyote iwe ya katiba, uongozi, n.k. kwani wananchi watakuwa “hawataki” mabadiliko.
Kwa kifupi, hakuna kitu kama “wapinzani” kinachoweza kuwepo nje ya Watanzania wengi. Opposition can’t exist in a vacuum. Hivyo, vyama vya upinzani vikishindwa kihalali kwenye uchaguzi huu basi ni wazi kuwa ajenda yao haijakubaliwa na Watanzania wengi. Lakini vikionewa, basi ni Watanzania wengi ndio watakuwa wameonewa. Itakuwa ni jukumu la hao Watanzania wengi kupigania haki yao; sio kunyooshea vidole viongozi wa vyama vya upinzani.