Uchaguzi 2020 Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu, Wajiunga Pamoja Kuikampenia CCM, Watumia Basi Maalum, CCM Campaign Bus, Kufikia Wengi, Wasaidia Sana CCM Kuvuna Kura!

Uchaguzi 2020 Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu, Wajiunga Pamoja Kuikampenia CCM, Watumia Basi Maalum, CCM Campaign Bus, Kufikia Wengi, Wasaidia Sana CCM Kuvuna Kura!

Wanabodi,

Katika pita pita yangu mitaa ya jijini Dar es Salaam hii suku ya nwisho ya kampeni, nimekutana na Basi maalum la kampeni ya CCM, nilipouliza, ndipo nikajulishwa hao ni
vijana wahitimu wa vyuo vikuu, wameamua kujiunga pamoja kuunda kikundi cha CCM Campaign Bus ili kuikampenia CCM, kwa kutumia basi maalum waliloliita "CCM Campaign Bus", basi hilo wakati wa rush hours, linapita mabarabari kuangazia roots zilizoelenewa, na kusaidia kusafirisha bure abiria, ku supplement usafiri wa dala dala, hivyo kuwafikia watu wengi, wa kawaida ambao hawapati muda wa kuhudhuria kampeni.

Basi hili la CCM Campaign Bus, limeisaidia sana CCM kufahamika hivyo kuvuna kura kibao.

Wasikilize vijana hawa

Paskali
Paskali Hao ni vjana wahitimu wanaokula mema ya nchi hii. Nimetafakari inawezekanaje wahitimu wanaosota mitaani na kuendesha bodaboda huku vieti vikioza waende na bus kunadi nini

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
JPM MITANO TENAAA

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Leo umedhihirisha kichwani hamna kitu umeshindwa hata kutafautisha neno root na route.Kumbe nyie watu wengine tunapoteza muda kubishana na nyie kumbe akili zimeshawatoroka
 
Sasa nimemuelewa mh. rais Dr John Pombe Joseph Magufuri ,pale alipotoa maana rasmi
ya jina Mayala.
Nawatakia kampeni njema.
 
Hao watakuwa wanachuo chako mwenye njaa mwenzao, wanachuo wana Jambo lap kesho. Kawadanganya ajira mpaka Sasa hajizitoa anasubiri aapishwe awatukane na kuwapa majembe wakakime kijijini!!!
 
Wanabodi,

Katika pita pita yangu mitaa ya jijini Dar es Salaam hii suku ya nwisho ya kampeni, nimekutana na Basi maalum la kampeni ya CCM, nilipouliza, ndipo nikajulishwa hao ni
vijana wahitimu wa vyuo vikuu, wameamua kujiunga pamoja kuunda kikundi cha CCM Campaign Bus ili kuikampenia CCM, kwa kutumia basi maalum waliloliita "CCM Campaign Bus", basi hilo wakati wa rush hours, linapita mabarabari kuangazia roots zilizoelenewa, na kusaidia kusafirisha bure abiria, ku supplement usafiri wa dala dala, hivyo kuwafikia watu wengi, wa kawaida ambao hawapati muda wa kuhudhuria kampeni.

Basi hili la CCM Campaign Bus, limeisaidia sana CCM kufahamika hivyo kuvuna kura kibao.

Wasikilize vijana hawa

Paskali

Katikati ya giza la ubaguzi wa mikopo kwa wanachuo waliosoma shule binafsi,bila kujali kuwa waliipunguzia serikali mzigo,tena katikati ya riba kubwa ya mikopo ya wanachuo,watu wanazidi kupumbazwa kabisa!
 
CCM kama wakirudi madarakani na ukakosa uteuzi basi uje una Nuksi ya bundi sio kwa jitihada hizi we jamaa.
 
CCM itashinda huu uchaguzi kirahisi sana, kwa sababu muundo wa tume ya uchaguzi, na jinsi katiba ilivyo havitoi mwanya wa asiye madarakani kushinda u rais!!

Hivyo naungana na ww Pasco kusema kwamba CCM itashinda!!

Binafsi nilitamani JPM ashinde kwa ushindi finyu wa angalau 51% labda pengine ingeweza kumbadilisha na kufanya vizuri zaidi kuliko awamu iliyopita!!

Wapinzani kama kweli wanataka mabadiliko, basi waanze na kupigania badiliko la katiba kwanza. Lasivyo watakuwa wakilia kila mwaka kuwa wanaonewa!!
Kama matokeo kwenye vituo vya kupigia kura hayatabandikwa inammaanisha hapo kuna bao la mkono
 
Mnamo mwaka 2015 JPM alijipigia chapuo sana kuwa ni Rais wa wanyonge. Sikuelewa sana, nikasema ngoja nijipe muda nione.

Baada ya mwaka mmoja tu nikaona dalili za wanyonge kuumizwa sana, huku akidai ananyoosha nchi. Sikuelewa!

Hapa chini nakudadavulia mambo ambayo yanaonesha JPM alivyowafukarisha hoi bin taaban hata wale waliokuwa nacho kidogo.

1. Aliongeza makato ya bodi ya mikopo (HESLB) kutoka 8% hadi 15% kila mwezi
Mshahara hajaongeza hata tone, anadai anajenga reli, na kununua ndege. Hivi jamani, Rais hujaongeza mshahara wa mtumishi, unaongeza vipi makato? Naombeni mnisaidie kushangaa! Mshahara hutaki kuongeza, bado unawaongezea makato kweli?

Chini ya JPM, aliyekuwa anapokea laki 3, kwa makato haya amefanywa kupokea laki 1 na pointi.

(maskini amekuwa fukara, hoi bin taaban).

2. Alipandisha kilo ya sukari kutoka 1,800/- ya jk hadi sh. 2,500/- au zaidi
Wananchi wakiwa wanyonge vile vile kaingia kazuia kuingizwa sukari, bila hesabu wala maarifa. Matokeo yake sukari ikapungua, bei ikashuti. Kaanza kukimbizana na watu ma-godown huko. Ovyo kabisa!

Mwisho wa siku anatangaza eti bei elekezi eti sh. 2,500/- Nisaidieni kushangaa!

Hivi umekuta bei 1,800/- kwa kg, yeye jpm miaka miwili tu ikawa mara mbili sh. 3,000/-

Yani iko hivi hela ambayo maskini alikuwa ananunua kg 2, leo ananunua kg 1 tu imeisha.

(waliokuwa maskini amewafanya mafukara, hoi bin taaban)

3. Alizuia minada ya mazao kama mbaazi, korosho, ufuta n.k.
Akawapekekea jeshi watu wa kusini kuchukua korosho zao. Matokeo yake, bei ya mbaazi ikashuka kutoka sh 1500/- kwa kg hadi sh. 200/- kwa kg zikakosa wanunuzi, hasara kwa maskini.

Korosho zilivyobebwa hakuna ajuaye. Jeshi kwenye mambo ya kiraia, huwezi kuhoji. Wengine wakaishia kuambiwa korosho zao zilikuwa eti mbovu. Mpaka leo hawana kitu. Hawana hela na uendelezaji wa mashamba msimu mpya umekuwa mgumu.

(maskini mkulima amefanywa fukara, hoi bin taaban)

4. Bomoa bomoa ya nyumba DSM (Kimara), na huko Moro bila fidia kwa sheria ya mwaka 1938/50.
Huyu JPM aliacha sheria za miaka ya 80, za road reserve kuwa mita 60. Akachukua sheria ya kikoloni road reserve mita 120.

Kabomoa mpaka ambako barabara haitapita. Waliokuwa na nyumba, wakabaki nje na maskini hatari. Kwa maisha yale yale

(maskini akafanywa, fukara hoi bin taaban)

5. Hatoi ajira
Toka ameingia madarakani ni madaktari elfu 3 na ushee na walimu baadhi wa sayansi ndio waliajiriwa.

Yani mzazi kasomesha mtoto, kwa kujikamua, enzi za jk walimu walikuwa hawaombi ajira, ilikuwa ukimaliza ualimu degree, au cheti/diploma, unasubiri kupangiwa kituo. Ukatae mwenyewe kazi. Ila leo soma, maliza ng'ombe za wazazi, na kazi JPM hatoi.

(maskini amekuwa fukara zaidi, hoi bin taaban)

6. Hakuwajengea walioharibikiwa nyumba na tetemeko la Kagera pamoja na kukusanya michango kila pembe ya dunia.
Maskini wa Kagera, akaambiwa hajaletewa tetemeko.

(maskini akawa fukara, hoi bin taaban)

7. Kikokotoo cha pensheni ya wastaafu.
Akaleta kikotoo eti ukistaafu zile hela ulizohifadhi, upewe kiduchu. Yani ufanye kazi miaka 60, uzeeke. Wkt unataka hela yako, jpm anasema chukua kiduchu. Huko nyuma wastaafu walikuwa wanapewa mara moja 75% ya hela , yeye akasema wapewe 25% tu.

(hapa maskini mstaafu anapunguziwa hata jasho lake la kwenda kupumzikia). Fukara, hoi bin taaban.

8. Kahawa huko kagera alikuta wanauza kilo 2500/-, kazuia wa Uganda wasije kuinunua. Ikashuka bei hadi sh 1000/-

Maskini akawa fukara zaidi, hoi bin taaban chini ya JPM.

Kwa ufupi:
Wakulima hoi bin taaban
Wafanyakazi hoi bin taaban
Wastaafu hoi bin taaban
Waliomaliza vyuo hoi bin taaban
Wafanyabiashara hoi bin taaban
Wavuvi hoi bin taaban

Eti huyu anataka mi5 tena!! Afanye nini?

Huyu ni rais wa wanyonge gani?

Ongezea wengine walio hoi bin taabani
 
Pascal Mayalla, time is a factor of production. Hao vijana wa CCM ni jobless, time wasters, muda wa kufanya kazi wanazurura, na wewe msomi nguli wa habari na Sheria unafurahia.
Rasilimali muda ikipotea huipati Tena, Bora uooteza pesa lakini si muda.
Huu muda wa kuwatafutia madaraka wenzao watakuja kuulilia siku moja.
Kampeni zinaisha na wanarudi kwenye msoto wao wa Kila siku.
CCM imeahindwa kubuni vyanzo vipya vya ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu, elimu ya Kati na ya chini.
CCM ni bug time failure
Uwe unatumia Akili kwa hiyo wanaopiga Kampeni kwa ajili ya kina lissu wote hawana Ajira Hukufuatilia wakati Obama Anagombea vijan wakivyojitolea kumtafutia kura Memzidiwa Maarifa na CCM tulieni Sawa Ziwaaingie TANO TENA
 
Wanabodi,

Katika pita pita yangu mitaa ya jijini Dar es Salaam hii suku ya nwisho ya kampeni, nimekutana na Basi maalum la kampeni ya CCM, nilipouliza, ndipo nikajulishwa hao ni
vijana wahitimu wa vyuo vikuu, wameamua kujiunga pamoja kuunda kikundi cha CCM Campaign Bus ili kuikampenia CCM, kwa kutumia basi maalum waliloliita "CCM Campaign Bus", basi hilo wakati wa rush hours, linapita mabarabari kuangazia roots zilizoelenewa, na kusaidia kusafirisha bure abiria, ku supplement usafiri wa dala dala, hivyo kuwafikia watu wengi, wa kawaida ambao hawapati muda wa kuhudhuria kampeni.

Basi hili la CCM Campaign Bus, limeisaidia sana CCM kufahamika hivyo kuvuna kura kibao.

Wasikilize vijana hawa

Paskali

Hao ni wahitimu wa vyuo vikuu waliokariri definition ya "Catalyst" kama baba yao Mzee Meko a.k.a Mfalme Juha!
 
Kesho ndio siku maalumu kuweka historia ya kuifungasha virago CHADEMA na Lissu Mkoa wa Dar es salaam kuwapiga chini Wagombea wake wote kuanzia wa Urais ,Ubunge na Udiwani

Dar kesho tutaiongoza Mikoa mingine kumfungasha virago mbelgiji Tundu Lissu Dar hadi aigope akisikia Dar presha iwe inampanda kwa kukumbuka kipigo cha kura alichal
CCM Jimbo la Ubungo mmelikosa kweupee peee
 
Back
Top Bottom