kiuchumi,
nadhani sote ni mashahidi,
kila kona ya nchi kuna ujenzi wa miundominu ya hususani ya barabara na reli ya SGR, ili kurahisisha bidhaa, huduma na watu kusafiri kwa urahisi na haraka kutoka eneo moja hadi jingine.
Sambamba na hilo,
usafiri wa anga, usafiri wa majini, usafiri wa reli na barabara ni nafuu sana na ni wa uhakika zaidi kuliko wakati mwingine wowote tangu tupate uhuru.
Huduma za umeme, maji safi ya kutosha kwa shughuli za viwandani na kilimo ni vya uhakika kila mahali.
Mazingira mazuri ya biashara, masoko ya kisasa yapo kila mahali nchini na hili limechochea pakubwa uwekezaji na ubia katika kila sekta za kiuchum.
Kijamii,
kuna mageuzi makubwa sana kwenye upatikanaji wa huduma za afya kute nchin, maboresho katika sekta ya elimu ni ya kiwango cha juu sana na yanafanya elimu ya Tanzania kua bora zaidi Africa.
Suala la amani, ulinzi na usalama Tanzania limeendelea kua kichocheo na kivutio kikubwa cha utalii na shughuli za biashara kufanyika usiku na mchana.
Kisiasa,
yapo mabadiliko na mageuzi makubwa sana katika sheria hususan katika tume huru ya taifa ya uchaguzi na zile sheria za uchaguzi wenyewe, nandio maana hivi sasa mpaka wafungwa walio magerezani wanaweza kushiriki kupiga kura, lakini pia wakurugenzi wa halmashauri kuwekwa kando kama wasimamizi wa uchaguzi na badala yake mtumishi yeyote wa umma anweza kupewa jukumu hilo na tume ya taifa ya uchaguzi.
Tanzania leo hii hali ya kidemokrasia ni nzuri zaidi ukilinganisha na nchi yoyote Africa Mashariki.
Na haya ni kwa uchache sana tu gentlena