Vijana wanaojiunga na UVCCM wakiwa vyuoni badilikeni, acheni uchawa

Vijana wanaojiunga na UVCCM wakiwa vyuoni badilikeni, acheni uchawa

nkize000

Member
Joined
Dec 3, 2020
Posts
5
Reaction score
5
Viajana wengi wana mawazo ya CCM iwasaidie sio wao waisaidie CCM, ndio maana unakuta wanajiunga wengi na akibaatika kupata nafasi atapiga hela, yaani hata ngazi za chini wanaiba hata hela ya kadi.

Anawaza kuwa nikimaliza nitaajiriwa au connection ya ajira nitaipata kupitia chama. Hana mchango wowote positive kusaidia chama.

Hata taasisi inakupa interview ijue una nini cha kusaidia taasisi ili na yenyewe ikusaidie.

Ndio wanakuja hadi kwenye makampuni wanawaza mishahara hawana hata idea ya kusaidia hizo taasisi zikue. Wanawaza wamalize chuo, waitwe kazini, wapangiwe majukumu kama maroboti!

Sipingi wala sikosoi, ila nawashauli tubadilike tuache uchawa. Nenda na fikra za kusaidia chama kwanza na wenye malengo haya wamefika mbali.
 
nchi ilipofkia sasa Kila kijana anawish akae kwenye mizani sawasawa, angalau jina ling'ae kwenye ripoti ya sieji.
 
CCM imezeeka...

CCM Taifa limewashinda.

Vijana wanaangaliaa fursa tu. Full kulamba miguu na nonino ya wakubwa ili mradi kupata riziki.

Mtaani kunamsemo tunatumia chukua kadi ya CCM mapema upate asali na maziwa/Teuzi na Ajira.
 
Back
Top Bottom