Vijana wanaoongozana na wachezaji uwanjani wakati wa ufunguzi wa mechi wana kazi gani?

Vijana wanaoongozana na wachezaji uwanjani wakati wa ufunguzi wa mechi wana kazi gani?

Ni amri ya mungu tukaijaze dunia kwa hiyo kila mchezaji anatakiwa aingie na mtoto ili watu wakumbuke kuijaza dunia.....
 
Kuacha hao wanaojibu kimizaha

Wale watoto wengi wao ni Academy Player

Lengo kubwa ni kutoa hamasa ya kimichezo kwa kizazi kijacho

Pili kujengewa waweze kujiamini mbele ya hadhira wanapoonesha vipaji vyao

Kukumbusha haki za watoto

Pia ni kuonesha au kutambua vipaji vipya vya soka
 
Jumapili njema kwa kila mmoja wetu.

Ndugu zangu Nina jambo naomba kuuliza ukitazama mechi za ulaya kuna wale watoto ambao wakati timu zinaingia uwanjani wanakuwa wameongoza wa wachezaji hadi ndani ya pitch.nataka kujua wale watoto wanafanya kazi gani?

Natanguliza shukrani za dhati kwenu
Shughuli yao inaweza kuonekana ni ndogo lakini, ina umuhimu mkubwa sana kwa utamaduni wa soka na kisaikolojia pia.
Kwani husaidia kuboresha mazingira ya michezo kwa urafiki, mshikamano, na kuonesha heshima.
Na kwa watoto, ni nafasi ya kipekee ya kujifunza maadili ya michezo na kushiriki katika matukio makubwa ya kimichezo.
Kuwapo kwa watoto hao ni ishara ya kueneza maadili ya michezo, urafiki, na usawa kati ya wachezaji wa timu pinzani.

Kazi yao!
Hali ya uwepo wa watoto husaidia wachezaji kupunguza shinikizo kabla ya mechi muhimu. Inaleta mazingira ya kirafiki na furaha.
Inawahamasisha watoto wadogo kushiriki zaidi na michezo, kuwafanya waone ndoto zao za kuwa wanasoka ziko karibu.
Hupatikanaje?
Vilabu vingi huandaa mashindano au bahati nasibu kwa watoto wanaotaka kuwa sehemu ya tukio hilo.
Baadhi ya watoto ni wa familia za wafadhili/wadhamini au huchaguliwa kupitia makampuni yanayofadhili/ kudhamini mechi hizo.
Watoto wa mashabiki waaminifu au wanachama wa klabu wanapewa nafasi hizi.
Wakati mwingine hutoka vikundi maalum kama shule, vituo vya watoto yatima, au watoto wenye mahitaji maalum hupata nafasi hizi kama ishara ya msaada na mshikamano.

Ova
 
Jumapili njema kwa kila mmoja wetu.

Ndugu zangu Nina jambo naomba kuuliza ukitazama mechi za ulaya kuna wale watoto ambao wakati timu zinaingia uwanjani wanakuwa wameongoza wa wachezaji hadi ndani ya pitch.nataka kujua wale watoto wanafanya kazi gani?

Natanguliza shukrani za dhati kwenu
Wanafanya kazi ya kuongozana na wachezaji
 
Borussia Dotmund hili wameliweza sana,wanaingiaga na watoto kibao na hata wakati mwingine wachezaji wa timu kubwa kucheza na vitoto kama kuwafurahisha tu
 
Labda ni vijana wa football academy wale, wanafundisha mchezo wa mpira wa miguu
 
BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALITUTAJIA MAADUI.

1. UMASIKINI
2.UJINGA.
3. MARADHI.

Akasema Hawa ni maadui wa kweli kweli katika hili Taifa.

LEO 2024 BAADA YA MIAKA 60 TUMEKUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI.

2024 maadui wameongeseka Zaidi kuliko wale watatu wa 1961.

1.Umasikini na ufukara.
2.Ujinga na upumbavu.3.Magonwa na Maradhi
4.Mmomonyoko wa Maadili.
ushoga, usagaji Kamali, sugar mamy, sugar Dady mashangazi
5 AJIRA
5. Rushwa na Upendelo

6. USimba na u yanga.
7. Mitandao ya kijamii Tiktok, x, nk
8. Manabii wa uongo na Mashehe Uchwara.
9. Ajali nyingi mno.
10. Gharama kubwa za maisha, ujenzi holela nk

MAMBO NI MENGI SANA VIJANA WA KITANZANIA WANAWAZA MAMBO YA HOVYO SANA SIMBA NA YANGA ZINATAWALA MIKEKA NK.

OKOENI TAIFA LENU LEO.
MKIFIKA MBINGUNI MTAHOJIWA NA MUNGU MLILIFANYIA NINI TAIFA LENU NIMEMALIZA.
Utekaji
 
Back
Top Bottom