MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nchi nzima kama sio dunia nzima kwa sasa kilio kikubwa ni vijana kudai hawana "connections" za kupata malisho mazuri. Connections za ajira, biashara au hata ufadhili wa masomo. Mimi nimejitolea kuwakumbusha vijana mambo kadhaa ya muhimu ili kujiweka kwenye mazingira ya kushikwa mkono na wanaoweza kufanya hivyo. Huu ushauri wangu sio sheria kwamba lazima ufuatwe. Kijana kama unataka mafanikio yakufuate zingatia sana yafuatayo;
1. ANZA NA MUNGU
Kwa imani yako mtangulize Mungu. Hakuna mcha Mungu ambaye ataachwa aaibike. Hapa simaanishi ndo uwe mfuasi wa Mwamposa au wanaotajwa kuwa manabii. Mche Mungu kwa mujibu wa kitabu chako kitakatifu.
2. HAKIKISHA KUNA MAELEWANO KATI YAKO NA WAZAZI/WALEZI
Ukiweza kwenda sawa na wazazi utabarikiwa sana. Najua kuna wazazi saa nyingine ni kama wanawachokoza watoto ila wewe jitahidi uwe mjanja kwenda nao sawa. Wazazi ni wadhaifu mno kwa watoto wao hivyo ukiwa kama mtu mzima jitahidi kuwasoma wanachotaka na wasichokitaka. Baraka za wazazi ni za muhimu kwenye haya mapambano. Halafu hawa watu wenye connections ndo hao waliosoma na wazazi wetu hivyo wakati mwingine unaweza kumwona mzazi wako kapigika kumbe kuna best yake wa zamani akimpigia simu moja tu unashangaa unaitwa kwenye kitengo fasta.
3. HAKIKISHA UNAKUWA MFANO MWEMA KWENYE FAMILIA HADI MTAANI KWAKO
Siku hizi wavivu wamejipa jina la INTROVERTS. Kwamba wao hushinda tu ndani. Kijana huwezi pata kazi kama hufanyi kazi. Hakikisha pale nyumbani unapiga kazi kama punda. Usiwe mvivu. Watu wanataka kujua kuanzia nyumbani ukoje. Unaweza kushangaa tu jirani akakukonnect kwenye mchongo wa maana. Shiriki shughuli zote za nyumbani na za hapo mtaani kwenu. Kwa mfano ukitokea msiba jitolee kupiga kazi. Kuna waombolezaji wenye michongo.
4. KUWA MKWELI NA MWAMINIFU
Hili sitaliongelea sana kwa sababu lieleweka. Hata kama unaona uaminifu na ukweli unakushinda pambana uweze kuwa hivyo kwa ajili ya kesho yako iliyo bora.
5. KUWA MSIKILIZAJI ZAIDI
Acha kiherehere jomba. Ukikutana na watu kuwa msikilizaji zaidi badala ya kuleta ujuaji. Hata kama unajua VUNGA kwanza hadi uulizwe.
6. HESHIMU WATU
Hili ni la lazima. Heshimu kila mtu bila kujali kipato wala hadhi yake. Kwa mfano wakati naingia chuo sikuwa na hata hela Tsh 500k ya kulipia usajili. Siku moja napita zangu mtaa aliokuwa anaishi mjomba wangu mmoja aliyekuwa naye ana hali tete sana ya kiuchumi nikaona ngoja nimsalimie. Kwenye stori nikamweleza hali yangu akasema hana hela ila kuna mtu atampigia simu chuo ili nipate usajili. Nilidhani utani ila ndo kilichotokea. Nilipata usajili na kuendelea na masomo.
7. USIWE NA TAMAA
Kuwa na subira. Iwe biashara au ajira jitahidi uache papara. Nenda taratibu kila kitu kitakuwa sawa. Zingatia point namba 4.
8. JIONGEZEE THAMANI
Kwenye kila unachofanya hakikisha kinakuongezea thamani. Hata ukitaka kujiburudisha nenda sehemu isiyoonekana ya kishenzi. Kuonekana maeneo kama Kimboka au Mrina ni kujipunguzia thamani yako. Kuambatana na watu wenye sifa mbaya kwenye jamii inapunguza thamani. Ulevi, uasherati na mambo mengine ya hovyo kuwa nay