A
Anonymous
Guest
Habari watanzania, shukrani za dhati ni kwa Mungu mwenyezi kwa kutupenda upeo hata akamtoa mwana wake wa pekee ili atukomboe kwa wale watakao muamini (yohan 3;16)
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, ya Adha katika usafiri wa dala dala za Temeke-Mbezi na maeneo mengine hasa wakati wajioni.
Kumetokea tabia ya watu hasa vijana katika vituo vya daladala, kipindi ambacho idadi ya abiria ni wengi kuliko mgari, vijana hao hupigania na kuingia katika daladala kama vile nao ni wasafiri ili hali mwishoe huwa ni wauza siti. Yaani yeye anapigania anaingia kwenye gari, akishaingia anauza siti aliyopata kwa mteja ambaye ni abiria husika.
Kwakweli tabia hii inakera sana , kwani katika usafiri huu wanatuletea usumbufu mkubwa sana. Pia, waweza kuwa ni miongoni wa vijana ambao si waaminifu wakawaibia watu, pia tabia hii inaondoa utu na uthamini wa watu wengine ikizingatiwa kuwa wapo watu wa aina mbalimbali wanaoutumia usafiri huu, ambao walihitaji kipaumbele kama vile mama wajawazito, wenye ulemavu na wazee, lakini kwa vitendo vya vijana hawa kugombania kwa nguvu na kuja kuuza siti si cha kiungwana.
Kwanza, hii sijaiona kama ni fursa kwa jamii yetu na kwa uchumi wa nchi yetu, vijana hawa waelimishwe kuwa kuwahi siti na kuiuza kwa sh.500 sijambo zuri bali uvunjifu wa amani na ustaarabu wa kitanzania.
Hivyo tunaliomba jeshi la polisi Tanzania, LATRA, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na wahusika wa usafiri wa Dar es Salaam, kulitatua tatizo hili, kwa kutoa ONYO na katazo pamoja na kupiga faini gari lolote litakaloonekana kutoa fursa kwa vijana wa aina hii.
Mungu awabariki sana
@polisiTanzania
@Latra