mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Mnavobebelea kuajiriwa mnadhan cc ambao hatujaariwa hatuendeshi familia zetu, ajira ni kama kua na mzazi akishadead unapambana kwa kila hali na hakuna lisilowezekana
[emoji23] [emoji23] yaani wewe jamaa umeifanya jioni yangu iwe na kicheko. 9876543210Kwa sera mpya ya awamu hii tuna mfanyabiashara yupo magogoni, usishangae siku anawaagiza polisi waanze kutembeza Karanga na aisikirimu mtaani,
Baki kazini kwanza hadi wanajeshi wamalize opereshen zote, walianzia bureau wakaja korosh sasa sijui wataanza kutembeza line za sim mtaani hawa jamaa?
Dah, mkuu hii comment si mchezo.Kwa sera mpya ya awamu hii tuna mfanyabiashara yupo magogoni, usishangae siku anawaagiza polisi waanze kutembeza Karanga na aisikirimu mtaani,
Baki kazini kwanza hadi wanajeshi wamalize opereshen zote, walianzia bureau wakaja korosh sasa sijui wataanza kutembeza line za sim mtaani hawa jamaa?
Dah, mkuu hii comment si mchezo.Kwa sera mpya ya awamu hii tuna mfanyabiashara yupo magogoni, usishangae siku anawaagiza polisi waanze kutembeza Karanga na aisikirimu mtaani,
Baki kazini kwanza hadi wanajeshi wamalize opereshen zote, walianzia bureau wakaja korosh sasa sijui wataanza kutembeza line za sim mtaani hawa jamaa?
Halafu haya mambo ya kuajiriwa yanategemea mtu na mtu na sio lazima kuacha kazi kama unaona hauwezi maana yawezekana ofisini unapata i.e 2m mpake 3m kwa mwezi hivyo kama kwenye biashara unaweza pata 7-8m baada ya matumizi hapo unaweza acha kazi tofauti na hapo ni shida tupuHapo ndio draft linapoanzia sasa. Kipato cha kila mwezi, kijumuishe mambo ya bima za afya pia.
Kwa mtu uliyezoea kuajiriwa maisha yako yote leo hii unaambiwa tengeneza faida ya 8M kwa mwezi si unaweza kuokota makopo?
Kwa kiwango nnachomfaham General Mangi , najua atatoboa tu. Tatizo safari hii alitaka kuruka kabla hajakomaa vizuri. Kinachomsumbua na kumnyima usingizi ni kiu ya mafanikio na kufanya mambo makubwa. Changamoto zipo lakini haimaanishi hatafanikiwa, hii ilikua ni moja ya sehemu muhimu ya kujifunza.
Kila la kheri Mangi
Ahsante Mkuu,
Napokea heri zote.
Nilijaribu, nimejifunza, bado ninauthubutu.
Jambo moja nna uhakika nalo, utafanikiwa tu, lakini itachukua muda.
Kwa hii shule uliyopita na kama umefanikiwa kupunguza anasa, bata na viwanja muda utazidi kuwa mfupi zaidi.
Waliofanikiwa wote wana discipline ya pesa. Na pesa ina tabia moja, ukiiheshimu na kuithamini, inaweka kambi kwako, ukiikejeli inapeperuka.
Noted tatizo la huyu jamaa hana displiniUlikuwa haujajipanga tu wewe,watu wameacha kazi na wakatusua,sasa unasema wewe ni mtu wa club,totoz unafikiri kwa styles hizo utaweza kufanikiwa?
Mmesahau kuwa aliendekeza starehe pia ,ndo imemla vibaya hivo vitu haviendani na biashara inatakiwa uwe km mchaga,mkinga au mndaliVijana tuna kihemko sana,
Tunataka kwa kipindi kifupi tuwe kama Mo,
Hizi mambo ngoja tuweke kumbukumbu na isaidie kwa wengine
Hakika mkuu,
Ukitaka pesa kubali mambo mengine uwe mshamba tu.
Hii kujifanya alwatan mjini ndo umasikini wenyewe huo.
Nishaweza kuachana na Pombe, kwenda club na anasa zingine.
Nidhamu inahitajika kwa kila jambo.
Nilijifunza kwa maumivu makali mno. Kwenye kabati la nguo kukuta 4M au 5 haikua tatizo, unabadili tairi za gari, unapiga rim mpya, unaweka mziki mnene, mara unabadili sofa, japo ulizonazo bado nzima, ukipita mlimani city wakati huo ndio bado ipo kwenye chati, lazima uondoke na home theater au TV hata kama nyumbani iliyopo haisumbui. Maamuzi ya kukurupuka kuhusu matumizi ya pesa ndio yalikua yanatawala wakati wote.
Kila jambo likija wakati usio sahihi ni shida. Kwanza nilikua under 25, uzuri wanawake na pombe haikua fani yangu.
Nnachosisitiza, kila mmoja ana njia yake, hazifanani. Kuna watu wameajiriwa, wanatengeneza pesa ndefu na wanamiradi inaenda vizuri tu. Kuna watu wamejiajiri, ukikaa nao unaweza kuacha kazi kesho yake. Tukumbuke kila njia au uamuzi una changamoto zake.
Binafsi sijutii hata kidogo,Ungechukua likizo ya miezi mitatu bila malipo na mwezi mmoja wa likizo yako ya mwaka. Miezi minne ingesaidia kuona muelekeo wa biashara.