Hii hoja ni kamili 100%
Mpango wa Mungu ni kumfanya mume awe Juu
Amesema awe kichwa cha familia
mume atumie Jasho kupata mkate mezani
Ila mke ni msaidizi tu!
Katika Biblia
Mwanzo 3:16
Akamwambia mwanamke,
Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako;
kwa utungu utazaa watoto;
na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, NAYE ATAKUTAWALA.
Eti Leo Rais ni mwanamke aisee!!!
Spika nae wanataka awe mwanamke aisee
Hata mkuu wa Majeshi nae ni inshu ya muda tu!
Mungu atusamehe sana hii dhambi!
Marekani pamoja na yote wanajifanya kuwa wana uhuru ila kamwe mwanamke atabaki kuwa nafasi yake ile ile ya chini!
Hillary Clinton alikuwa na sifa zote za kuwa Rais
hiyo ikulu yenyewe ameishi
kashika nafasi nyingi tu nyeti
Ila kuliko USA awe mwanamke wanakaona ni
bora tu Rais awe Trump ambaye walijua huenda hana sifa zozote zile!
coz kwao Urais ni Taasisi na sio sisi huku ambao
Urais ni mtu!
Kifupi hii dhambi imeingia hadi makanisani
Wanawake sasa wanasimama kuhubiri na wana vyeo ndani ya makanisa yao!
Japo mie ni mkristo ila
Hapa Islam itabaki kuwa dini yenye hadhi
Kwa kutambua nafasi ya mwanamke
wanaitekeleza kwa vitendo!
sio sisi wanafiki tunafanya mambo ili Jamii itusifu, ilihali tunajua kabisa kuwa ni kosa mbele ya Mungu.